Tundu Lissu: Bila kuwa na Uwazi na Uwajibikaji, CHADEMA itakufa

Tundu Lissu: Bila kuwa na Uwazi na Uwajibikaji, CHADEMA itakufa

Lisu akutane na wajumbe aongee nao hayo, aache kututafuta exist door kwa kuongea hovyo hovyo.

Wangapi huko SYW ni wajumbe/wapiga kura? Yeye kaamua kuiitaabisha chadema kwa kuongea chochote na lolote analolifahamu kwa yoyote bila kujali maswala ya ndani ya chama na yale ya public.

Mimi kwa mtizamo wangu naona Lisu anasema chadema haifai, na sijui anasubiri nini wakati aliishasema, chadema ikiacha misingi yake anaondoka kwasababu chadema siyo baba wala mama yake.

Kwanini haondoki kama chama kimeoza kiasi hicho, anasubiri nini?
 
Nguvu ya chama cha siasa ni public support not infighting za power struggle baina ya viongozi; huko ni kukidhoofisha chama na kukipotezea imani kwa wapiga kura.

Lissu hafai kwa nafasi ya uongozi, hata kama kweli Mbowe kaishiwa pumzi mara 1000% ya Heche ni ropo-ropo mno.
Yote haya ni upuuzi mtupu.
Mambo ya Mbowe yamekwisha fahamika. Hana jipya tena analoweza kulileta CHADEMA, mbali ya kujitafutia maslahi mwenyewe na wanao mzunguka.

Wewe huna 'credentials' za namna yoyote ya kumjuwa ni kiongozi gani anafaa kuiongoza CHADEMA Kutokana na hulka zako ulizo onyesha humu Jukwaani, tokea uingie, sinamashaka hata kidogo kwamba wewe siyo mtu wa kukusikiliza kwa lolote la maana. Huna ushauri wowote unao weza kumfanya mtu auchukulie kwa makini. Unatawaliwa sana na 'pomposity' za kutaka uonekane unajuwa mambo; hata bila ya kupima usahihi wa hayo mambo katika hali ya matatizo yaliyopo.

You're useless.
 
Kwa kweli Lissu anazidi kujipambanua; kuwa tofauti kabisa na haya magenge ya viongozi wachafu yaliyopo sasa hivi madarakani na huko kwenye vyama vya upinzani.

Yeye amejipambanua kuwa tofauti kabisa.
Kama mtu unashindwa kuelewa haya yaliyo semwa na Tundu Lissu hapa; siyo kwamba huna akili za kuelewa, bali ni kuwa akili zako zimetekwa, kuna sababu maalum zinazo kuzuia kuelewa./kukubali yanayo zungumziwa.
Chawa wanajitoa ufahamu tu lakini wanajua kabisa kuwa Lissu yuko sahihi. Kama mnafanya mambo ya hovyo kama unadhirifu na uminyaji wa demokrasia ndani ya chama chenu mnapata wapi moral authority ya kuikemea CCM kwa mambo hayo hayo?
 
Usiwe king'ang'anizi tu wa hoja bila kutumia akili kufikiri.
Maswala ya CHADEMA yameongelewa sana ndani ya Kamati Kuu ya chama hicho. Hata siku moja hukusikia yaliyo kuwa yakiongelewa huko.
Uwezekano wa kuyafumbua matatizo huko ndani umeshindikana na juhudi za kuendeleza ubovu huo zikiendelea. Sasa wewe ulitaka nini kifanyike; kuendelea kulea uozo huko huko ndani kwa jina la 'collective responsibility', au kuchukuwa wajibu wa kukiokoa chama!
Chama siyo mali ya mtu, au ya viongozi, ni mali ya wananchi.
Kwa hiyo sasa maswala yameletwa kwa wenye chama, waamue. Hizo siri unazo taka zifichwe ni zipi, hasa; unaweza kuzitaja?
Una hakika ni siri za chama, au ni za watu binafsi; hata kama ni viongozi wa chama?

Kwa nini wewe na wengine mnakazania sana madudu ya mtu/watu binafsi na wala siyo ya chama yalindwe? Chama kinafaidika vipi na hawa watu kufichiwa hizo siri?

