Tundu Lissu aingia Ngorongoro na kupokelewa kwa kishindo

Tundu Lissu aingia Ngorongoro na kupokelewa kwa kishindo

Acha kupotosha. Hapo sio Ngorongoro. Hizo picha ni za Monduli. Unapata faida gani kudanganya umma?
Tafuta pesa ule maisha na watoto wakali kama viongozi wako wewe, achana na ujira wa Lumumba utakusababishia njaa hadi siku unaondoka hapa duniani

Tafuta pesa.jpg
 
Kinachonirudishaga nyuma kwa Tundu Lisu ni kitendo chake cha kuungana na Acacia na kusema tutashitakiwa MIGA
Mi najiuliza tu ikiwa hao ndiyo watetezi wake siku tukimpa nchi si itakuwa afadhali ya hapa tulipo?

Ni kwamba nchi kweli inahitaji wananchi kusikilizwa ila Sasa nani awasikikize ndiyo pengine tunatuka mkojo yunakanyaga....
 
Kinachonirudishaga nyuma kwa Tundu Lisu ni kitendo chake cha kuungana na Acacia na kusema tutashitakiwa MIGA
Tiririoni 400 uliziona? Makinikia haitoki? Kesi kadhaa za kampuni za madini dhidi yetu tumeshinda? Manufaa ya asilimia 50 kwa 50 ya kampuni ya Twiga umeyaona kwenye ripoti ya CAG?
 
Kinachonirudishaga nyuma kwa Tundu Lisu ni kitendo chake cha kuungana na Acacia na kusema tutashitakiwa MIGA
Ila hushangai huna Noah mpaka leo!!
Hizo bilioni 190 USD mlishalipwa?
Mlisikia vizuri Prof. Kabudi aliposema hatuwadai Acacia Chochote, bali ilibidi wang'ang'anie wanawadai ili wasishtakiwe. Unajua wangeshtakiwa wapi!!
Hivi unajua mkataba ilioingia Serikali na Barrick ni mkataba mbovu kuliko wa kwanza!! Hata siku ile wamefikia makubaliano, ulisikia akisema chochote yule mtendaji mkuu wa Barrick? Ni Kabudi aliyeongea tena kwa kiswahili tu nadhani alijua walichoafikiana ni tofauti na alichotuambia.
Umewahi kusikia taarifa za Barrick zikijadiriwa hata huko bungeni? Kwa taarifa yako ni moja ya masharti waliyopewa Serikali.
Tundu Lisu alikuwa sahihi na ili serikali isiaibike ilikubali yaishe. Unaweza kuachia zile bilioni Dola 190 kirahisi tu, wewe hujiulizi!!!
 
Binafsi Mimi miongoni mwa wanao mkubari mama 90% na choomba mama sela yake ya kugeuza magereza kua vyuo vya ufundi na walimu kutoka Veta na ujenzi wa Veta Kila Kijiji Hayo mambo mengine yakuzidi kutuaminisha watanzania Wote tumeguswa na swala la Bandari sio kweli kwa sababu Ifike mahali Sasa Tumuunge mkono raisi wetu kwa kuhakikisha Watanzania Tunakua na taluma na sio Ubabaishaji.
Point?
 
Nachukua nafasi hii kutangaza kuwadharau watu wote walioshiriki kuhujumu Jambo Tv Online ili ishindwe kuripoti Mkutano Kabambe wa Tundu Ole Lissu alipowahutubia Wamasai, ambao ni wahanga wa kuhamishwa kwenye maeneo yao huko Ngorongoro

Laana ya milele iwaandame wao na vizazi vyao katika maisha yao yote yaliyosalia hapa duniani , Amina

Siasa hizi za kishamba zilizopitwa na Wakati , hazina nafasi tena kwenye nchi hii , tupingane kwa hoja .
Laana ya milele iwaandame wao na vizazi vyao katika maisha yao yote yaliyosalia hapa duniani , Amina[emoji419][emoji375]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom