Tundu Lissu akamatwa na Polisi akiwa Ngorongoro hotel Wilayani Karatu
Ualimu ngazi ipi waliofeli wanasomea?
Pia haujui wale walikuwa wanafaulu vizuri darasa la saba ndo walikuwa wanakwenda form one,waliofaulu wastani walikuwa wanakwenda ualimu.Hata secondary hivyo hivyo wanaofaulu wastani wanakwenda ualimu,wanaofaulu vizuri wanakwenda A level.A level hivyo hivyo.
 
Baadae wengine waliokamatwa na Jeshi hilo ni Mhe. Susan Kiwanga, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe. Catherine Ruge Katibu Bawacha Taifa, Mhe. Twaha Mwaipaya, walinzi wa Mhe. Lissu pamoja na watu wengine.
Nadhani watakuwa wanarejeshwa dar ili waje wapumzike kidogo.
 
TL, Ni mchonganishi na mchochezi anajaribu kuichonganisha serekali na wananchi, huyu ni mtu hatari sana na wa kuogopa kama ukoma,
Naishauri serekali yangu na nimekuwa nikishauri kila wakati, kwamba kila jambo liwe na wakati wake ndio maana kuna wakati wa kula, wakati wa kulala, masaa ya kazi nakadhalika,
HIVYO HATA HIZI SIASA ZIWE NA NYAKATI ZAKE, MIEZI MITATU KABLA YA CHAGUZI HUSIKA, AU KWA CHAGUZI ZA WABUNGE NA URAISI IWE MIEZI SITA KABLA YA UCHAGUZI HUSIKA.
-Hili lisipowekwa mapema wanasiasa watatuletea matatizo na hatutafanya kazi kila siku tutakuwa mbio mbio, kazi hazitafanyika miradi haita kwenda, wajinga watakuwa wanawachangia wanasiasa, wanasiasa mambo yao ya dezodezo yatakuwa yanakwenda mtaji mdomo wako! -
 
Kwenye nchi za watu weusi inataka moyo wa chuma kutetea raia wake ambao kimsingi hata hawaelewi haki zao na faida ya mwanaharakati kama tundu lissu, freeman Aikaeli, John pambalu, twaha mwaipaya na wengine wengi.. Itafika wakati mapinduzi yafanywe na wachache tu tukitegemea watanzania waandamane kudai haki hapo hatutaweza

Kifuatacho ni Chama kuandaa mbinu kabambe za kukabiliana na ccm pasipo nguvu ya umma maana umma wenyewe hawana meno ndio maana serikali inajitafunia nchi inavyotaka.. Tundu lissu inabidi ajuwe kuwa hao anaowatetea ndohaohao wakishapewa ardhi ya ngorongoro watamshukuru Samia Kwa kuwaacha waendelee kuishi ndani ya hifadhi kuliko lissu aliepambana kuwatetea
Mkuu,

Watu weusi wame laanika

Malipo ya kuwapigania watu weusi ni kifo.

Yani ni afadhali kumpigania nyoka [emoji216] kuliko mtu mweusi mwafrika.
 
Tundu Lissu alisema maridhiano yaani zile 4Rs hakuna tena, hivyo sasa hivi CHADEMA hawayajui maongezi yoyote na CCM, so kila mtu atumie nguvu zake, kwa maana nyingine ukifute zile 4Rs hakuna pia mikutano ya hadhara..
 
Jana nilimshangaa sana Mh.Tundu Lissu kutaka kuforce mambo. Nilitarajia kama mwanasheria wa Mazingira angekaua mstari wa mbele kuelimisha jamii kuhusu utunzaji wa hifadhi yetu dhidi ya ongezeko la watu.
CHADEMA kuna mambo inabidi Tue makini sana,bila hivyo tutakuja kupata aibu kubwa
 
Sisi watu wa chini tunamuelewa lissu zaidi kuliko ccm. Hata mtulazimishe vipi ccm hapana.
Hao badala ya kufanya siasa wamegeuka kua wanaharakati wakudandia matukio na kuchonganisha serikali na raia, sisi upinzani hatujui siasa,....tumeshindwa kujenga grassroot ofisi za chama na kufungua matawi kwa kuuza philosophy za chama tunatafuta umaharufu kupitia matukio mbali mbali.
Kuna haja ya kupata chama cha siasa ambacho kinaweza kujenga sera mbadala ya chama tawala sio kupunga kila jambo bila kuonyesha mbadala wake, Lissu amakua mwanaharakati sio mwana siasa tena bora angefungua NGO ya kutetea hakati zake, kama ni mazingira au haki za binaadamu ili ajulikane iko wapi.
 
