Ndiyo, hauwezi kuniambia niipuuze katiba ya nchi iliyo zao la mchakato wa waasisi wa taifa hili waliojitoa mhanga kwa jasho na damu kuitengeneza Tanzania, kwa maneno ya mtu mmoja tu mwenye kelele za ulalamishi. Waasisi wetu si tu kwamba walikuwa na akili tu, pia walikuwa na maono, na uthubutu, walijitesa, wakajitoa mhanga, wakajinyima, wakatupatia nchi hii na katiba yetu.
Kama Nyerere alionyesha concern kuhusu madaraka ya Rais, yeah! it was just a concern. Hakusema katiba ni mbaya au Rais hawezi kutumia madaraka yale kwa manufaa na maslahi mapana ya nchi.
Nimchukulie serious Lissu kwa kipi, kwa mfano? Kelele za ulalamishi?