PreGE2025 Tundu Lissu amegoma kesi yake kuendeshwa kwa njia ya Mtandao. Kesi yaendelea Mahakamani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Una uelewa mdogo mno
Rudia kusoma hata kichwa cha habari tu nacho umeshindwa kuelewa?

Anayekataa kesi isiendeshwe wazi ni Lisu sio serikali wala polisi wala CCM
Kwamba akienda mahakamani haiwezi kurusha online? Ama hiyo online lazima awe gerezani ndio inafanya kazi? Hilo link lenyewe ni lizito kisha mnataka kujifanya mnaendesha kidigital?!
 
Ombi la kwanza ni hilo anaomba ahirisho dogo wajiandae chakujibu. Naona wanataka kupewa maelekezo kutoka juu. Ameulizwa mnajiandaa nini wakati kila kitu kipo wazi mtujibu. Akasema anahitaji kuongea na mamlaka zingine ili ajue atasema nini.
Kesi imewashinda kabla hawajaianza😀😀
 
Kwann isifanyike live kisha iwe live recorded ili dunia nzima ione?
 

1. Haki ya Kusomewa Mashtaka Mahakamani kwa Hadhira ya Umma​


Katiba ya Tanzania, Ibara ya 13(6)(a):
Inasema kwamba kila mtu ana haki ya kusikilizwa na mahakama au chombo kingine cha haki, kilicho huru na kisichoegemea upande wowote, na katika mazingira ya wazi, isipokuwa kama kuna sababu za msingi za kufanya hivyo faraghani.


➡️ Maana yake: Mshtakiwa ana haki ya kusomewa mashtaka mbele ya mahakama hadharani, na hii mara nyingi hufanyika ana kwa ana kwa mara ya kwanza, ili kuhakikisha:


  • Uhalali wa kumshikilia unathibitishwa.
  • Anajulishwa rasmi mashtaka yanayomkabili.
  • Ana nafasi ya kuomba dhamana au kujibu mashtaka.

2. Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA), Sura ya 20​


Sheria hii inaweka utaratibu wa hatua mbalimbali za mashauri ya jinai.
Kifungu cha 187(1) kinataja kuwa:
➡️ Maana yake: Mshtakiwa anatakiwa awepo mahakamani kwa kusomewa mashtaka yake, si kwa njia ya mtandao kabla ya hatua hizo kukamilika.

3. Utaratibu wa Mtandao na Haki za Mshtakiwa​


Kwa kutumia teknolojia ya video au mtandao, kuna miongozo inayotakiwa ifuatwe, ikiwa ni pamoja na:


  • Mshtakiwa kukubali kuendelea kwa njia hiyo.
  • Kuhakikisha kwamba haki zake hazivunjwi (kama kushauriwa na wakili, kusikia kila kilichosemwa, n.k).
  • Kuwepo kwa mazingira salama ya mawasiliano.

Ikiwa mshtakiwa hajakubali kwa hiari, au hajawahi kufikishwa mahakamani ana kwa ana, basi kutumia mtandao bila kukamilisha hatua hizo za awali kunaweza kuonekana ni ukiukaji wa haki zake za msingi.

Hitimisho:​


Kwa kuzingatia Katiba na sheria za Tanzania, kuna msingi wa kisheria unaoweza kuhalalisha msimamo wa Lissu kugoma kuendelea kwa njia ya mtandao ikiwa hakuwahi kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza kusomewa mashtaka. Hili linaenda sambamba na haki ya kuwa na mchakato wa haki, uwazi, na usawa mbele ya sheria.
 
Well
 
Endeleen kwanza nisafirishe Familia yangu kwenda ulaya nikirudi nikichafue mitandaoni
 
Dah hakika haki na sheria kwenye hii inchi zipo tu kwenye maandishi lakini hakuna haki/sheria inayotekelezwa....kwa hili serikali ya mama kizimkazi imejivua nguo.
 
Wewe ni mwanasheria bila shaka na umeelewa sheria iliyotumika ndio maana umekuja na andiko hili.
Heko kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…