Mwaka 2016 mpaka 2020 Tanzania iligubikwa na makelele ya Tundu Lisu aloyejiona yeye tu ndiyo mwenye haki ya kumshauri rais wa nchi wa wakati huo na ni lazima ushauri wake ufuatwe!
Hata hivyo hayati Magufuli alisimama imara na kupuuza makelele yote ya wakala wa mabeberu Tundu Lisu.
Kama hayati raisi Magufuli asingekuwa imara na akasikiliza makelele ya Lisu, haya hapa yangetokea Tanzania.
1. Tanzania tusingekuwa na bwawa la kufua umeme ambalo ni moja ya mabwawa makubwa barani Afrika. Urefu wa bwawa la Nyerere ni km100 yani sawa na urefu wa kutoka Dar mpaka Chalinze.
Tundu Lisu kwa kutumiwa na mbabeberu kwa ahadi ya kumlisha yeye na familia yake pamoja na kumpa hifadhi Ubelgiji alipinga sana ujenzi wa bwawa hili kwa kisingizio kwamba litasababisha uharibifu wa mazingira na mvua hazitanyesha tena Tanzania!. Leo mwaka 2023 bwawa linajazwa maji na Tanzania imegubikwa na mafuriko kila sehemu kwani mvua zinanyesha sana kinyume na utabiri wa Tundu Lisu.
2. Tanzania isingekuwa na ujenzi wa SGR.
Tundu Lisu alipinga sana ujenzi wa reli hii ya umeme na yenye kasi zaidi Afrika yote.
3. Serikali isingehamia Dodoma.
Tundu Lisu na Mbowe walipinga sana serikali kuhamia Dodoma wakisema huko ni kutesa watumishi na kwamba serikali ibaki tu Dares salaam kwa ndoto za mwl Nyerere zimepotwa na wakati. Hayati Magufuli aliziba masikio na leo serikali yote ipo Dodoma.
4. Kampuni ya madini ya Acacia ingekuwepo.
Licha ya kwamba Lisu amesoma kwa kodi za watanzania lakini aligeuka kuwa mwanasheria wa Acacia na akasema ataisaidia kutushitaki MIGA, kama tukiendelea kuwadai hela za wizi wa makinikia. Hayati Magufuli aliendelea mbele hadi kampuni ya Acacia ikafutwa na kuzaliwa kampuni mpya ya Twiga ambayo watanzania wapo kwenye management na Tanzania yakafunguliwa masoko ya madini kila sehemu, na watanzania wakanufaika na madini yao.
5. Kenya na India zingeendelea kuongoza kwenye uuzaji wa madini ya Tanzanite .
Kutokana na ukweli madini ya Tanzanite yanapatikana Tanzania tu. Hayati Magufuli alichukua hatua kali sana za kudhibiti madini ya Tanzanite ikiwemo kujenga ukuta wa kuzunguka mgodi huo, hatua hizo zilipingwa mno na Lissu na akaita ni udikteta mkubwa kufanya hivyo