Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Sijapokea wito kutoka Tume ya Uchaguzi. Sitarajii kuacha Kampeni kwa kuitikia wito kutoka mitandaoni

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Sijapokea wito kutoka Tume ya Uchaguzi. Sitarajii kuacha Kampeni kwa kuitikia wito kutoka mitandaoni

Spana za Lissu zimewabana wanahaha kwa kila namna. Chakubanga kila uchwao anajitutumua kufanya press kupunguza moto maana kuuzima hawawezi ila kaangukia pua watu hatuelewi!

Hivi kwanini Lissu hakugombea yeye 2015 jamani? Sasa hivi ndio naamini, yalikuwa makosa sana kimkakati kumpa nafasi ya kugombea bwana yule. Huyu ndiye mpinzani sasa, huyu ndiye anayepaswa kupewa kura zetu za Urais.
 
Mgombea wa CCM anapotumia lugha ya kikabila hadharani kipindi hiki cha kampeni, anapotoa hongo kwa wapigakura kwa kulazimisha barabara zianze kujengwa ktk eneo husika nje ya bajeti, anapotumia lugha za vitisho kwa wapiga kura wasichague upinzani, achilia mbali "mungu hoyeee" bado vikaragosi wake wa tume hawayaoni hayo.
Hivi kweli jamaa anasemaga "Mungu oyee" au wanamuwekea maneno mdomoni? [emoji3]
 
Atapelekewa Leo asbh hii, kabla hajaanza kampeni zake kwani tarehe 29.09. Si bado au imepita ? .vijana wamelipwa Per diem ya siku 10, na ontrasit na food and refreshment ili kumpelekea hyo surmons mkononi. Kufanya kazi tume raha sana, mgombea yupo arusha unamfuata mwanza
Na sisi tutanatak aende akawape shule
 
Huyo mzee ambae hata kuongea hawezi, maneno yanashindwa kutoka mdomoni, inaonekana hata kiswahili hajui vizuri ndio wakumuhoji Lissu?.
Atawekewa hiyo clip yake na atapigwa maswali kutoka kwenye hiyo clip hadi atachangamyikiwa 😂😂😂.
Ajiulizi Kwa nini kina Jaji Kaijage na Mbarouk wamejiweka nyuma???😂😂😂
 
Hata Membe mlikuwa mnamwambia hivi hivi,

Leo yupo analia pekeake
Kwani Lissu ni Membe? Humjui Lissu wewe.

Kikwete wenu alisema ni bora slaa awe Raisi kuliko Lissu kuwa Mbunge 😂😂😂

Chukueni ushauri wa mtumishi Mwingira tu, Lissu ni Mshindi hamuwezi kupambana nae!! Kama risasi zenu 16 zilishindwa kummaliza Mungu akamtetea, kipi kitamrudisha nyuma?

Mungu kashawakataa Ccm mkizidi kushupaza shingo ndo atawapa pigo kuu hadi mtaumia 😂😂😂
 
Lissu yupo sahihi na anatufundisha masuala mengi.
sana, kua lazima mambo yaende kisayansi, huwezi kuitwa kipuuzi tu uende nipe official letter nije na sio unaniita mitandaoni halafu ghafla unaanza kunifundisha kunadi sera na kipi cha kusema na kuwapangia watanzania cha kufanya, watanzania sio mamburula , japo wapo mamburula wachache wanaotetea mambo haya ya kijinga.
 
CCM imekaa muda mrefu madarakani hadi imesahau kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo.
 
Back
Top Bottom