Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais anasema hatutashitakiwa, kwa mwaka 2020 pekee makampuni matatu yametushitaki kwenye mahakama za kimataifa

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais anasema hatutashitakiwa, kwa mwaka 2020 pekee makampuni matatu yametushitaki kwenye mahakama za kimataifa

TL binafsi nilisikitika sana alipojeruhiwa. Ila sikubaliani Naye kabisa kwa jinsi anavyopenda kuona Tanzania inanyanyasika na kupata shida na mataifa ya nje. Yeye ananufaika na nini?
Nani kakwambia Tundu Lissu anafurahia kuona Tanzania inanyanyasika??? Tundu siku zote alishauri the best approach Ila nyie mkamdharau na maneno ya kebehi . Leo yamewakuta mnamsingizia Lissu tena??? Dunia ya ubabe iliashapitaga huko. Saivi ni akili
 
Hizo ni kesi zilizochochewa na Lisu mwenyewe na Zito alafu anakuja kudai natishiwa kuuwawa.

Kesi unaweza kuchochea vipi kama hufahamu sheria ni bora kunyamaza hivi wewe unaweza kuchochewa na mtu wakati hakuna hoja yoyote unayodai ukaenda mahakamani sababu ya kuchochewa na mtu na unafahamu ukishindwa unalipa gharama ya kesi
 
Akiwa mjini Kahama, mgombea urais wa Jamhuriya muungano ndugu Tundu Antipas Lissu amesema kuwa makampuni makubwa matatu kwa mwaka huu pekee yameishtaki Tanzania kwenye mahakama za kimataifa.

"Si walisema hatutashtakiwa? Oooh Lissu alisema tutashtakiwa...mbona sasa hatujashtakiwa? Niwaambieni, kwa mwaka huu pekee makampuni matatu yametushtaki kwenye mahakama za kimataifa" Amesema Lissu bila kubainisha haya makampuni.

My take: Kutokana na Rais kubana uhuru wa upatikanaji habari na kutokana na mambo ya ajabu tunayoelezwa na serikali huku mengine yakiwa waziwazi ya uongo, naamini alichosema Lissu.
Amini unachotaka kuamini! Lakini ni Bora x 1000000 Magufuli kuliko mhuni huyo unayejiaminisha kwake👇
 
Mkono Nimrod ameitetea tanesco sana mkuu

..Mkono alikwenda kutafuta mawakili huko nje wanaoweza kusimamia kesi hiyo.

..kwa kesi za ndani Tanesco walikuwa wakizipeleka kwa firm ya Nimrod Mkono ambaye ana mawakili waliosajiliwa Tz.

..kesi za nje zilikuwa zinapelekwa kwa Mkono, na yeye alikuwa akienda nje ktk nchi husika na kukodi mawakili.

..hata serikali inaposhitakiwa nje ya nchi, AG hukodisha mawakili ktk nchi/mahakama husika kusimamia kesi.
 
..burden of proof iko kwa serikali kuonyesha kwamba haishtakiwi.
Hapana, burden of proof ni kwa mtoa shutuma siyo mshutumiwaji. Msingi wa innocent until proven guilty inatokana na msingi huohuo.
 
..kaka hizi ni SIASA.

..ukishutumiwa ktk siasa unajibu tuhuma.

..usipojibu itaonekana umekubali hizo tuhuma.
Sawa kabisa. Magufuli anaweza kujibu tu kuwa "Mpuuzeni Lissu ni mwongo, hatujashitakiwa popote;" hiyo siyo proof ila ni response tu. Lissu ndiye anayetakiwa kutoa proof kuwa kweli tumeshitakiwa kwenye mahakama ABC chini ya kesi namba xyz kwa makosa kadha kadha kadha.

Elewa pi kuwa kushtakiwa siyo tatizo kabisa, tatizo ni pale unaposhindwa kwenye kesi. Hata yule kaburu alitushitaki Gauteng na Toronto, lakini hakuambulia kitu, akaamuliwa kutulipa.
 