Jana nilimshangaa sana Mh.Tundu Lissu kutaka kuforce mambo. Nilitarajia kama mwanasheria wa Mazingira angekaua mstari wa mbele kuelimisha jamii kuhusu utunzaji wa hifadhi yetu dhidi ya ongezeko la watu.
CHADEMA kuna mambo inabidi Tue makini sana,bila hivyo tutakuja kupata aibu kubwa
Lissu alienda kwa ajili ya shughuli za kisiasa, hakwenda Ngorongoro kuwahesabu nyumbu au waarabu wa mama yenu, polisi walitakiwa kumuacha afanye kilichompeleka kwasababu hakuvunja sheria yoyote ya nchi, wao polisi ndio wahuni.
 
Sisi watu wa chini tunamuelewa lissu zaidi kuliko ccm. Hata mtulazimishe vipi ccm hapana.
Sio kweli,ni kua mmejazana mihemko tu basi. Ata ndani ya CHADEMA wengi atuelewi anachokifanya asa ili la Ngongoro.
 
Wakati mwingine tunashindwa kuona na kusema kweli kisa tumejivika gunia la upofu. Sehemu ila ata wakati wa Kampeini tunafanya za door to door campaign basi.
Lissu alienda kwa ajili ya shughuli za kisiasa, hakwenda Ngorongoro kuwahesabu nyumbu au waarabu wa mama yenu, polisi walitakiwa kunuacha afanye kilichompeleka kwasababu hakuvunja sheria yoyote ya nchi, wao polisi ndio wahuni.
 
Kuna tetesi kuwa Tundu Lissu amekamatwa na Polisi asubuhi hii akiwa hotelini huko Karatu.

Taarifa zaidi kukujia hapahapa jukwaani.

UPDATE:
Waliokamatwa Karatu hadi sasa ni

  1. Makamu Mwenyekiti CHADEMA Tundu Lissu
  2. Walinzi wote wa Tundu Lissu
  3. Katibu wa BAWACHA Catherine Ruge
  4. Mzee Hashim, Mwenyekiti Wa Baraza La Wazee CHADEMA Taifa
  5. Suzan Kiwanga na
  6. Mwandishi wa Jambo TV (Oscar).

Polisi wanaendelea kuwatafuta wengine walio ambatana na Tundu Lissu Wilayani Karatu

View attachment 2744826

====

Leo Septemba 10, 2023 Majira ya saa nne asubuhi Jeshi la Polisi wilaya ya Karatu lilifika Hotel ya Ngorongoro iliyopo Karatu na kuizingira, Polisi hao wakiwa na mitutu ya bunduki pamoja na mabomu. Jeshi hilo liliwaeleza wahudumu wa hotel hiyo kuwa wanataka kujua chumba alicholala Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara Mhe. Tundu Lissu wakaelezwa na kwenda kwenye chumba hicho.

Baada ya purukushani ya Jeshi la Polisi na walinzi wa Mhe. Lissu, Jeshi hilo lilingia kwa nguvu katika chumba alichofikia Mhe. Lissu na kuondoka nae bila kueleza wanaenda nae wapi.

Baadae wengine waliokamatwa na Jeshi hilo ni Mhe. Susan Kiwanga, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe. Catherine Ruge Katibu Bawacha Taifa, Mhe. Twaha Mwaipaya, walinzi wa Mhe. Lissu pamoja na watu wengine.

Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea Karatu.
View attachment 2744848
Samwel Welwel
Kawaite tec wasome waraka wakuipangia serekali tuna mabaraza mawili tu tec na binge ndiowanaisimamia serekali au unaongeza latatu nachadema?
 
Kuna tetesi kuwa Tundu Lissu amekamatwa na Polisi asubuhi hii akiwa hotelini huko Karatu.

Taarifa zaidi kukujia hapahapa jukwaani.