Siri za watu binafsi zinazo kidhoofisha chama zifichwe, kwa jina la 'collective responsibility', kwa nini?
Hatua ya kwanza kwenye any organization set up kama hukubaliani na maamuzi ya wenzako kwa tofaut kubwa ni ku resign nafasi zako zote..

Hakuna leadership ya maana bila principle...

Hisia huwa zinaisha yanaanza majuto
 
I highly doubt if you were in your right mind when you decided to expose your idiocy in public!

Ngoja nikwambie kitu kandombo..
The car you're riding wont take you far....

Sasa how does my ideocy in public bother your a$$ in any meaningful way?
 
Ngoja nikwambie kitu kandombo..
The car you're riding wont take you far....

Sasa how does my ideocy in public bother your a$$ in any meaningful way?
Kesha piga vyombo vya si unajua holiday hizi..

Watu ana wa-quote yeye, akijibiwa anakuja lugha zake mbofu-mbofu.

Hovyo kweli
 
Ingekuwa rahisi hivyo kuongelea mambo ya ndani katiba za taasisi nyingi zisingeweka kipengele cha kuwataka wajumbe watunze siri za vikao.

Au hata makampuni makubwa huko duniani wasingeweka kipengele cha ‘restrictive covenant’ kinachozuia watu walioshika nafasi za senior designers na other senior strategic planning posts; kuweza kuacha kazi tu wenyewe bila ya kufukuzwa halafu uende kwa mshindani wao. Hilo halipo una siri zao, ndio maana unawekwa kipengele kitakacho kuzuia kwenda huko walau ipite miaka miwili kwanza baada ya kuacha kazi usipeleke mbinu zao huko.

Same kuna shida CDM kwa maelezo ya Lissu, lakini kwa nafasi yeye sio mtu wa kuongea; tena akiwa bado makamu mwenyekiti (kiongozi). Walau angekuwa ameachia hiyo nafasi kwanza ndio aongee, ata kama anagombea uenyekiti.

Lissu hana sifa ya uongozi kwa tabia zake. Hajui hata negotiations ni give and take; you don’t get everything in negotiations. Yeye ukisikiliza unaona kuna demands wakati hana upper hand kwenye bargaining power.

Lissu hatoshi, na Mbowe amepwaya.
Hizo Siri zinazotakiwa kutunzwa siyo za wizi baba.

Au kwenu nyie Wachaga wizi siyo haramu?
 
Elewa neno taasisi yenye manufaa ya umma. Kuna vitu vinapaswa kuwa wazi kabisa, mfano mapato na matumizi. Wala usijaribu kupinga.
 
Ebu leta mfano mmoja duniani ambapo kiongozi anaponda chama chake akiwa bado ni sehemu ya vikao vikuu vya chama au serikali.

Hata Ruto alipoanza campaign zake aliachana na shughuli za serikali tena ilikuwa ya mseto.
Wakati wa sakata la G55 la wale wabunge waliokuwa wanadai Tanganyika yao wakiongozwa na Njelu Kasaka ulikuwa na umri gani? Nyerere akiwa mwenyekiti mstaafu na mjumbe wa kamati kuu ya CCM aliwazodoa wazi viongozi wake akianza kwa kumsema mwenyekiti (Mwinyi) kuwa ni dhaifu na kuwa anapelekeshwa na akina Malecela (PM) na Kolimba (KM),alifikia hata hatua ya kuwaandikia kitabu "Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania"
 
Huo ndo ukweli, tupende tusipende, mfano tunapinga kuweka ukomo kwenye uongozi wa chama, siku ccm wakipeleka bungeni mswada wa kuondoka ukomo wa urais tusipige makelele
Mbowe
Anahubiri demokrasia ambayo yeye mwenyewe hana
Upinzani tz hawaaminiki.
 
Uwazi na uwajibukaji ndo utafanya CHADEMA idumu sio kuficha Uovu. Amyeaongea hayo kwenye Clubhouse alipoulizwa kwamba haoni kama kuongea mambo kwa Uwazi kunaua Umoja wa kitaifa wa chama? Kwanini asionhelee mambo ndani?

Kufanya mambo kwa Uwazi kunaleta uwajibikaji.

Wananchi wanatakiwa waambiwe mapato na matumizi sio kuficha ficha.

