Tundu Lissu: Rais Samia ameuza bandari zetu zote zilizopo na zitakazokuwepo

Tundu Lissu: Rais Samia ameuza bandari zetu zote zilizopo na zitakazokuwepo

Tunahitaji tuwe wananchi au raia tunaojielewa, tunaoweza kupambana katika dunia ya sasa kuliko kuwategemea viongozi tu na kuwatupia lawama.
Najua kuna watu wanasema madaraka yote yapo kwa Rais kwa mujibu wa katiba, Hiyo ni kweli, lakini haimaanishi tusubirie kupata matatizo au kifo kama wanyama wanaochinywa au kuliwa. Lazima tufanye vitendo vya kuwalaumu na kuwashughulikia wale wataalamu au wasaidizi wa Rais wanaosababisha hali hii.
Mara nyingi, watu waovu, wapuuzi, wazembe na wajinga wametumia mwavuli wa Rais au collective responsibility serikalini kusababisha matatizo kwa raia na hasara kwa taifa kwa ujumla.
Kila mwananchi apambane na kuunganisha nguvu kwenye nafasi yake dhidi ya unyonyaji wa kimataifa na madalali wao walio ndani.
 
Sijui kama kuna jambo ambalo Lissu amewahi kulipinga au kuliongelea halafu muda usije kuwa upande wake.
Vipi Air tanzania si alipinga kuanzishwa kwake? Au umesahau? Vipi Urais si aligombea kama mpinzani?

Hajawahi kumpinga Mbowe?

Vipi risasi au hizo alitaka zimtwange?
 
Hilo siyo tatizo kabisa, unafikiri hata mwendazake alikuwa anaelewa?

Si ndiyo maana wapo makatibu wakuu na wasaidizi kibao wa mambo ya sheria Ikulu. Au wote ni maboya?
Unafikiri mwendazake alikuwa mjinga!?
alikuwa anasoma na kufanya kazi hadi usiku wa manane
 
Hii serikali imekuwa kama Mafia Cartel, kuna kitu kita Yield somewhere, ni suala la muda tu. Huwezi kuliliwa na watu milioni 60 wanaokuomba usiwauze utumwani halafu wewe useme umeziba Masikio
 
Back
Top Bottom