Kijana acha kuwa Moumbavu, Mikutano ni haki ya kikatiba, hizo kesi pia ni haki kikatiba, sio zawadi.wapi kasema Samia anaupiga mwingi? Unajua kama siyo "maridhiano" hata mikutano ya vyama ingelikuwa bado imefungiwa? Kesi 400 plus zingelikuwa bado mahakamani, etc etc. Sema kuwa huo ni mwanzo.... bado mengi ya kufaya kuleta utawala bora, katiba mpya tume huru y uchaguzi etc etc.
NIKUULIZE: Lisu atamlazimishaje samia alete katiba mpya? Tume huru ya uchaguzi? naomba jibu. kwanini hajafanya leo na jana, mpaka awe mwenyekiti?
Daaah unaumiza sanaMkuu, Kibao alikuwa ni mtu wa karibu sana wa Mbowe. Na alikuwa anajua mengi. Tutafakari: 1. Mwenyekiti anafuatwa gerezani na ''watu wasiojulikana'' na kufanya mazungumzo ya kina. 2. Anatolewa gerezani na kwenda kwa mama moja kwa moja na wafanya mazungumzo ya faragha wao wawili tu. 3. Abdul na makapu yake yaliyojaa fedha anamtembelea mwenyekiti na baadhi ya viongozi wa chama na anaondoka makapu yakiwa tupu. 3. Mwenyekiti anaambiwa amuunganishe Abdul na Lissu ili naye apate mgao wake na anamteua Wenjele kufanya hiyo kazi. 4. Wenjele na Abdul wanakwenda na makapu yao yaliyojaa fedha kwa Lissu lakini Lissu anayakataa. 5. Lissu anafanya uchunguzi mkali na wa siri na mzee Kibao anampa details zote. 6. Lissu anaanika hadharani kuhusu makapu ya fedha. 7. Mwenyekiti anaitisha kikao ili amwadhibu Lissu 8. Lissu anatoa ushahidi wa kina na mwenyekiti anaufyata. 9.Mwenyekiti anagundua kumbe Kibao alitoa siri. 10. Mwenyekiti anamrudia Abdul na kumweleza alichofanya Kibao, na Abdul anamwambia mama, na mama anamwambia mkuu wa ''wasiojulikana'' na ''wasiojulikana'' wanatumwa kufanya waliyofanya. 11. Wakati wa mazishi ya Kibao, familia inakuja juu lakini mwenyekiti anaingilia kati kinafiki na kusema wawe na adabu.
Bora mbowe anyamaze akianza kujibu tuhuma ni aibu, maana walikaa meza moja na kupanga matukio, leo lawama kwa Mbowe [emoji2][emoji2]Lissu alimiminiwa risasi,Lissu huyo huyo alisaidiwa kwa kirefu kukodi ndege,kumsafirisha hadi Nairobi Kenya kwa matibabu na Mheshimiwa Mwenyekiti Mbowe.
Gharama za matibabu na mwenendo wa tiba hadi akatinga Belgium ni Mbowe.
Ikiwa Lissu anasema Mbowe ni prime suspect basi Chadema imekufa na kuzikwa juzi.
Lissu atakuwa yuko kwenye hatari sana. Naelewa sasa kwanini aliomba ahakikishiwe usalama wake na aliomba ulinzi kwa serikali, sasa sishangai akivaa bullet proof vest.
Sababu ya kumuondoa Kibao inaweza kutumika hiyo hiyo kujaribu kumuondoa Lissu duniani.
na watu wakapongeza FAM ana busara sana kumbe anajua anateta familiaNa watu hao hawakuwa wepesi maana hadi walijua nyendo zake wakaenda kumkamata katika basi ambako Mzee wa watu alidhani ni usafiri salama.
Kumbe ndio maana Mbowe alizuia wanachama waliokuwa na hasira msibani wasimfanyie fujo Masauni!
