Tundu Lissu ameongea na Radio Citizen Kenya asubuhi ya leo, ameleezea hali ya usalama nchini pamoja na suala la Corona

Tundu Lissu ameongea na Radio Citizen Kenya asubuhi ya leo, ameleezea hali ya usalama nchini pamoja na suala la Corona

Huyu anataka kuongoza hii nchi.. huku akikimbilia kutuonyesha hataki kutumia.. vyombo vya habari vya nchini.. huyu angeuza nchi yetu kama angebahatika kuchaguliwa kuwa Rais..

Anaonyesha yupo radhi.. media za nchi za nje ziendelee.. kuliko za nchini.. mpenda mabeberu.. hajali uchumi wa nchi yetu.. wala kusaidia kutengeneza ajira.. kwa sababu kawaona bora Kenyans waendelee.. poleni washabiki wake wafwu..

Magufuli 💯 Mzalendo
Akili za kitopian, mzuie vyombo vya ndani visioneshe matukio na hotuba zake afu atafute njia ya kuhutumia na kuwasiliana na wapiga kura mlete uzezeta huu!! Tilieni dawa ndio Kwanza inaingia.
 
Yaani mie huyu simuelewi kabisa, hivi wapiga kula wake wako kenya?, Watanzania wangapi wana access na hizo radio za kenya!
sasa kama media za wabongo zinaogopa kumpa coverage unataka na wa nje nae wafuate ivoivo.
Uzuri hizo media zao na bongo zinasikika
 
Hivi Lisu anataka urais wa tz au Kenya?

Maana ukiangalia hata katika hotuba zake zote hakuna inayoisha bila kutaja Kenya
Lazima awataje? anaishi leo kwa kuwa ana chupa nyingi ya damu za wakenya
 
Sisis watz ndio tumemshauri aongee huko nyia wasaka vyeo mtuache na Rais wetu....
 
Fursa zote kama kiongozi mtarajiwa wa nchi lazima ziwe explored.

Hii ina maana nchi majirani, nchi za kanda kama SADC, COMESA, AU - UMOJA WA AFRIKA na wadau wengine wa maendeleo lazima kuwa karibu nao kupunguza tofauti na pia kutengeneza fursa kwa Tanzania na waTanzania.

Hatuwezi kujifungia, Tanzania inaihitaji dunia kuliko dunia inavyoihitaji Tanzania hivyo lazima kuwa na mikakati ya ki-geopolitics kujenga ushawishi na kutafuta blocks za nchi zinazofanana nasi ili kuweza ku negotiate treaties, multilateral negotiaions n.k kwa kifupi kuwa na diplomasia-ya-kiuchumi imara kwa manufaa ya raia wa Tanzania na nchi kwa ujumla.

Heko kwa kamanda Tundu Lissu na CHADEMA kwa kuifungulia milango Tanzania iliyokuwa imejitenga na kukosa fursa kibao katika ulimwengu huu ambao umekuwa kijiji yaani mfumo wa Globalization.

Huwezi kujua ushindani au mapungufu ya nchi fulani kama hatutakuwa na diplomasi- ya-kiuchumi itakayo inyanyua Tanzania irudi katika nafasi yake husika kimataifa.
The quotation is from Otto von Bismarck, first Chancellor of Germany : There are no permanent enemies, and no permanent friends , only permanent interests Otto von Bismarck
hivi hao wa nje unadhani wanatupenda saaana!!!
hebu tumia akili yako, tule mfano wa nchi ambayo sisi tunaipenda saaaaana.
hakuna nchi kama hiyo.
kama uonavyo sisi yuko bizi na nchi yetu, na wao wa bze na maisha yao wenyewe vilevile
 
CHADEMA wanatakiwa kupeleka malalamiko rasmi tume ya uchaguzi na MCT kwa vyombo vya habari kugoma kutangaza matukio ya CHADEMA.

Huu ni ushauri mzuri, japo sioni kama watapata ufumbuzi wowote, maana anayeagiza vyombo vya habari visimtangaze Lisu, ana chuki ya wazi na Lisu, na ana nguvu kuliko hizo mamlaka zote.
 
aende akazungumzie hata akiwa bafuni.....hesabu zote tarehe 28 october 2020
 
WAMEGUNDUA NI MROPAKAJI MZURI TU,WANATAKA KUMTUMIA ILI NAYE APATE CHEAP POPULARITY.


This time hatucheki na wazee wa gia za angani na kuzungusha mikono,ni spanner tu.
 
Yaani mie huyu simuelewi kabisa, hivi wapiga kula wake wako kenya?, Watanzania wangapi wana access na hizo radio za kenya!
Kama mmewakataza wenye vyombo vy habari nchini kwenu wasimpe airtime yeye afanyeje??
 
Lissu ajielewi na hicho ndio kitu kikubwa kitakachomwangusha hata kama vyombo vya hapa havimpi nafasi bado wapiga kura wake wapo Tanzania.Toka mwanzo alivyoanza kufanya mahojiano na vyombo vya nje utaona kabisa matamshi yake hayaendani na nini wanachotaka watanzaniaa.Kuna mambo mengi ambayo watanzania wangependa kusikia toka kwake kama maswala ya pensheni za wafanyakazi na vitu vingine lakini yeye amejikita na mambo ambayo si tu hayamsaidii mtanzania bali pia hayakubariki.
 
August 10 2020
Mjadala mpana wa dakika 30 kwa njia ya simu na Tundu Lissu katika kipindi Jambo Kenya cha kituo cha Radio Citizen cha jijini Nairobi Kenya



Tundu Lissu anayewania kiti cha urais nchini Tanzania amesema kwamba viashiria vyote vinaonesha kwamba uchumi wa nchi hio umeenda chini miaka 5 iliyopita. Afafanua nenda mtaani uone biashara....Tanzania breweries mlipaji mkubwa wa kodi amepunguza uzalishaji...mifano ipo mingi.

Mgombea Urais Tanzania, Tundu Lissu amekiri kwamba hana imani na Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania amedai kwamba tume hio ni ya Rais Magufuli na chama chake cha CCM.
source: Radio Citizen
Source: CHADEMA TV MEDIA
Source: Erythrocyte
 
Lissu ajielewi na hicho ndio kitu kikubwa kitakachomwangusha hata kama vyombo vya hapa havimpi nafasi bado wapiga kura wake wapo Tanzania.Toka mwanzo alivyoanza kufanya mahojiano na vyombo vya nje utaona kabisa matamshi yake hayaendani na nini wanachotaka watanzaniaa.Kuna mambo mengi ambayo watanzania wangependa kusikia toka kwake kama maswala ya pensheni za wafanyakazi na vitu vingine lakini yeye amejikita na mambo ambayo si tu hayamsaidii mtanzania bali pia hayakubariki.
Mwaka huu mtavimba hata mtapasuka.

Mwambieni Meko aache ukandamizaji kwa vyombo vya habari vya Bongo la sivyo Lissu atatumia hata CNN kufikisha ujumbe kwa watanzania.
 
Huyu anatapatapa tu hana jipya, hoja zake za kitoto kabisa. Propaganda zake hazifai kabisa. Huyu ndiye mgombea urais wa chama fulani.
 
Back
Top Bottom