Fursa zote kama kiongozi mtarajiwa wa nchi lazima ziwe explored.
Hii ina maana nchi majirani, nchi za kanda kama SADC, COMESA, AU - UMOJA WA AFRIKA na wadau wengine wa maendeleo lazima kuwa karibu nao kupunguza tofauti na pia kutengeneza fursa kwa Tanzania na waTanzania.
Hatuwezi kujifungia, Tanzania inaihitaji dunia kuliko dunia inavyoihitaji Tanzania hivyo lazima kuwa na mikakati ya ki-geopolitics kujenga ushawishi na kutafuta blocks za nchi zinazofanana nasi ili kuweza ku negotiate treaties, multilateral negotiaions n.k kwa kifupi kuwa na diplomasia-ya-kiuchumi imara kwa manufaa ya raia wa Tanzania na nchi kwa ujumla.
Heko kwa kamanda Tundu Lissu na CHADEMA kwa kuifungulia milango Tanzania iliyokuwa imejitenga na kukosa fursa kibao katika ulimwengu huu ambao umekuwa kijiji yaani mfumo wa Globalization.
Huwezi kujua ushindani au mapungufu ya nchi fulani kama hatutakuwa na diplomasi- ya-kiuchumi itakayo inyanyua Tanzania irudi katika nafasi yake husika kimataifa.
The quotation is from Otto von Bismarck, first Chancellor of Germany : There are no permanent enemies, and no permanent friends , only permanent interests Otto von Bismarck