Tundu Lissu kurejea Nchini January 25, 2023

Tundu Lissu kurejea Nchini January 25, 2023

Shetani ana nguvu sana hapa duniani kwa wanaotanguliza matumbo. Kuna € m50 imetolewa, lazima ionekane kazi inafanyika.

..una maana barrick walimhonga magufuli?

..sukuma gang wakikusikia watakutafuna mzimamzima.
 
Rais wa awamu ile aliwasakama sana kupita kiasi.

Ilisemekana alitaka kuufuta
kabisa nchini.

Lakini kumbe Upinzani uko ndani ya mioyo ya watu.

Sasa werevu wanajiuliza iwapo alikuwa na nia thabiti ya kweli ya uadilifu Kwanini alichukia upinzani?

Je mbona ilipaswa kushirikiana nao kufanya kazi na kuwatumia Kama watch dogs ?

Je jamaa si wangetumika kumstua mahala Penye upigaji ambapo yamkini yeye angekuwa bado hajafahamu?
Binafsi nilitegemea ujio wa Lissu ungekuwa habari kubwa kila kona ya nchi. Lakini Mandonga anaiteka mitaa kuliko Lissu hii ni hatari kwa upinzani. Kama hakuna mtu anastuka presidential candidate ametangaza comeback ujue kazi ni kubwa uko mbeleni...mjipange sana
 
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Mhe. Tundu Lissu ametangaza kurejea rasmi nchini January 25, 2023 saa 7 mchana baada ya kukaa uhamishoni kwa muda mrefu.

View attachment 2479728

"Hatuwezi kuendelea kuishi uhamishoni bila ukomo. Hivyo basi, ninapenda kuwafahamisha kwamba, panapo majaliwa, nitakanyaga udongo wa ardhi ya Tanzania kwa mara nyingine tena siku ya Jumatano ya tarehe 25 Januari, 2023, majira ya saa saba na dakika 35 mchana." amesema

Ameongeza, “Kwa muda huo, ninatarajia kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, Dar es Salaam, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia nikitokea Brussels, Ubelgiji, kwa kupitia Addis Ababa, Ethiopia. Nitafurahi sana kwa mapokezi yoyote siku hiyo."

Kuhusu suala la Katiba Mpya, Mhe. Lissu amesema “Kwa vyovyote itakavyokuwa, mwaka huu utakuwa mwaka muhimu sana katika historia ya nchi yetu. Ni mwaka ambao, kama tukiamua kwa dhati ya mioyo yetu, tutapata Katiba Mpya na ya kidemokrasia, yenye mfumo huru wa uchaguzi, inayojali na kulinda haki za wananchi na inayoweka misingi imara ya uwajibikaji wa viongozi wetu kwa wananchi na wawakilishi wao.”

Anarudi nyumbani kuja kushiriki katika kuandika ukurasa wa kwanza mpya wa kitabu chenye kurasa 365 cha mwaka huu wa 2023, anaamini kwamba, kwa umoja wetu na kwa mapenzi yetu kwa nchi yetu, tutaandika kitabu kizuri.

Mwanasiasa huyo machachari, Mbunge wa zamani wa Jimbo la Singida Mashariki ambae pia ni mwanasheria Nguli nchini alinusurika kifo baada ya kushambuliwa kwa risasi za moto na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 wakati vikao vya Bunge vikiendelea Jijini Dodoma.

Pamoja na kutangaza kurejea kwake, bado ameonesha wasiwasi juu ya mambo mbalimbali yasiyo ya kawaida yanayoweza kutokea wakati huo. Hata hivyo, anaamini kuwa Mungu anaiwazia mema nchi hii.

"Ninafahamu kwamba, licha ya ahadi ya Mheshimiwa Rais na licha ya utayari wangu na wetu, siku zijazo hazitakuwa rahisi. Ninajua kuwa tutakabiliwa na majaribu ya kila aina na tutapitishwa katika tanuru kubwa la matatizo na magumu mengi."

“Mwenyezi Mungu anatuwazia sisi Watanzania “mawazo ya kutustawisha na wala sio ya kutuumiza, mawazo ya kutupa tumaini kwa siku zetu zijazo. Tukiweka nia ya dhati na kuitekeleza kwa dhati, tutayashinda majaribio na magumu yaliyo mbele ya safari yetu."

Chanzo: Twitter Spaces (Tundu Lissu)
Sasa sawa, amekuwa mlokole ananukuu mandiko ya Biblia?
 
"Sikutoa salamu za mwaka sababu M/Kiti alikua na kikao na Rais @SuluhuSamia baada ya kikao nimeridhika Rais anania njema na Taifa letu, natangaza 25 Jan, 2023 itakua J/tano nitarudi Tanzania kufanya kazi ya demokrasia na Rais Samia" - Tundu Lissu

Mwisho wa kunukuuu
Ujumbe mchungu sana kwa wale uvccm waliopitwa na wakati
 
Mh. Rais Samia hongera sana, naamini kila mtanzania aliye kimbilia nje ya nchi atarejea nyumbani na kuishi maisha yake kwa amani na furaha ya kweli huku wakiendelea na shughuli zao halali za kuwapatia kipato.

Ila tuweke wazi, tuipende nchi yetu kwa dhati, hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania, kuichafua nchi, kuisema vibaya serikali kwa matusi au lugha chafu chafu haisaidii chochote, kama ikiwa una hoja kubwa au umeona kuna ufisadi mkubwa au umeona kiongozi mkubwa wa serikali kakosea, kuna namna nzuri sana ya kuwakilisha hoja yako kwenye vyombo husika na ikafanyiwa kazi na matokeo bora tukaona.

Nchi yetu ikichafuka hata aliyeichafua nae anachafuka na niseme tu, tusijidanganye hata kidogo hakuna mzungu au beberu yeyote anaipenda nchi yetu kuliko sisi wenyewe, hivyo kuikashifu au kuisema vibaya nchi yako, labda utegemee msaada wa wazungu huko ni kupotoka.

Tanzania ni yetu sote na itajengwa na sisi watanzania wenyewe.
 
Duh! Propaganda za kitoto sana hizi mkuu, ushoga upo since hata Abraham hajawepo kwenye uso wa dunia! Wewe mwenyewe na kujimwambafy hapa unaweza kuwa shoga vile vile! Stupid
Kuwepo ushoga tangu enzi za Ibrahim si habari mpya; habari mpya ni watu kuhongwa € 50m kuja kuhamasisha ushoga.

Lipi gumu hapo kueleweka kwako?
 
Tarehe 21 itakuaje, au itaahirishwa.?

 
Back
Top Bottom