UPDATE:
Waliokamatwa Karatu hadi sasa ni

  1. Makamu Mwenyekiti CHADEMA Tundu Lissu
  2. Walinzi wote wa Tundu Lissu
  3. Katibu wa BAWACHA Catherine Ruge
  4. Mzee Hashim, Mwenyekiti Wa Baraza La Wazee CHADEMA Taifa
  5. Suzan Kiwanga na
  6. Mwandishi wa Jambo TV (Oscar).

Polisi wanaendelea kuwatafuta wengine walio ambatana na Tundu Lissu Wilayani Karatu

View attachment 2744826

====

Leo Septemba 10, 2023 Majira ya saa nne asubuhi Jeshi la Polisi wilaya ya Karatu lilifika Hotel ya Ngorongoro iliyopo Karatu na kuizingira, Polisi hao wakiwa na mitutu ya bunduki pamoja na mabomu. Jeshi hilo liliwaeleza wahudumu wa hotel hiyo kuwa wanataka kujua chumba alicholala Makamu Mwenyekiti wa Chama Bara Mhe. Tundu Lissu wakaelezwa na kwenda kwenye chumba hicho.

Baada ya purukushani ya Jeshi la Polisi na walinzi wa Mhe. Lissu, Jeshi hilo lilingia kwa nguvu katika chumba alichofikia Mhe. Lissu na kuondoka nae bila kueleza wanaenda nae wapi.

Baadae wengine waliokamatwa na Jeshi hilo ni Mhe. Susan Kiwanga, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mhe. Catherine Ruge Katibu Bawacha Taifa, Mhe. Twaha Mwaipaya, walinzi wa Mhe. Lissu pamoja na watu wengine.

Tunaendelea kufuatilia kinachoendelea Karatu.
View attachment 2744848
Samwel Welwel
Polisi wanapokea maagizo, wasipo fanya kama walivyo agizwa ni uhaini na watafukuzwa kazi lakini pia hata kifungo:
Kwa wapenda Demokrasia wasilaumu Polisi, walaumu mfumo[hapa mnanielewa].

Polisi wetu ni wasomi na wnaelewa sana wanachofanya, ila hawawezi kukaidi amri toka "sehemu za juu".

Nawashauri muendelee kuomba Mungu aamulie huu ugomvi kama alivyo amulia kipindi kile cha "vyuma"
 
Kamanda ata kuandika ujui kabisa!!
Hapa tunaongelea facts...Wamasai waliokuwepo miaka hiyo yote idadi yao na sasa ni tofauti sana. Hivi katika akili zenu sijui mnasomea nini? Ujui kua ongezeko la watu ni hatari kwa hifadhi? Hapo Ngongoro kuna Mmasai anaemiliki ardhi au nyumba ya kisasa?
Serikali ingewaondoa bila kua na alternative ilo lingeeleweka...kila familia inayo hamishwa inapewa nyuma na hati ya ardhi.....you can even figure this out?
Nakubaliana na wewe kwamba Masai waliokuwepo Zamani na sasa ni tofauti na wameongezeka pia ila nimeuliza swali kuwa hiyo athari ya kimazingira inaikumba tu Twamzania na sio nchi zingine while Kenya Wamasai wao wakizidi kuwepo sehemu hizo na wakiongezeka same amount as it is Sometimes tufanye reseach sio tusubiri kuambiwa tuseme nini na waliopo juu yetu...

NB: maneno niliyokosea kuyaandika Sijakosea nimefanya Sarcasm makusudi ili maana halisi ya neno niwe nalo lisitumike against me (Law's mogul)
 
Sio kweli,ni kua mmejazana mihemko tu basi. Ata ndani ya CHADEMA wengi atuelewi anachokifanya asa ili la Ngongoro.
Wewe ni mpumbavu! Kama hujui historia ya ngorongoro toka enzi za mwinyi baba basi huna moral authority ya kusema lolote. Tambua kwamba kila rais akija mzanzibari anataka kuwapa waarabu ngorongoro kwanini?
 
Sio kweli,ni kua mmejazana mihemko tu basi. Ata ndani ya CHADEMA wengi atuelewi anachokifanya asa ili la Ngongoro.
Uko CHADEMA kimakosa,ingia CHAMATA(CHAMA CHA MACHAWA).
 
Back
Top Bottom