Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Sijapokea wito kutoka Tume ya Uchaguzi. Sitarajii kuacha Kampeni kwa kuitikia wito kutoka mitandaoni

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Sijapokea wito kutoka Tume ya Uchaguzi. Sitarajii kuacha Kampeni kwa kuitikia wito kutoka mitandaoni

Spana za Lissu zimewabana wanahaha kwa kila namna. Chakubanga kila uchwao anajitutumua kufanya press kupunguza moto maana kuuzima hawawezi ila kaangukia pua watu hatuelewi!

Hivi kwanini Lissu hakugombea yeye 2015 jamani? Sasa hivi ndio naamini, yalikuwa makosa sana kimkakati kumpa nafasi ya kugombea bwana yule. Huyu ndiye mpinzani sasa, huyu ndiye anayepaswa kupewa kura zetu za Urais.
Awamu hii ndio nzuri zaidi manake Lissu amerudi toka kuzimu.
 
Lissu anatapatapa barua itamfikia Kama ni mwanaume akatae kwenda aone kama hataondolewa kwenye orodha ya wagombea.
Lissu amesema hawezi kwenda kwa habari za mitandaoni akipewa wito rasmi kwa barua atakwenda, hata tofauti hii huijui!
 
Mheshimiwa Lissu wamemis semina yako"usikatae nenda ukawapige semina ya uchaguzi kabla ya October 28.ili utengeneze njia kwa tume zjazo "..wanashindwa kutumia njia ya kuomba ila wanahamu na madini yako!!
Asiende watamuwekea sumu kwenye viti
 
Lissu yupo sahihi na anatufundisha masuala mengi.
Tatizo nyie wa CCM hamfundishiki kwa sababu akili yenu ni ndogo sana mmekuwa tuned kumsikiliza mropokaji mwenzenu kutoka Chato ambaye miaka 5 ameshindikana kufundishika lugha muhimu kwake ambayo ni nyepesi mno hata chekechea wanaimudu muda mfupi tu wakianza darasa. Kuna Watanzania wengi sana walikwenda kusoma Vyuo Vikuu nchi za nje zinazofundisha kwa lugha zao lakini Wabongo wale wanajifunza lugha miezi 6 tu wanaanza masomo ya Chuo Kikuu na wanafunzi wenyeji.

Kumaliza Vyuo wanafunzi wa Bongo wanaandika Thesis za Degree zao kwa lugha za wenyeji na kutathiminiwa pamoja na za wanafunzi wenyeji na kupitishwa na kugawanywa nakala kama kawaida ya Vyuo husika. Mgombea Urais na PhD yake inayokuwa midomoni mwa wateuliwa wake kila wakitaja jina lake na Mwalimu by profession hata lugha yetu adhimu inampiga chenga! PhD haisemwi ni ya Chuo gani.
 
Tume lazima iiratibu kampen za wagombea kama ni za kuleta taharuki zistopishwe mara moja.
 
Kuna uzi mmoja unazungumzia tamasha la wasanii Iringa,unaenda taratibu sana##octoba tuna Jambo letu##
 
Uchaguzi wa mwaka huu mbali ya wagombea kusaka ushindi lakini pia tunapata darasa la mambo mbalimbali.

Tundu Lisu anasema hadi sasa hajapokea tuhuma zozote kutoka Tume ya uchaguzi wala mgombea yoyote au chama chochote cha siasa.
NEC kama wana tuhuma dhidi yangu (Lissu) basi wanapaswa kuzileta kimaandishi nami nitakuwa na saa 48 za kujibu kimaandishi kwa mujibu wa kanuni, amemalizia Lissu.

Source Dar Mpya tv

Maendeleo hayana vyama!
 
Sheria ndo inataka hivyo, chama kinalalamika kwa tume, chama knacholalamikiwa kinajibu kwa niaba ya mgombea. Mgombea anaendelea na kampeni zake maana aliyemdhamini mgombea ni chama.

Sijui kama NEC ina wanasheria, au mwanasheria wao ni Polepole
 
Akiwa mjini Nyamongo mgombea kiti cha urais kupitia cdm mh Lissu amesema kuwa hana mpango wa kwenda Dodoma kesho.

NEC wamemtaka mh Lissu kesho kwenda dodoma kujieleza mbele ya tume juu ya matamshi ya mh Lissu.

Tazama ujumbe wa mh Lissu aliyo wapatia watanzania juu ya wito huo wa NEC.

Screenshot_20200928-201034.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akiwa mjini Nyamongo mgombea kiti cha urais kupitia cdm mh Lissu amesema kuwa hana mpango wa kwenda Dodoma kesho.

NEC wamemtaka mh Lissu kesho kwenda dodoma kujieleza mbele ya tume juu ya matamshi ya mh Lissu.

Tazama ujumbe wa mh Lissu aliyo wapatia watanzania juu ya wito huo wa NEC. View attachment 1583753

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuh! Huyu genius Lisu ataisumbua Sana hii tume
 
Back
Top Bottom