Tundu Lissu: Aliyenipa ushahidi wa pesa za Abdul na mama yake kwa sasa ni marehemu

Tundu Lissu: Aliyenipa ushahidi wa pesa za Abdul na mama yake kwa sasa ni marehemu

Endelea kupiga supu tajiri nyama ziko chini. Ndo kwanza kumekucha, ikivuma sana lazima ipasuke huu ni muda wa CHADEMA kupasuka na haizuiliki. Ukishakuwa na taasisi lakini uendeshaji wake unasimamiwa na mtu mmoja au kikundi kidogo cha watu haiwezi ku last long.

Muda utasema vizuri hata huo ushahidi kama haya yameanza kutokea naamini with time nao utaonekana. Taratiibu bila haraka

Merry X-Mass
Mkuu, wakumbushe pia kwamba ilianza kitambo sana sana mno kwa uvumi na tetesi za hapa na pale, watu wakidai mbona kama mwenyekiti na makamu wake haziivi, hawashibani, wanapishana?

Lakini wenye mahaba yao niue waliendelea kushupaza shingo, huku wakibisha na kutukana - eti mtasuburi sana!

Ni kweli kila kukicha kuna ukurasa fulani unawekwa wazi! Hadi hatua hii karibu kila kauli ya jukwaani au mitandaoni iliyokuwa na utata, sasa inaanza kueleweka vizuri.

Hakika, tuna safari ndefu sana kama taifa!!!
 
Mimi nilishtuka nilipo sikia habari za mtu aliyempa Lissu hizo info ni marehemu na kwamba alikuwa mjumbe wa kamati kuu

Nikajiuliza huyo mtu ni nani na alikufa kifo cha aina gani?

Mambo ya Abdul na Wenje na rushwa zao ni swala la hivi karibuni tu, Aliyefariki karibuni ambaye ni mjumbe bila shaka ni Mzee Ali Kibao

Kwa mazingira haya sio chadema wala serikali watatoka kwenye kashfa ya kifo cha Kibao, hii inaelekea ni joint operation kati ya serikali na baadhi ya watu chadema

Halafu ndio maana pia mama yenu aling'aka aliposkia kifo cha Kibao na kuishia kusema kwa hasira kifo ni kifo tu wamekufa wangapi mnahangaika na Kibao?

Huenda siri alizokuwa nazo Kibao zina implicate familia yake ndio maana akawa kama katiwa pilipili

Muda ni mwalimu mzuri, Tusubirie
Ni kweli hata mimi najiuliza vipi mpango wa kumuua Lissu ili Mbowe asingiziwe ???.
 
Hahahaa.

Sicheki Lissu kupigwa risasi.

Nacheka tu jinsi narrative inavyoanza kubadilika kidogo kidogo.

Mwanzoni villain alikuwa Magufuli.

Sasa hivi kibao kimeanza kubadilika kidogo kidogo.

Muda si mrefu kuna mtu atatapika yote aliyonayo moyoni.

Ila kwa huu ufa ulioanza kujionyesha, CHADEMA haitokuwa tena kama ilivyokuwa zamani.

Hii CHADEMA ya sasa na ijayo, ni dhaifu sana.

Na kuhusu Mbowe, kuna watu humu walikuwa wanahoji sana ushiriki wake katika kupotea kwa Ben Saanane na kushambuliwa kwa Lissu.

Hiyo ilikuwa ni kipindi kile cha Magufuli.

Lakini kwa vile Magufuli ndo alikuwa villain kwa wakati huo, jaribio lolote lile la hata kuhoji tu uwezekano wa labda Mbowe alikuwa anajua zaidi kuhusu hayo matukio kuliko na alivyokuwa anaonekana, lilikumbwa na push back kali sana toka kwa makamanda.

Like, how dare you question our dear chairman! Mbowe ndiye aliyekodi ndege binafsi kum airlift Lissu kwenda Nairobi akiwa hajitambui.

Anywho, ngoja niendelee kuangalia hii ngoma iliyo inogile.

Ila idea ya kwamba sasa Mbowe ameanza kuwa villain, ni tamu kuliko cranberry sauce iliyopo kwenye menu ya kesho kwenye mlo wa Krismasi 🤣.

It will be sweet to watch what transpires.
Yan mzee ni bingwa kweli usikute hata ile helicopta ilikuwa ni kujivua kabsa incase lissu angekata moto watu ni ma mastermind by the way mtu ambaye ni threat ndani ya CDM automatically anakuwa threat kwa watawala since he never takes order from the top of the chama to neutralise any situation in the country
 
Kalamu,

Huoni kwamba anatumia weledi wake kisheria kutuhadaa?

Ikiwa shahidi muhimu ni marehemu, awezaje itwa court kushuhudia iwapo Lissu amepandiahwa kizimbani?
Mkuu, labda kama hufuatilii hili timbwili lilivyoanza tangu mwanzo kabisa.

