Tundu Lissu: Kufa kwa Magufuli ni 'Poetic Justice'

Tutajua mengi, kama, kama tu CCM itakubali scrutiny. Mh. Lissu anajua 'mengi' ipo siku! aliwahi kusikika akisema. Mh. Tundu Lissu hajawahi kusema Hayati Magufuli ndiye aliyempiga Risasi, tuache kupotoshana kana kuwa Magufuli ndiye aliyefanya hivyo.

Msimlishe maneno.

Bahari, maziwa, mito, visima yatakaushwa, mawe yatapinduliwa hati ikibidi yasukumwe kwenda milimani Ukweli lazima upatikane ili wote ambao wameumizwa na sakata hili wapate amani.

Binafsi nateseka sana, mmoja amepotea na inawezekana amekufa, mwingine kapigwa risasi karibu afe... na wote hawa sijawahi kukutana nao, mmoja tulikuwa mstaari mmoja katika kuchagiza ukweli, kuomba haki zitendeke....God knows we were pleading for christake! wakati nilianza kukata tamaa hapa jamvini, aliniinua....mwingine huyu nilimwandika vibaya humu siku mbili tatu baadae akatandikwa risasi, walahi nilikimbilia kufuta Posti kama sio Uzi ule kwa ajili niliona kama nilikuwa mchonganishi, Max Anaweza kutafuta posti ile... TL et al

Jamani haijalishi, watu pande zote wameumia, wanaumia na Wataumia naumia kuona tuanpoenda nikule kule kwa hivi vijembe na kejeli tunavyoviona havina impact katika jamii., kwa watu, na Familia zao

Tuwe wakweli, tuandike ya kweli. Yale ya kuambiwa, "tuongeze na zetu" Tuwakemee, Tuwakosoe, tuwanyooshe wale wanaopotea kijumla, Tujibishane kwa hoja na mijadala yenye Tija....Kuna watu wenye uwezo mkubwa humu lakini ukikutana na vurumai humu saa nyingine mshike mshike unamtwanga hata anayekuja kukusaidia au unatwangwa na unayeenda kumsaidia....yoote hiyo ni kwa ajili ya ujengaji wa jazba from the get go! Tuepuke na "twende moja kwa moja kwenye mada" siyo ya kwetu hayo, siyo ya lugha za siasa Tanzania


....naenda kazini, ninywe kahawa na sambusa yangu nitarudi nikipunguza jazba.

Amani iwatandae.

Aluta Continua.
 
Hawa watu WALIKUWA wanachonganishwa pasipo wao kujua kuwa walikuwa wanachonganishwa. KWA hiyo kwa sasa unatakiwa uwaunganishe ZAIDI badala ya KUENDELEA kuwachochea
 
Ni uongo mkubwa, acha kumjaza TL uwongo kisa alikuwa mpinzani mkubwa wa Magu!
 
Kila unachofanya Duniani kina matokea yake,ukipambana na serikali yoyote matokeo ni kifo au uhame nchi husika.
Ndiyo maana Mwandishi Asange anawindwa na Marekani mpaka Leo kwa sababu za kudukua mawasiliano yake.
Kwahiyo kuwa mpinzani wa hoja za serikali adhabu yake ni kupigwa risasi ama!!??? Nchi hii tulifika hatua mbaya sana kidemokrasi na kipindi cha Magu, binafsi najihisi niko Hai tangu ile March 2021 jiwe kuondoka.
 
Tundu Lissu itachukua muda sana kugundua watu gani walihusika kushambuliwa kwake, kuna siku atakuja muomba msamaha Hayati JPM.
Hivi mpaka sasa hajui kuwa kushambuliwa kwake kulitokana na kutishia kiti cha mwenyenacho?
Kama hajui hilo basi atakuwa one of the dumbest dudes of our time!
 
Kwani Tundu Lisu, hata kufa ? hataishi milele, Naye hakifa tushangilie kifo chake ?

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Utashangilia kifo cha Lisu, kwani yeye amemwua nani? Amemdhulumu nani? Amembambikia kesi za uhujumu uchumi nani?

