Mimi huwa sina unafiki; hilo lielewe kwanza.
Ushauri wako nauelewa na najuwa nia yako njema. Lakini angalia unavyo kuwa hakimu mwenyewe hapa!
Ni kitu gani ambacho umeona "siyo kweli"?
Na kama kweli unayaamini haya maneno yako hapa; moja kwa moja ungetambuwa kuwaunaninyima haki yangu, au siyo? Mimi siruhusiwi kuwa na "...uhuru wa manoni na mitizamo yangu..."? Mbona unataka kunifungia?
Mkuu 'Mizania', elewa tu kwamba maswala haya yanayo zungumziwa humu JF, siyo mzaha, siyo utani. Ingekuwa ni mkutano pale uwanjani, watu wangetiana ngeo vichwani, na hata kuuana. Haya maswala ya nchi yetu ni vita.
Napenda sana kuwa na staha, mahali ambapo kuna staha. Humu ndani hakuna staha. Huyu unaye mtetea hapa naona hujui historia yake humu. Huyu ni mtu ambaye alikwisha diriki hata kuandika humu humu kwa furaha kabisa yaliyo mpata Tundu Lissu alipo koswa koswa na zile risasi; na hapo hapo akaendelea kuhimiza wengine wamalizie kazi hiyo iliyo shindikana huko nyuma.
Sasa nikuulize wewe; kwa nini hukusema lolote wakati mtu huyu akitumia uhuru wake kujieleza?
Mwisho. Nia yako njeama naitambua, lakini kwa bahati mbaya hutambui vita kubwa inayo endelea nchini mwetu wakati huu.