Natumaini amejiandaa vyema.
Kama ni ushauri: atulie, asibabaishwe na chochote; aonyeshe anao utulivu wa kuwa kiongozi wa nchi mwenye busara.
Ajue kwamba hapambani na Magufuli, Magufuli atpambana na rekodi yake mwenyewe na aliyokwishafanya au kutoyafanya ambayo yanafahamika vizuri na wananchi wote.
Aielewe vyema ajenda ya chama chake, na akubaliane na wenzake kwamba ajenda hiyo ni ajenda ya waTanzania wote; ni ajenda ya kulijenga taifa lenye heshima mbele ya mataifa mengine yote.
Kuna vitu vinatia shida sana huko CHADEMA, awe mwangalifu sana navyo. Sasa hivi sitavitaja.
Ni muhimu awaonyeshe waTanzania kwamba 'he is presidential material' na sio mtu wa kuropokaropoka tu kwa lolote linalomjia kichwani.
Mengine yote awaachie waTanzania, watayashughulikia kwa niaba yake. Yeye atatakiwa kuonyesha njia tu.