Kwanza, alitamka kwamba kuna mtu mkubwa ndani ya chama alitaka ashirikiane na kada wa chama tawala ili ampe TAL rushwa. Hakuwa ametaja jina, na watu wakadhani uzushi.

Siku zilipoenda, kila mmoja anashangaa huyo Mzee Wenje anaibuka akidai ni kweli kuna sekeseke kama hilo! Umeona?!

Hebu fikiria, kama TAL alishtukia ile rushwa mapema kabisa kiasi cha kukataa kwenda nao hotelini, hivi unadhani hakujiandaa kwa ajili ya yatokayo kwa siku za mbeleni - yaani kukusanya taarifa na ushahidi just in case?

Namaanisha, kwa nini huamini kwamba TAL anao ushahidi wa kutosha kabisa juu ya yote hayo - huku akijua fika kwamba tukio kama hilo liwahusulo papa wakubwa ndani na nje ya chama lazima tu ingetumika nguvu kubwa mno ya kulizima, kama tuonavyo sasa?

Kwa mfano, tuseme labda alirekodi matukio yote ya maongezi hayo kisiri (just saying!) au yale mazungumzo yake (dokezo kuhusu rushwa) na marehemu Ali Kibao?!

Wala haihitaji akili nyingi kujua kwamba jamaa amebeba siri nzito sana ambazo akimwaga zote hadharani kwa pamoja, sidhani kama kutakalika nchini!

Mie nilipoona juzi ameanza kuvaa bullet proof, nikajiwazia mambo mengi mno!!!
 
Mkuu, wakumbushe pia kwamba ilianza kitambo sana sana mno kwa uvumi na tetesi za hapa na pale, watu wakidai mbona kama mwenyekiti na makamu wake haziivi, hawashibani, wanapishana?

Lakini wenye mahaba yao niue waliendelea kushupaza shingo, huku wakibisha na kutukana - eti mtasuburi sana!

Ni kweli kila kukicha kuna ukurasa fulani unawekwa wazi! Hadi hatua hii karibu kila kauli ya jukwaani au mitandaoni iliyokuwa na utata, sasa inaanza kueleweka vizuri.

Hakika, tuna safari ndefu sana kama taifa!!!
Halafu wakaja kubisha wakidai zinaiva

2015 Ilikua baba ndubwi na mzee wa mihogo, 2025 baba ndubwi na domokaya

Haya
 
Mgombea Uenyekiti wa Chadema Tundu Lissu amefunguka kupitia Twitter space jinsi alivyokusanya ushahidi wa kutosha kuhusu rushwa ya pesa za Abdul na mama yake kwa viongozi wa Chadema.

Ameeleza kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati kuu ya Chama cha CHADEMA aliyempatia ushahidi wa kina kuhusiana na tuhuma hizo na aliyemsaidia kuthibitisha tuhuma hizo mbele ya kamati kuu ya Chama cha CHADEMA kwa sasa ni Marehemu. Hata hivyo Lissu alikataa kumtaja Mjumbe huyo akidai kwamba haitasaidia kitu chochote.

Na alipoulizwa iwapo kifo cha Mzee Ali Kibao kinahusiana na tuhuma za pesa za Abdul aliomba asilizungumzie Hilo kwa sasa.
Wea iz Britanicca?
Mzee wa zandaaani
 
Mkuu, Kibao alikuwa ni mtu wa karibu sana wa Mbowe. Na alikuwa anajua mengi.

Tutafakari:
1. Mwenyekiti anafuatwa gerezani na ''watu wasiojulikana'' na kufanya mazungumzo ya kina.

2. Anatolewa gerezani na kwenda kwa mama moja kwa moja na wafanya mazungumzo ya faragha wao wawili tu.

3. Abdul na makapu yake yaliyojaa fedha anamtembelea mwenyekiti na baadhi ya viongozi wa chama na anaondoka makapu yakiwa tupu.

3. Mwenyekiti anaambiwa amuunganishe Abdul na Lissu ili naye apate mgao wake na anamteua Wenjele kufanya hiyo kazi.

4. Wenjele na Abdul wanakwenda na makapu yao yaliyojaa fedha kwa Lissu lakini Lissu anayakataa.

5. Lissu anafanya uchunguzi mkali na wa siri na mzee Kibao anampa details zote.

6. Lissu anaanika hadharani kuhusu makapu ya fedha.

7. Mwenyekiti anaitisha kikao ili amwadhibu Lissu

8. Lissu anatoa ushahidi wa kina na mwenyekiti anaufyata.

9. Mwenyekiti anagundua kumbe Kibao alitoa siri.

10. Mwenyekiti anamrudia Abdul na kumweleza alichofanya Kibao, na Abdul anamwambia mama, na mama anamwambia mkuu wa ''wasiojulikana'' na ''wasiojulikana'' wanatumwa kufanya waliyofanya.

11. Wakati wa mazishi ya Kibao, familia inakuja juu lakini mwenyekiti anaingilia kati kinafiki na kusema wawe na adabu.
Duuuuuu hatari kubwa Aiseee
 
Back
Top Bottom