Tundu Lissu: Sabaya siyo mkosaji wa kisiasa ni jambazi

Tundu Lissu: Sabaya siyo mkosaji wa kisiasa ni jambazi

Anawashwa huyu mzee. Hizi siasa huwa zinawatoa akili kabisa. Anachokifanya yeye ni kuwashambulia wenzie kama ambavyo ye alishambuliwa. Tofauti ye anashambulia kwa maneno wakati yeye alishambuliwa kwa silaha.
Sukuma Gang nyie ni wapumbavu sana,kumtetea jambazi sugu Sabaya lazima ujizime data kwanza.
 
Wewe ndio mjinga, ungewauliza hao wauliza maswali kwa nini hayo wanayouliza?
Yeye anajibu maswali mliyokuja nayo, hapangi maswali
Hawa watu hawana akili kabisa sijui kwanini. Utadhani TAL alienda kutoa hotuba Radioni kumbe aliitwa kwenye interview na Kuna maswali yanayoulizwa, asingeyajibu wangesema Ni jeuri!
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu alihojiwa na Dar 24 Media siku chache zilizopia. Akiwa katika mahojiano hayo Lissu amezungumza masuala mengi yanayohusu mwenendo wa kisiasa nchini.

Aidha alipoulizwa kuhusu kumchukulia Mkuu wa Wilaya wa zamani wa Hai, Lengai Ole Sabaya kama Mkosaji wa kisiasa, Tundu Lissu alipinga kwa kueleza kuwa kiongozi huyo hafai kuchukuliwa kama Mfungwa wa kisiasa, asema kiongozi huyo ni jambazi. Katika hilo Lissu amesema:

View attachment 2510359

Mwandishi: Ukimtazama Sabaya anastahiki kuachiwa kama mkosaji wa kisiasa.

Lissu: Sabaya sio mkosaji wa kisiasa, Sabaya ni jambazi.

Mwandishi: Unahukumu Tundu

Lissu: Amehukumiwa! Ni mimi ndiyo nimemhukumu? Amehukumiwa kwa Ujambazi wa kutumia silaha. Na ambayo tunayafahamu sisi aliyoyafanya. Angeshtakiwa kwa yote ambayo tunayafahamu angekaa gerezani maisha yake yote.

Mwandishi: Lakini alikuwa anafanya kwa utashi wa kisiasa!

Lissu: Sio kwa utashi wa kisiasa, hakuna utashi wa kisiasa kwa kufanya makosa ya jinai. Wakwetu amesingiziwa, Sabaya hajasingiziwa. Shida yangu mimi na serikali ya Samia ni hii, kina Sabaya wapo wengi ajabu.

Mwandishi: Wapo uraiani?

LIssu: Ndiyo wapo Uraiani.

Mwandishi: Kama nani?

Lissu: Mfano: Paul Makonda anatakiwa ashughulikiwe. Makosa mengine ameyafanya waziwazi kabisa. Amenyang'anya watu magari, nyumba. Amevamia Clouds.

Mwandishi: Una Ushahidi?

Lissu: Upo! Umeonekana. Nakwambia kuna kina Sabaya wengi sana. Watu waliokuwa wanawanyang'anya watu mali na kuwafungulia makosa ya uongo haya. Kina DPP Mganga Biswalo leo jaji. Namsikia Mama juzi anasema wanawanyang'anya watu hela wanazipeleka China. Wote hawa walifanya makosa ya jinai wanapaswa kushughulikiwa kijinai. Lakini anachukuliwa Sabaya anakaangwa peke yake. That's my only regret. Na hiyo inaleta taswira kwamba pengine labda kuna sababu zingine zingine.

Mwandishi: Kwa nani?

Lissu: Kwa Sabaya, lakini the fact kwamba anang'ang'aniwa peke yake wakati waliotenda makosa kama haya

Akina Sabaya waliobaki uraiani kama Paul Makonda washughulikiwe!
Mpuuzi shoga huyu. Sabaya kwake lazima atakua adui. Eti jambazi sasa mbona mahakama kawashinda wamemshikilia kutafuna njia mpya kumuangamiza.
 
Mpuuzi shoga huyu. Sabaya kwake lazima atakua adui. Eti jambazi sasa mbona mahakama kawashinda wamemshikilia kutafuna njia mpya kumuangamiza.
Bro Kama hii ndio njia sahihi ya kujibu hoja na kumtetea General Sabaya! Hata watawala ambao upo upande wao wanakushangaa!
 
Mpuuzi shoga huyu. Sabaya kwake lazima atakua adui. Eti jambazi sasa mbona mahakama kawashinda wamemshikilia kutafuna njia mpya kumuangamiza.
Wewe bwege ukitaka kumtetea mtu jaribu kupata facts zote ili uweze kujenga hoja zako kiweledi. Huyu bwana wako jambazi sugu Sabaya yupo lupango kwa kesi nyingine ya uhujumu uchumi ambayo haina dhamana siyo ile aliyofungwa miaka 30 kisha akashinda rufaa . Kwa taarifa yako hata hiyo aliyoshinda rufaa Dola imekata rufaa mahakama ya Rufaa kwa hiyo yuko rumande kihalali kabisa na bado zipo kesi nyingine Takukuru ziko kwenye hatu za mwisho za upelelezi ili zifikishwe Mahakamani. Wewe kama vipi tafuta bwana mwingine uolewe tu kumsubri huyo utazeekea kwa wazazi wako.
 
Sasa ushahidi si ulishapelekwa mahakamani hadi video za CCTV zipo.

Wewe una akili kweli?
Huyo jamaa ni punguani sana mimi huwa namuonea huruma mama yake kwa kumuweka tumboni miezi 9 bila kufanya abortion na kutuletea kiumbe cha hovyo...
 
"Lengai Ole Sabaya sio mkosaji wa kisiasa, Sabaya ni jambazi, na amehukumiwa kwa ujambazi.

Angeshtakiwa kwa yote ambayo aliyoyafanya na ambayo tunayafahamu angekaa gerezani maisha yake yote" TunduALissu,
Screenshot_20230408-132140.jpg

 
Back
Top Bottom