Kifo cha mtu hatari kwa maisha ya wengine, ni faraja kwa waliosalia, lakini kifo cha mtu mwema ni masikitiko na huzuni kubwa kwa walio wazima.

Biblia pia inasema kuwa mtu mwovu dhidi ya wenzake akifa huwa na furaha lakini mtu mwema akifa huwa na huzuni.

When a wicked man dies, his hope perishes; all he expected from his power comes to nothing.8The righteous man is rescued from trouble, and it comes on the wicked instead.9With his mouth the godless destroys his neighbor, but through knowledge the righteous escape.10When the righteous prosper, the city rejoices; when the wicked perish, there are shouts of joy.

10Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi; mwovu atowekapo, kuna kelele za furaha.
 
Hivi mpaka sasa hajui kuwa kushambuliwa kwake kulitokana na kutishia kiti cha mwenyenacho?
Kama hajui hilo basi atakuwa one of the dumbest dudes of our time!

Hizo theory tu kila mtu anayake. Lakini hakuna hata. Mmoja atajua ukweli .
Anybody akikoswa kuondolewa uhai wake atamchukia sana yule anaedhani anahusika. Ukoswe kupoteza uhai in the most painful way halafu ucheke ucheke hovyo? Lazima uwe aggresive kama binadamu.
 
10Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi;

mwovu atowekapo, kuna kelele za furaha.
 
10Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi;

mwovu atowekapo, kuna kelele za furaha.
 
Kama CCM walitufundisha kuimba Iddi Amin akifa mim siwez kulia, nutamtupa kagera awe chakula cha mamba, wakat ukatili wa huyo mtu sis wengne hata hatukuuona. Kwa nin saiv mnatutaka kusikitikie kifo cha katili tulie mshuhudia kwa macho yetu wenyew. Yaan mnataka kila kitu kutuelekeza mnachotaka nyie ndo tukifat, jambo baya hadi nyie mtuambie kua hili ni baya hata km tunaliona kwa macho yetu wenyew. Nyie lilieni mungu wenu mliemwabudu sisi tufurahie kuondoka kwa mtesi wetu tusiingiliane. Tuwe na uvumilivu wa kisiasa kama tulivofundishwa, Period.

Sent from my CPH2159 using JamiiForums mobile app
 
Mimi huwa sikubaliani sana na Lissu katika misingi ya kisiasa, lakini katika hili la kifo cha Magufuli naunga mkono.
Binadamu tunalipa makosa yetu hapahapa duniani.

KARMA.
Hata vitabu vitakatifu na vya kale vilisema auaye kwa upanga, hufa kwa upanga au binadamu atakunywa kipimo kile kile alichowapangia wengine.

Siyo bure kwamba wasiojulikana sasa wamepotea.
 
Kasoro Sukuma gang kama wewe na wanufaika wachache ndiyo hawakuomba, ila Watanzania wengi walimlilia Mola awaondolee lile balaa na Mola akasikia kilio chao akaliondoa kwa Corona
Kumbe unajua kila mtu atakufa ikiwemo na wewe mwenyewe.Nikadhani wewe ni Immortal.Hayo ya watanzania wengi waliomba ni porojo zako tu.
 
Mimi ni mpinzani, Magufuli alitufanyia makubwa, kitendo Cha kusema vibya Magufuli 2025 tuna pingia Kura CCM.
 
Ni Mungu ndiye aliyetuokoa sisi tuliopitia mateso ya mwendazake, kwa hiyo kifo cha magufuli mimi nilishangalia na huwa nashangilia mpaka leo
 
Mfano Lissu angekuwa baba yako halafu akapigwa risasi zile ungemfurahia Magufuli?
Kwani mmejuaje kama alipigwa nao, kwa nini msipanue wigo na kusema kapigwa na maadui ndani ya chama chake...watu wanaweza wali take advantage ya mahusiano na Serikali
 
Mfano Lissu angekuwa baba yako halafu akapigwa risasi zile ungemfurahia Magufuli?
Hivi Leo ukija gundua kumbe adui alikuwa ndani ya chama chake utasemaje...do you think it's impossible..?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…