Usiwe king'ang'anizi tu wa hoja bila kutumia akili kufikiri.
Maswala ya CHADEMA yameongelewa sana ndani ya Kamati Kuu ya chama hicho. Hata siku moja hukusikia yaliyo kuwa yakiongelewa huko.
Uwezekano wa kuyafumbua matatizo huko ndani umeshindikana na juhudi za kuendeleza ubovu huo zikiendelea. Sasa wewe ulitaka nini kifanyike; kuendelea kulea uozo huko huko ndani kwa jina la 'collective responsibility', au kuchukuwa wajibu wa kukiokoa chama!
Chama siyo mali ya mtu, au ya viongozi, ni mali ya wananchi.
Kwa hiyo sasa maswala yameletwa kwa wenye chama, waamue. Hizo siri unazo taka zifichwe ni zipi, hasa; unaweza kuzitaja?
Una hakika ni siri za chama, au ni za watu binafsi; hata kama ni viongozi wa chama?
Kwa nini wewe na wengine mnakazania sana madudu ya mtu/watu binafsi na wala siyo ya chama yalindwe? Chama kinafaidika vipi na hawa watu kufichiwa hizo siri?
Siri za watu binafsi zinazo kidhoofisha chama zifichwe, kwa jina la 'collective responsibility', kwa nini?