Tundu Lissu: Aliyeongoza Kikosi cha wauaji walioagizwa kuniua ni Paul Makonda, ndio maana Marekani ilimzuia

Tundu Lissu: Aliyeongoza Kikosi cha wauaji walioagizwa kuniua ni Paul Makonda, ndio maana Marekani ilimzuia

Mwambie kizimkazi kuwa wazungu wameanza kutekenya SERIKALI yake kwasababu yake Maneno yake ya taarabu yameanza kuzaa matuda Kwa kuanza na kesi hii...
Ushahidi wa matukio haya yote yapo Huko UK wanasubiri kesi ianze Kwa kampuni ya tigo kufunguliwa mashitaka, ule msemo WA wasiojulikana unaenda kujulikana kwa kuvuliwa nguo.

Picha za satellite zimepatikana na ushahidi upo wazi wanasubiriwa Tu tigo kuingia mahakamani hapa tutajua Siri zote
 
Kwa hiyo tunaongelea Tindu Lissu tu. Hakuna kitu kingine? Hizo ndo sera za CDM?
Kama Tanzania imeingia mikataba ya Kimataifa na kuiridhia ikiwemo mikataba ihusuyo haki za binadamu kama lilivyotamkwa mwaka 1948. Hali kadhalika kama bill of rights tumekubali kuiweka katika katiba yetu na kwakua moja wapo ya haki za binadamu ni haki ya kuishi, na kwakua katika ahadi za mwanaccm moja wapo ni binadamu wote ni sawa. Ipo haja ya wewe kufundishwa kwamba hakuna kitu chochote kinachoweza kulinganishwa na uhai wa mtu. Hakuna mtu mwenye haki ya kuutwa uhai wa mtu kwa namna yoyote ile. Tusiposema na kukemea bayana kwamba kuua watu wasiokua na hatia ni kosa itakua jamhuri ya aina gani ambapo watu wanauana kama wanyama ati kisa tu tumetofautiana itikadi mtazamo au mawazo.
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara Tundu Lissu amezungumza hayo mbele ya wanahabari leo, Jumatano Septemba 25.2024, jijini Dar es Salaam

Kiongozi wa kikosi cha mauaji dhidi yangu mwaka 2017 alikuwa Paul Makonda. Aliwaongoza wauwaji walionipigia risasi 36 Dodoma.” - Tundu Lissu

"Shambulio dhidi yangu (shambulio la Tundu Lissu kupigwa risasi) limetokea katikati ya majengo ya serikali wanayokaa Mawaziri, Naibu Spika Tulika akson kwa wakati ule (sasa ni Spika wa Bunge), Waziri Harrison Mwakyembe (aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo), Waziri wa Nishati wa wakati ule yeye alikuwa anakaaa juu na mimi nilikuwa nakaa chini" -Lissu

"Katika majenho ambayo yana ulinzi na yanakaa wakubwa (viongozi wa juu/waandamizi) eneo hilo lilikuwa sio tu lina ulinzi masaa 24 bali lilikuwa vilevile na kamera za CCTV, na kama mtakumbuka baada ya shamhulio hilo aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma alikuwa anaitwa 'Mroto' alitangaza kuwa Polisi walikua wamepata ile picha za hiyo CCTV kamera iliyokuwa inatazama ile parking lot ambayo nilikuwa nimeshambuliwa" -Lissu
Kwa tuhuma hz nzito kwa bashite bado amekalia ofisi ya uma? Tanpol fanya kz yenu
 
Huwezi kusikia Tlaatlaah na yule chawa mwingine wakisema neno kwenye hili
huyu wakili Lisu si sawa tu na yule wakili anaitwa sijui matrekta, ambae anabwekagabwekaga kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari akifikka mahakamani anatia huruma tu, hamna kitu, ndiyo sasa ya huyi kidomodomo anae ropokaropoka tu hapo, kwenye mambo ya msingi anaendekeza hisia ili aonewe huruma na jamii...

nipo hapa, hakuna amabacho atasaidika nacho huyo muungwana..

hata hivyo,
naendelea kumskiza ili nipate fursa na haki zaidi, ili niweze kumshauri kitaalamu zaidi :pedroP:
 
Huu ujinga ni wa kiwango cha lami, kumtuhumu mtu bila ushahidi ni pumba iliyoje
Lissu anajua anachofanya, Wewe ndio hujui.

Anayetuhumiwa hapo ni mkuu wa mkoa, mteule wa Rais, ana tools zote za kumfungulia Lissu kesi ya defamation. Akafanye hivyo 😀

Kama haujapendezwa pia msaidie Makonda kufungua kesi.

Hii issue tunayo sana, as long as uchunguzi dhidi ya kupigwa kwake risasi uko pending. Halafu sio issue ya Lissu pekeyake ni issue ya familia hadi wajukuu .

There’s more than one way to skin a cat!
 
huyu wakili Lisu si sawa tu na yule wakili anaitwa sijui matrekta, ambae anabwekagabwekaga kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari akifikka mahakamani anatia huruma tu, hamna kitu, ndiyo sasa ya huyi kidomodomo anae ropokaropoka tu hapo, kwenye mambo ya msingi anaendekeza hisia ili aonewe huruma na jamii...

nipo hapa, hakuna amabacho atasaidika nacho huyo muungwana..

hata hivyo,
naendelea kumskiza ili nipate fursa na haki zaidi, ili niweze kumshauri kitaalamu zaidi :pedroP:
Anabweka bweka kama.bosi wako anavyobweka bweka
 
Mh. Lissu alitibiwa na wafadhili wake - je ni kweli kwa muktadha huo atakuwa na risiti za matibabu?
 
Ndio maana ninasema 4R za mama yenu ni utapeli mtupu.

Jambazi kama hili likarudishwa na kupewa ofisi ya umma halafu useme huo ni mrengo tofauti kiuongozi?
images (14).jpeg
 
Anaweweseka nini wakati anaeleza ukweli na uhalisia. Ninyi wauaji mnapata shida sana majina yenu yanapowekwa wazi. Lazima siku moja msimame kizimbani. Hiyo siku ipo tu, hata mfanye nini. Mlaaniwe wauaji.
Nasikitika mnamdhihaki lissu!
 
Back
Top Bottom