Mkuu, Kibao alikuwa ni mtu wa karibu sana wa Mbowe. Na alikuwa anajua mengi. Tutafakari: 1. Mwenyekiti anafuatwa gerezani na ''watu wasiojulikana'' na kufanya mazungumzo ya kina. 2. Anatolewa gerezani na kwenda kwa mama moja kwa moja na wafanya mazungumzo ya faragha wao wawili tu. 3. Abdul na makapu yake yaliyojaa fedha anamtembelea mwenyekiti na baadhi ya viongozi wa chama na anaondoka makapu yakiwa tupu. 3. Mwenyekiti anaambiwa amuunganishe Abdul na Lissu ili naye apate mgao wake na anamteua Wenjele kufanya hiyo kazi. 4. Wenjele na Abdul wanakwenda na makapu yao yaliyojaa fedha kwa Lissu lakini Lissu anayakataa. 5. Lissu anafanya uchunguzi mkali na wa siri na mzee Kibao anampa details zote. 6. Lissu anaanika hadharani kuhusu makapu ya fedha. 7. Mwenyekiti anaitisha kikao ili amwadhibu Lissu 8. Lissu anatoa ushahidi wa kina na mwenyekiti anaufyata. 9.Mwenyekiti anagundua kumbe Kibao alitoa siri. 10. Mwenyekiti anamrudia Abdul na kumweleza alichofanya Kibao, na Abdul anamwambia mama, na mama anamwambia mkuu wa ''wasiojulikana'' na ''wasiojulikana'' wanatumwa kufanya waliyofanya. 11. Wakati wa mazishi ya Kibao, familia inakuja juu lakini mwenyekiti anaingilia kati kinafiki na kusema wawe na adabu.