Tundu Lissu: Aliyenipa ushahidi wa pesa za Abdul na mama yake kwa sasa ni marehemu

Mkuu, wakumbushe pia kwamba ilianza kitambo sana sana mno kwa uvumi na tetesi za hapa na pale, watu wakidai mbona kama mwenyekiti na makamu wake haziivi, hawashibani, wanapishana?

Lakini wenye mahaba yao niue waliendelea kushupaza shingo, huku wakibisha na kutukana - eti mtasuburi sana!

Ni kweli kila kukicha kuna ukurasa fulani unawekwa wazi! Hadi hatua hii karibu kila kauli ya jukwaani au mitandaoni iliyokuwa na utata, sasa inaanza kueleweka vizuri.

Hakika, tuna safari ndefu sana kama taifa!!!
 
Ni kweli hata mimi najiuliza vipi mpango wa kumuua Lissu ili Mbowe asingiziwe ???.
 
Yan mzee ni bingwa kweli usikute hata ile helicopta ilikuwa ni kujivua kabsa incase lissu angekata moto watu ni ma mastermind by the way mtu ambaye ni threat ndani ya CDM automatically anakuwa threat kwa watawala since he never takes order from the top of the chama to neutralise any situation in the country
 
Kalamu,

Huoni kwamba anatumia weledi wake kisheria kutuhadaa?

Ikiwa shahidi muhimu ni marehemu, awezaje itwa court kushuhudia iwapo Lissu amepandiahwa kizimbani?
Mkuu, labda kama hufuatilii hili timbwili lilivyoanza tangu mwanzo kabisa.

Kwanza, alitamka kwamba kuna mtu mkubwa ndani ya chama alitaka ashirikiane na kada wa chama tawala ili ampe TAL rushwa. Hakuwa ametaja jina, na watu wakadhani uzushi.

Siku zilipoenda, kila mmoja anashangaa huyo Mzee Wenje anaibuka akidai ni kweli kuna sekeseke kama hilo! Umeona?!

Hebu fikiria, kama TAL alishtukia ile rushwa mapema kabisa kiasi cha kukataa kwenda nao hotelini, hivi unadhani hakujiandaa kwa ajili ya yatokayo kwa siku za mbeleni - yaani kukusanya taarifa na ushahidi just in case?

Namaanisha, kwa nini huamini kwamba TAL anao ushahidi wa kutosha kabisa juu ya yote hayo - huku akijua fika kwamba tukio kama hilo liwahusulo papa wakubwa ndani na nje ya chama lazima tu ingetumika nguvu kubwa mno ya kulizima, kama tuonavyo sasa?

Kwa mfano, tuseme labda alirekodi matukio yote ya maongezi hayo kisiri (just saying!) au yale mazungumzo yake (dokezo kuhusu rushwa) na marehemu Ali Kibao?!

Wala haihitaji akili nyingi kujua kwamba jamaa amebeba siri nzito sana ambazo akimwaga zote hadharani kwa pamoja, sidhani kama kutakalika nchini!

Mie nilipoona juzi ameanza kuvaa bullet proof, nikajiwazia mambo mengi mno!!!
 
Halafu wakaja kubisha wakidai zinaiva

2015 Ilikua baba ndubwi na mzee wa mihogo, 2025 baba ndubwi na domokaya

Haya
 
Wea iz Britanicca?
Mzee wa zandaaani
 
Duuuuuu hatari kubwa Aiseee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…