Zakaria Lang'o
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 2,593
- 2,768
Ndugu Watanzania wenzangu, hii ni rai yangu kwenu na ni kwa heshima kubwa napenda kuomba ushirikiano tukiwa wananchi wapenda haki na amani katika nchi yetu, kwamba tuwe tayari kumlinda ndugu yetu Tundu Antipas Lisu hapo atakapofika nchini tarehe 27/07/2020.
Kila mmoja wetu anaelewa Nini kilimpata Lisu mchana wa tarehe 07/09/2017 pale area D jijini Dodoma. Alimiminiwa risasi 38 na watu ambao serikali yetu inadai ni "wasiojulikana." Katika risasi zile 38, 16 ziliingia mwilini mwake. Aliumia mno, lakini Mwenyezi Mungu ni mwema, amepona na hatimaye ANARUDI nyumbani.
Nimemsikiliza akizungumza kwa uchungu jinsi ambavyo Jeshi la polisi halionyeshi kujali madhila aliyopata hata baada ya kuandikiwa barua juu ombi la kumpatia ulinzi. Hili linasikitisha sana. Ni udhihirisho wa wazi kuwa wale wasiojulikana ni dhahiri wana muunganiko na aidha serikali ya Tanzania au na Polisi wetu.
Nasema hivi kwa sababu nakumbuka kuiona na kuisoma tweet ya Mhe. Rais Magufuli usiku wa tarehe 7/9/2017 ikidai kusikitikia kilichotokea na kuahidi kuvitaka vyombo vya usalama kufuatilia na kwafikisha mbele ya sheria wale wote waliohusika. Hadi leo hakuna lolote lililofanyika zaidi ya vitendo vya dhahiri vya ukandamizaji dhidi ya haki za Lisu kama: kukataa kutoa fedha za matibabu ambazo ni stahiki zake; kumnyang'anya ubunge kwa jeuri tu bila kufuata taratibu za kisheria kulikofanywa na spika Ndugai!; mawakili wa serikali kuitaka mahakama ifute dhamana na kumkamata kama mtoro katika kesi wakati serikali ikifahamu fika juu ya madhila aliyoyapata na sababu za kutokuwepo nchini.
Hivyo basi kwa pamoja mwananchi mwenzetu anaporudi baada ya kupata masaibu yote yaliyomkuta tafadhali tujitolee kumlinda.
Kwa pamoja tuikemee serikali yetu iache tabia za ukatili dhidi ya Mwananchi wake, Tundu Lisu na wananchi wengine. Tuelewe kuwa tabia ya serikali kunyamazia ukatili wanaofanyiwa watu ni hatari kwa amani na usalama wa nchi yetu.
Ndugu Watanzania wenzangu nawaomba kwa umoja wetu tusikiachie kikundi kidogo Cha watu wajiitao "serikali" kiwadhulumu baadhi ya wananchi wake haki hasa ya kuishi kwa kudai tumewapa mamlaka au kwamba yamefanywa na " watu wasiojulikana." Hakuna Mwananchi aliye na uwezo wa kutoa mamlaka kwa yeyote kudhulumu haki za watu.
Kulingana na katiba ya nchi yetu Ibara ya 8 ".......serikali itapata madaraka yake kutoka kwa wananchi.
...... Lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi."
TUMLINDE LISU DHIDI YEYOTE MWENYE DHAMIRA CHAFU DHIDI YAKE, NI RAI YANGU KWENU WATANZANIA.
Asanteni.