Pre GE2025 Tundu Lissu: Kuna Rushwa inatuvuruga ndani ya CHADEMA

Pre GE2025 Tundu Lissu: Kuna Rushwa inatuvuruga ndani ya CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbowe keshalamba mpunga, halafu hataki kukubali ukweli. Zaidi zaidi amegundua kwamba chama kinaweza kumpa utajiri mwingi zaidi kwa njia rahisi kabisa.

Nasikia analamba mpunga halafu anawaambia wajumbe kwamba, najilipa kwasababu nilishawahi kukikopesha chama huko nyuma.

Mazuzu nayo yanakubaliana tu 🤣🤣
Mbowe anajua siasa kwamba Cha muhimu ni kuwa na Wabunge sio kuhangaika na Urais wa kina Lisu ambao hawawezi kuupata.
 
..mpunga umetoka kwa nani?

..au umetoka kwa Mama Abduli?

..yeye Mama Abduli amegawa nini, mpaka kuwa na mpunga wa kutuvurugia vyama vyetu?
 
..mpunga umetoka kwa nani?

..au umetoka kwa Mama Abduli?

..yeye Mama Abduli amegawa nini, mpaka kuwa na mpunga wa kutuvurugia vyama vyetu?
Mpunga umetoka kwa mdhamini mkuu, a.k.a Boss Lady ambaye hali akifahamu fika kwamba akitoa mpunga kwa masharti atakivuruga chama, alifanya hivyo kwa maksudi.

Hii resentment ya kina Msigwa na Lissu ilianza tangu kipindi cha Mwenyekiti kulambishwa asali, huu uchaguzi wa juzi was the last straw to break a camel's back.​
 
CCM ishakuwa mavi ya kale, iko madarakani kwasababu ya vyombo vya dola. Hakuna chama pale.

Ila CHADEMA, hata madaraka hawajagusa washaanza kuishi kama CCM, unataka tuwaelewaje kweli ?

Mbowe is obsessed with worldly possessions as an Ottoman Pasha.​

..hata Mama Abduli naye amepagawa na madaraka ndio maana anavuruga vyama vya upinzani.

..yanayotokea kwa Chadema yalishatokea kwa Nccr, na Cuf, na chanzo ni fedha zilizotoka Ccm.
 
Mpunga umetoka kwa mdhamini mkuu, a.k.a Boss Lady ambaye hali akifahamu fika kwamba akitoa mpunga kwa masharti atakivuruga chama alifanya hivyo.

Hii resentment ya kina Msigwa na Lissu ilianza tangu kipindi cha Mwenyekiti kulambishwa asali, huu uchaguzi wa juzi was the last straw to break a camel's back.​

..end of the day tunaoumia ni wananchi.

..bila kumuadabisha Boss lady hali hii haiwezi kubadilika.
 
Mbowe anajua siasa kwamba Cha muhimu ni kuwa na Wabunge sio kuhangaika na Urais wa kina Lisu ambao hawawezi kuupata.
Sasa watu wenye mawazo ya hivi ndiyo mnanufaika na The Status Quo. Kiufupi Tanzania inahitaji mabadiliko makubwa ya kimfumo ili itoke hapa ilipo.

Yaletwe na CCM au upinzani, I simply don't care. Ila huu upuuzi wa kugeuza siasa kama ajira, huku nchi ni masikini halikubaliki kabisa.​
 
Mimi sinufaiki na yeyote na Wala sitegemei kwamba Kuna mwanasiasa ataninufaisha so kwangu mambo ye u ya siasa sio jambo la msingi ni kama burudani tuu Kwa sababu nafahamu hakuna mwanasiasa wa kukusaidia hapa Duniani.
 
Hakuna uchaguzi usiokuwa na rushwa. Hata wa umonita tu watoto wanajribu kuhonga. Badala ya kulalamika ahakikishe kuwa chama chake kinachukua hatua thabiti kukabiliana na tatizo. Yeye kama Makamu Mwenyekiti kuendelea kulilalamikia hadharani halisaidii sana. Sana sana linaleta wazo pia kuwa bosi wake ama anahusika au halitilii maanani. Ameishasema, tumemuelewa. Sasa awashuhulikie wala rushwa na watoa rushwa wote katika chama chake.