Wanadai eti kusema maovu kwa uwazi kunaua umoja wa chama kwamba yazungumziwe ndani.

Lissu amesema kama Uwazi ni jambo baya, basi tukubaliane uwazi ni jambo baya.

Hivyo hata CCM wanapofanyia gizani mambo ya kuhujumu taifa kama kuuzwa kwa bamdari tusipige kelele.

Amesema mambo ya kufanyia mambo gizani mara nyingi yanakuwa ni nia ovu. Wanapotumia madaraka yao vibaya, wanapotumia fedha za Umma vibaya na mambo yote yanayofanyia gizani tusipihe kelele. Tukubaliane Uwazi kwa CCM ni jambo baya hivyo hivyo na ndani ya chama tukubaliane Uwazi ni jambo baya unahatibu umoja wa chama.

Lissu amesema anacjofahamu ni mihimu kuwe na uwazi kwenye shughuli za Chama. Tunaficha nini na kwanini?

Kwanini tunaficha kwa mfano matumizi ya fedha za chama? Tunamficha nani na kwanini?

Mambo ya Umma yawe hadharani. Giza linazaa abuse Giza linazaa matumizi mabaya ya madaraka. Vitu vinavyo zungumzwa gizani hata visipo tekelezwa hakuna anayeweza kujua.

Chama cha mageuzi kama chadema hakiwezi kikakumbatia giza halafu tukasema sisi ni chama cha mageuzi.

Tukifanya mambo gizani chama kitakufa. Mtu asije kujidanganya kwamba chama hakiwezi kufa mfano ipo mingi. Hata UDP ilikuwa kubwa kuliko chadema.

Kwahiyo Uwazi utatufanya tuishi maisha marefu kuliko kukumbatia giza.
Lissu ataropokaaaaa mwisho wa siku uwenyekiti hatoupata. Na kwa tabia ya Nyumbu wa Chadema, baada ya wiki watamsahau kama walivyosahau maandamano ya Mange Kimambi! Ahahahahaha!!!
 
Ingekuwa rahisi hivyo kuongelea mambo ya ndani katiba za taasisi nyingi zisingeweka kipengele cha kuwataka wajumbe watunze siri za vikao.

Au hata makampuni makubwa huko duniani wasingeweka kipengele cha ‘restrictive covenant’ kinachozuia watu walioshika nafasi za senior designers na other senior strategic planning posts; kuweza kuacha kazi tu wenyewe bila ya kufukuzwa halafu uende kwa mshindani wao. Hilo halipo una siri zao, ndio maana unawekwa kipengele kitakacho kuzuia kwenda huko walau ipite miaka miwili kwanza baada ya kuacha kazi usipeleke mbinu zao huko.

Same kuna shida CDM kwa maelezo ya Lissu, lakini kwa nafasi yeye sio mtu wa kuongea; tena akiwa bado makamu mwenyekiti (kiongozi). Walau angekuwa ameachia hiyo nafasi kwanza ndio aongee, ata kama anagombea uenyekiti.

Lissu hana sifa ya uongozi kwa tabia zake. Hajui hata negotiations ni give and take; you don’t get everything in negotiations. Yeye ukisikiliza unaona kuna demands wakati hana upper hand kwenye bargaining power.

Lissu hatoshi, na Mbowe amepwaya.
We ulitaka nani aongee?
 
Hatua ya kwanza kwenye any organization set up kama hukubaliani na maamuzi ya wenzako kwa tofaut kubwa ni ku resign nafasi zako zote..

Hakuna leadership ya maana bila principle...

Hisia huwa zinaisha yanaanza majuto
Bado huelewi chochote.
Hicho chama siyo cha mtu, siyo 'organization' ya Mbowe.
Ni kipi kinacho kufanya wewe uamini kuwa kutokubaliana na anayofanya Mbowe, uamzi sahihi ni kumpisha Mbowe?
 
Ngoja nikwambie kitu kandombo..
The car you're riding wont take you far....

Sasa how does my ideocy in public bother your a$$ in any meaningful way?
Your own carriage is already stuck in the mud, mine is still "riding..."; and that is a very big difference between the two of us.
 
Back
Top Bottom