Hahaha msala anatupiwa marehemu😂Mgombea Uenyekiti wa Chadema Tundu Lissu amefunguka kupitia Twitter space jinsi alivyokusanya ushahidi wa kutosha kuhusu rushwa ya pesa za Abdul na mama yake kwa viongozi wa Chadema.
Ameeleza kuwa mmoja wa wajumbe wa kamati kuu ya Chama cha CHADEMA aliyempatia ushahidi wa kina kuhusiana na tuhuma hizo na aliyemsaidia kuthibitisha tuhuma hizo mbele ya kamati kuu ya Chama cha CHADEMA kwa sasa ni Marehemu. Hata hivyo Lissu alikataa kumtaja Mjumbe huyo akidai kwamba haitasaidia kitu chochote.
Na alipoulizwa iwapo kifo cha Mzee Ali Kibao kinahusiana na tuhuma za pesa za Abdul aliomba asilizungumzie Hilo kwa sasa.
Magufuli ndiye aliyeamuru Lissu kupigwa risasi. Na ndiye aliyeamuru Ben Saanane auawe. Wacha ufala.💯%.
Leo hii wameanza kuchenjiana wao kwa wao huku wengine wakidondosha vidokezo kuwa Mbowe anahusika moja kwa moja na baadhi ya matukio.
Ipo siku watamuomba radhi Magufuli na Pengine hata kumpigia kampeni kwa Papa ili apate utakatifu.
Kuna vitu vingine ukielezwa vina make sense. Hili ni mojawapo.Kalamu,
Huoni kwamba anatumia weledi wake kisheria kutuhadaa?
Ikiwa shahidi muhimu ni marehemu, awezaje itwa court kushuhudia iwapo Lissu amepandiahwa kizimbani?
kunja ngumi ,kunja ngumi kamandaMakamanda pipoooz😁😂
Mfumo ni nini ewe nanga? Ukiambia hata uelezee mfumo ni nini huwezi kuelezea?Yaani nyie mnamdanganya sana Lissu duniani hapa huwezi kupingana na mfumo, na mfumo haujawahi shindwa ni swala la mda tu. Pia na waambia mabadiliko tunayo yataka hayawezi kuletwa na wanasiasi kamwe.
Ni hatari sana.Kumbe ndio maana maCCM wanachukulia powa sana wananchi kwasababu wanajuwa hatuna kimbilio.
Kuna watu tumekosana na marafiki na Ndugu kwa kumtetetea Mbowe, watu wamepoteza maisha, mali muda na kila kitu kwa kuijenga CHADEMA wakati Mwenyekiti wake akiwa anafanya deal la kula kuuza nchi kwa kushirikiana na CCM.
ChawaHuo ni wajibu wa vyombo vya dola, peleka ushahidi ili huyo mtu wa cdm aaumbuke. Badala ya kuwabambikizia kesi, ushahidi wako ungekuwa mzuri.
Umewaza kama mimi simuamini kabisa huyu mwambaHuyu mbowe ni zaidi ya mwenyekiti huyu anaweza kuwa ni muhusika wa matukio mabaya ya wanachadema.
Hiyo ilikuwa ni kazi ya shetani mkuu Magu.Na inawezekana ndiye aliyepanga kumfyatulia risasi Lissu😁😁
Umeongea sahihi. Mimi nimebakia mwanasiasa wa hapa JF tu sio nje ya hapo. Kuna mambo ukiyajua utatamani usingeyajua. CHADEMA na CCM sio sehemu za mzaha.Aiseee!
Ipo shida kubwa CHADEMA, naomba isiwe hivi ninavyofikiri.
Lakini, siasa za Tanzania ni hatari mno. Kama mtu anajijua hayuko tayari kuagana na nyonga ni vyema asijihusishe kabisa.
Hapo ndio tunapishanaHujazoea maisha ya kufichua uovu. Yale mazoea ya kufunika ujambazi wa kisiasa kwa kivuli cha SIRI ZA NDANI ni upofu mkubwa na kudhulumu haki za wengi