Amandla...

Ninakazia:

Kujaribu kuwazodoa kina Mandela, Nyerere, Lissu, nk ni kujidhalilisha!
 
..hata Mama Abduli naye amepagawa na madaraka ndio maana anavuruga vyama vya upinzani.

..yanayotokea kwa Chadema yalishatokea kwa Nccr, na Cuf, na chanzo ni fedha zilizotoka Ccm.
..end of the day tunaoumia ni wananchi.

..bila kumuadabisha Boss lady hali hii haiwezi kubadilika.
Tayari Boss Lady ashashindwa huu mchezo. Watakaomwadabisha ni wale wahuni waliomuweka madarakani kiharamu 2021 ambao anajidanganya kwamba anaweza kuwazunguka kisa ana dola.

Hivyo wala usihofu, there's no honor among thieves wataparurana tu. Ila ambacho sisi na upinzani tunatakiwa kufanya ni kujiandaa kuokota Spoils of the coming war.​
 
View attachment 3064424
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara Tundu Lissu akizungumza katika mtandao wa kijamii wa Clubhouse amenukuliwa akisema

"Kuna tatizo la rushwa ya uchaguzi, yeyote anayesema hakuna tatizo anatudanganya, kuna tatizo la rushwa ya uchaguzi na rushwa ya uchaguzi ya mtu yeyote yule ni adui wa demokrasia na ni adui wa haki, kiongozi yeyote anayepatikana kwa kununua wapiga kura huwauza siku ikifika, kwa hiyo nilichokisema Iringa ninakisimamia kama nilivyokisema, kuna tatizo la rushwa linatuvuruga CHADEMA.

Tuangalie sisi wapika kura tuwe macho na wagombea wanaokuja kwa sababu wamenununua kugombea kwao, kwa sababu wamehonga ili wateuliwe wagombea, kwa sababu wamechafua ili waje wapate nafasi za kugombea na kuchaguliwa, Ninasimamia katika kile nilichokisema Iringa na tuwe macho"-

JAMBO TV
Lisu yuko sahihi, tunataka viongozi wanaoweza kusimama hadharani na kukemea rushwa kuanzia ndani ya chama chake. Ni wendawazimu kukemea rushwa ndani ya ccm na serekali, kisha kufumbia macho rushwa ya ndani ya cdm.
 
Mimi sinufaiki na yeyote na Wala sitegemei kwamba Kuna mwanasiasa ataninufaisha so kwangu mambo ye u ya siasa sio jambo la msingi ni kama burudani tuu Kwa sababu nafahamu hakuna mwanasiasa wa kukusaidia hapa Duniani.
Haya ni maneno ya kupaka rangi upepo.

Ndiyo, mwanasiasa hawezi kukusaidia lakini mfumo unaweza kubadilisha maisha yako, kwa jema au baya.

Leo hii hao wanasiasa wakicheza na mfumo, hata wewe unayejitia hunufaiki hapa unaweza kujikuta ni mkimbizi au marehemu kama ilivyokuwa Uganda, Rwanda, Burundi na Congo.​
 
Hakuna Cha mfumo wewe,pesa zitatafutwa Kwa mfumo wowote na siku zote mtafuta pesa anacheza na akili ya aliyeko madarakani
 
Usifananishe kabisa CHADEMA na CUF au NCCR. CHADEMA ndiyo chama pekee cha upinzani chenye mwelekeo.

kuwahi kutokea hapa Tanzania. Wanapoanza kuishi kama CCM au ACT sisi hatuwezi kuwaelewa. Kila mtu tangia Zitto, Slaa, Msigwa na kipindi ni Lissu wanaondoka kisa kugombana na Mbowe, sasa aidha wao ndiyo wako na tatizo au Mbowe ndiyo shida.

Wewe huwezi kuwa unagombana na kila mtu, na kila siku wewe ndiyo unaonewa na kuhujumiwa tu. Haiwezekani.

Something is not right.​
Na wakigombana na Mbowe wanakimbilia wapi? Tuanze hapo.

Amandla...
 
Back
Top Bottom