Akiwa mjini Kahama, mgombea urais wa Jamhuriya muungano ndugu Tundu Antipas Lissu amesema kuwa makampuni makubwa matatu kwa mwaka huu pekee yameishtaki Tanzania kwenye mahakama za kimataifa...
Kwahiyo kakaa ulaya kuchochea kesi sio? Kwanini aje ndio tuanze kushitakiwa? Ila kawa na adabu safari hii hajayataja hayo makampuni wasije mdhuru tena
 
Sawa kabisa. Magufuli anaweza kujibu tu kuwa "Mpuuzeni Lissu ni mwongo, hatujashitakiwa popote;" hiyo siyo proof ila ni response tu. Lissu ndiye anayetakiwa kutoa proof kuwa kweli tumeshitakiwa kwenye mahakama ABC chini ya kesi namba xyz kwa makosa kadha kadha kadha...

Gauteng sawa lakini sidhani kama kuna mrejesho wa yaliyotokea Toronto. I stand to be corrected kwenye hilo la Toronto.

Amandla...
 
Gauteng sawa lakini sidhani kama kuna mrejesho wa yaliyotokea Toronto. I stand to be corrected kwenye hilo la Toronto.

Amandla...
Ile ya case ya Toronto ilikuwa dismissed kuwa haina grounds; ndiyo maana haikuchukua muda mrefu kama ile ya Geuteng
 
Sawa kabisa. Magufuli anaweza kujibu tu kuwa "Mpuuzeni Lissu ni mwongo, hatujashitakiwa popote;" hiyo siyo proof ila ni response tu. Lissu ndiye anayetakiwa kutoa proof kuwa kweli tumeshitakiwa kwenye mahakama ABC chini ya kesi namba xyz kwa makosa kadha kadha kadha.

Elewa pi kuwa kushtakiwa siyo tatizo kabisa, tatizo ni pale unaposhindwa kwenye kesi. Hata yule kaburu alitushitaki Gauteng na Toronto, lakini hakuambulia kitu, akaamuliwa kutulipa.
Hawezi kujibu kwamba apuuzwe! Kwa vigezo gani?
 
Hawezi kujibu kwamba apuuzwe! Kwa vigezo gani?
Hajaleta ushahidi; rejea ile notion ya burden of proof huko nyuma. Ukimtuhumu mtu yeyote, siyo jukumu lake kuprove kuwa shutuma zao ni za uwongo. Wewe unayetuhumu ndiwe unayetakiwa kuprove.

Mtuhumiwa atakaupinga tu bila kutoa ushahidi wowote, na maneno mepesi sana ni hayo ya kuwa mpuuzeni mtu huyu ana matatizo ya akili.
 
Sawa kabisa. Magufuli anaweza kujibu tu kuwa "Mpuuzeni Lissu ni mwongo, hatujashitakiwa popote;" hiyo siyo proof ila ni response tu. Lissu ndiye anayetakiwa kutoa proof kuwa kweli tumeshitakiwa kwenye mahakama ABC chini ya kesi namba xyz kwa makosa kadha kadha kadha.

Elewa pi kuwa kushtakiwa siyo tatizo kabisa, tatizo ni pale unaposhindwa kwenye kesi. Hata yule kaburu alitushitaki Gauteng na Toronto, lakini hakuambulia kitu, akaamuliwa kutulipa.

Kwanza, Tundu Lissu huwa habahatishi ktk mambo haya.

Nadhani unakumbuka alivyofichua kesi ya bombadier kukamatwa. serikali ilijaribu kukanusha na ikaishia kuaibika.

Pili, nakubaliana na wewe kwamba kushtakiwa siyo jambo baya. serikali isione aibu kushtakiwa.
 
..kwanza, TL huwa habahatishi ktk mambo haya.

..nadhani unakumbuka alivyofichua kesi ya bombadier kukamatwa. serikali ilijaribu kukanusha na ikaishia kuaibika.

..pili, nakubaliana na wewe kwamba kushtakiwa siyo jambo baya. serikali isione aibu kushtakiwa.
Hiyo bullet ya kwanza bado ni speculation na conjectural tu. Hiyo bullet ya pili ni matokeo ya halo effect ya bias; kwamba kwa vila zamani alipatia, hata kama ilikuwa ni kwa kubashia tu, basi atakuwa anapatia kila kitu.

Mambo haya yanataka proof. Inawezekana kuwa kwa vile anasemekana kushirikikiana na wanasheria wa wanaolinda maslahi ya Barrick, wakafungua kesi frivorolous amabazo baadaye zitatupiliwa mbali na mahakama kuonyesha tu kuwa kweli kulikuwa na kesi.

Inabidi kesi anazotaja ziwe zimefunguliwa mwaka huu, siyo mwezi huu.
 
Back
Top Bottom