Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais anasema hatutashitakiwa, kwa mwaka 2020 pekee makampuni matatu yametushitaki kwenye mahakama za kimataifa

Raja hayo makampuni spewed majibu. Au kaa kimya tafuta hoja nyingine
 
Umasikini, Mardhi na Ujinga bado vinatuandama kwa kasi ya ajabu.
 
Hizo ni kesi zilizochochewa na Lisu mwenyewe na Zito alafu anakuja kudai natishiwa kuuwawa.
Kauli hizi zinatolewa na wanao tudhibitishia kuwa wamebobea kwa ujinga.
Kwani Lissu na Zitto ni wamiliki wa hizo kampuni? Au viongozi wao?
 
Nadhani mjadala wa kushitakiana ilikuwa specific kwenye issue ya accasia na hata hivyo kushitakiwa hakuepukiki kwa Hali Kama hiyo ukizingatia kwamba tumewanyang'anya tonge.
 
Nani kakwambia Tundu Lissu anafurahia kuona Tanzania inanyanyasika??? Tundu siku zote alishauri the best approach Ila nyie mkamdharau na maneno ya kebehi . Leo yamewakuta mnamsingizia Lissu tena??? Dunia ya ubabe iliashapitaga huko. Saivi ni akili

Kitu anachosahau ni kuwa sio kiongozi wa kuchaguliwa popote pale. Anafurahia sana anaposikia Tanzania ina kesi fulani. Yeye ananeemeka na hizo kesi?
 

JokaKuu, do you think TL can make a good president? Ile jazba yake inaogopesha sana
 

Kesi gani? Take Acacia?
 
Domo kaya huyo hana jipya, mzushi na asiye na hoja. Watanzania wanataka kusikia namna ya kuboresha maisha yao, Serikali imefanya vema haoni cha kupotosha anaongelea vitu ambavyo hata hao wasikilizaji hawamwelewi
 

Ndio maana hawataki content ya vyombo vya habari vya nje iingie nchini!
 
JokaKuu, do you think TL can make a good president? Ile jazba yake inaogopesha sana

..he is not a violent person.

..pamoja na "jazba" zake umewahi kusikia amemdhuru mtu yeyote?

..ni mtu anayependa haki kwa wote, siyo kwake peke yake.

..pia ana msaada kwa wengine, kwa maana akisikia mtu anaonewa hawezi kukaa kimya.

..lakini la mwisho, hata akifanikiwa itakuwa ni kwa ushindi mwembamba, hiyo itakuwa ni BIMA/INSURANCE kwetu kwamba hatakuwa Raisi mwenye absolute powers.
 
Yeye alisema acacia walikuwa sahihi kufanya wanachokifanya na tulikuwa tunatafuta matatizo kuwazuia kusafirisha makinikia. sasa ikawaje acacia wakakubali kutoa hizo usd 300m?

..alichosema siyo sahihi ni zile ripoti.

..kwamba ripoti zile zisingeweza kusimama ktk mahakama yoyote ile.

..kuna tofauti kubwa sana kati ya madai ya usd 191 billion na malipo ya usd 300 million.

..ni sawasawa na umdai mtu usd 636 halafu yeye akubali kulipa usd 1.

..barrick waliona wanapata hasara kutokana na mgogoro ule na ndiyo maana wakaamua kutulaghai na usd 300 million.

..hata hivyo bado hawajamaliza kulipa zote ingawa waliahidi toka mwaka 2017.
 
Jiwe alifikiri kuficha inasaidia ?Huo ndio mwanzo siri zote zinaenda kutoka ,aliminya vyombo vya habari na kutunga sheria kandamizi ili kuficha haya ,sasa mficha maradhi ugonjwa humuumbua.
 
Kushitakiwa hizo ni sifa za ziada maana mh Lissu ndiye chaguo la watanzania woote kwa sasa.
Hv kwa nini mnatujumuisha watanzania wote as if tulikaa kikao tukakubaliana? Semea nafsi yako usitusemee hatujakutuma
 
Hiyo mikataba ya kinyonyaji ilipitishwa na serikali ya chama cha upinzani?

Mlitumia wingi wenu bungeni kupitisha miswaada ya hovyo huku mkipiga mayowe na vigeregere.

Leo hii mnajifanya eti mikataba ya kinyonyaji! Subirini iingie serikali nyingine ndiyo mtajua kuwa maharage ni mboga au kitafunwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…