Usi generalise hii issue for no reason, Lissu amemzungumzia Magufuli specifically kwenye angle ya kulinda rasilimali za taifa, ndio amemsifia, lakini kama angegusa maeneo mengine, kama utawala bora na haki za binadamu, naamini story ingekuwa tofauti hapa, hata nawe ungekosa chakujitetea.
Tuliza munkari, just be specific.
Sasa Lissu yeye ndio miongoni mwa waliopotia mateso na Utawala wa Magufuli.
Anaona kuna afadhali ya Magufuli dhidi ya Samia katika Uongozi.
Hapo ulitakiwa ujipime tofauti yako wewe usie kubaliana na Lissu pia kabla ya kumpinga.
Hoja kubwa ya Lissu kua upande wa Magufuli katika hili ni Nchi hivyo Magufuli ana afadhali kubwa kuliko Samia.
Hawe alikua Dikteta au alipeleka Miradi kwa ubaguzi na mingine Mikubwa kwao au vyovyote lakini alitanguliza maslai ya Nchi mbele.
Kuna utofauti wa Lissu na Wanasiasa wengine pia na atakua ni Kiongozi wa aina yake kuwai kutokea.
Leo Lissu anatufunza kusamehe Mtu sio kwa maslai yake binafsi bali kwa maslai ya Nchi.
Lissu anaweka mateso ya kuuguza madonda aliyo pitia kipindi cha Magufuli Pembeni na anaungana naye kwa sababu ya kutetea Nchi.
Lissu anaweza kua anaumizwa na Atima ya waliotekwa na kupotezwa walio pata mateso na vilema lakini linapo kuja suhala la Nchi anatetea Nchi.
Hii ndio sifa ya Lissu mtafute katika kutafuta na kuchunguza Ukweli juu ya Atima ya wachimbaji wadogo wakaazi karibu na migodi ya Nyamongo na Buzwagi dhidi ya Makapuni ya Kigeni.
Alijitoa kwa dhati kutafuta Ukweli na aliweka Ukweli wazi.
Jambo lililo mpa heshima kubwa kwa jamii ya watu wa kanda ya ziwa na Watanzania.
Na ndio chimbuko lake la utetezi wa Rasilimali za Nchi na Nchi.
Hivyo katika maslai binafsi na ya wote Lissu atasimama katika maslai ya wote.
Katika hili jifunze kua Lissu anasema Nchi kwanza na hivyo Magufuli ana makosa.