Tundu Lissu amshangaa Rais Samia kumteua Alexander Mnyeti kuwa Waziri. Asema hana uadilifu

Tundu Lissu amshangaa Rais Samia kumteua Alexander Mnyeti kuwa Waziri. Asema hana uadilifu

Uzima Tele

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2023
Posts
1,270
Reaction score
2,822
Ni leo J'pili tarehe 3/9/2023 alipokuwa akiongea na wananchi katika Kijiji cha Kiabakari - Butiama mkoa wa Mara katika mfululizo wa mikutano ya CHADEMA katika OPERESHENI +255 KATIBA MPYA, OKOA BANDARI ZETU - Tanganyika.


Video: By Mwananchi Digital

--
Rais Samia ameteua Baraza la Mawaziri, katika walioteuliwa yupo Alexander Pastory Mnyeti ambaye ni mbunge wa jimbo la Misungwi mkoani Mwanza. Mnyeti alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara kabla hajawa Mbunge. Mnyeti na madiwani walipitia wote bila kupingwa sababu aliyekuwa mgombea na madiwani kata 27 walienguliwa wote.

Lissu anasema tume ya Haki ya Binadamu na Utawala Bora ilimtia hatiani Mnyeti na kusema kuwa hana maadili ya kuwa kiongozi na ni mla rushwa kwa vitendo alivyofanya akiwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Lissu anazidi kusema kuwa Rais anayeteua watu waliotiwa hatiani na mamlaka aliyoiteua ina maana anaunga mkono wala rushwa na hana uadilifu.
 
Mnyeti ni mhuni asiyefaa hata uongozi wa Kijiji. Nadhani focus ya mama ni kujifungamanisha na sukuma gang. Sasa ameona aanze na Mnyeti
 
Samia hana nia ya dhati ya kupambana na Rushwa na Upigaji.
 
Back
Top Bottom