Uchaguzi 2020 Tundu Lissu akiwa Tunduma leo

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu akiwa Tunduma leo

Kumbukeni baada ya Jecha kufuta matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar.Kumbe ccm walikuwa tayari wamesha print tshirt za kumpongeza Dr Sheni.Hamnaga uchaguzi...mpaka tume iwe HURU.Hiyo ndio risasi ya mwisho ya chichiem.
 
Hawa jamaa wa Tunduma ndio wamefunika kote alikopita Lissu, yaani hawa ndio hawataki kusikia ujinga ujinga wa kijani kabisa.
Kwani nao wamefikia hadhi ya kupiga deki lami ili TL apite?
 
Kuna Mkuu mmoja hapa JF anaitwa Jerico Nyerere , alizungumza kuwa watanzania ni wajinga na hii kufuatana na asilimia alizozitoa kuelezea wajinga.

Yeye ni mjinga pia kwa kuwa AME ANDIKA KITABU CHA UJASUSI NA TAIFA. haya yote unayo yaona yanatokea Mbeya, Iringa na yatakayo kokote kule ndani ya nchi ya Tanzania, wahusika wanafahamu au kabla ama muda mfupi baada ya kutokea. Kama maandamano na mikutano ya TUNDU LISSU Taifa linafahamu kinachotaka kitakachotokea. Kwa majasusi Lissu anafuata script.

Sisi JF ndio tunajua maandamano hayo tukiona kwenye Utube.

Kinachotokea katika mizunguuko ya Lissu ni afya kwa Taifa letu kwa kuwa kinaamsha walioko madarakani waongeze juhudi zao katika kuleta mabadiliko ya kijamii ndani ya nchi yetu.

Na kusema Watanzania ni wajinga namshauri Yerico Nyerere aone wananchi wa Mbeya na Iringa wamekiamsha na wamemjibu.
 
Akofu bagonza alikuwa anasema , nanukuu .

DINI si mali za viongozi, Vyama si mali ya viongozi na Serikali si mali ya viongozi. Lakini vyote (DINI, vyama na serikali) havimmiliki Mungu. Hata hivyo Kongamano limemtanguliza Mungu. Inapendeza, lakini wakumbuke:

-Mungu halindwi, analinda
-Mungu habebwi, anabeba
-Mungu haamrishwi, anaamrisha
-Mungu hamilikiwi, anamiliki
-Mungu si tukio ni mchakato.

mwisho wa kunukuu . Tafakuri hii inanifikirisha sana kwa sasa na kusanyiko la wana dini wale waliounga juhudi .
 
Mwaka huu tunahesabu kura wenyewe matokeo yanatangazwa vituoni.hii mambo ya tume inajumlisha kura hatuna imani nayo
 
Back
Top Bottom