Tundu Lissu amshangaa Rais Samia kumteua Alexander Mnyeti kuwa Waziri. Asema hana uadilifu

Uzima Tele

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2023
Posts
1,270
Reaction score
2,822
Ni leo J'pili tarehe 3/9/2023 alipokuwa akiongea na wananchi katika Kijiji cha Kiabakari - Butiama mkoa wa Mara katika mfululizo wa mikutano ya CHADEMA katika OPERESHENI +255 KATIBA MPYA, OKOA BANDARI ZETU - Tanganyika.

Your browser is not able to display this video.

Video: By Mwananchi Digital

--
Rais Samia ameteua Baraza la Mawaziri, katika walioteuliwa yupo Alexander Pastory Mnyeti ambaye ni mbunge wa jimbo la Misungwi mkoani Mwanza. Mnyeti alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara kabla hajawa Mbunge. Mnyeti na madiwani walipitia wote bila kupingwa sababu aliyekuwa mgombea na madiwani kata 27 walienguliwa wote.

Lissu anasema tume ya Haki ya Binadamu na Utawala Bora ilimtia hatiani Mnyeti na kusema kuwa hana maadili ya kuwa kiongozi na ni mla rushwa kwa vitendo alivyofanya akiwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Lissu anazidi kusema kuwa Rais anayeteua watu waliotiwa hatiani na mamlaka aliyoiteua ina maana anaunga mkono wala rushwa na hana uadilifu.
 
WaTz tuacheni roho mbaya ,kesho na kesho kutwa Lissu anaweza kuwa Raisi na akawachagua anaowaona yeye wanafaa bado kutatokea waTanzania watamshangaa.
 
Mnyeti ni mhuni asiyefaa hata uongozi wa Kijiji. Nadhani focus ya mama ni kujifungamanisha na sukuma gang. Sasa ameona aanze na Mnyeti
 
Kwani hukumuona Lisu anajifanya anakoseasea badala ya alekzanda anasema Abdallah πŸ˜‚πŸ˜‚
Hizi siasa za aina hiyo ni hatari kwa umoja wetu wa kitaifa tuzikemee before it's too late.
 
Samia hana nia ya dhati ya kupambana na Rushwa na Upigaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…