Tundu Lissu: Tumeuzwa na Rais Samia. Mkataba wa DP WORLD na Serikali ni Mkataba wa ovyo

Wabunge wetu hawa hawa. ndo wawe na weledi wa kusoma na kuichambua mikataba? Musiwaonee jamani wapo pale kwaajili ya kusema ndioooo . Wanailinda serikali yao. Kikubwa posho zao na maslahi yea yapo.
Mkuu acha kuwashushia heshma waheshimiwa wetu. Hakuna bunge lenye wabunge wazalendo kama lakwetu. Si umeona namna mhe. Mdee alivyopambana kwa hoja za kisheria na spika Tulia Ackson Mwansasu? Bunge liko vizuri ndo maana limeridhia kitu chenye maslahi na taifa mkuu.
 
Bunge limemaliza kila kitu haya mengine ni maongezi ya kwenye kanga. Hayana tena mantiki.
 
Hahahaha. Kweli umenena yakufaayo kuitwa mkuu. Hayo yooote yanakufaa sana. Lkn bunge limefanya jambo saaafi kabisa tusubiri maendeleo ya chap chap.
Labda una ndugu yako alikuwa akikwapua mapesa Bandarini na akikugawia ndo maana una wasiwasi kuwa akiingia mwekezaji room ya rushwa itapungua kwa kuwa atakuwa makini ili mtaji wake usipitee. Bunge hoyeeeeee! Musukama na wenzake hoyeeeeee!. Dkt Tulia Safiiiiiiii.
Inabidi sasa Jimbo la Mbeya mwaka 2025 apewe Tulia iwe isiwe. Maana anaendesha bunge vyema na kwa maslahi ya taifa kabisa.
 
Hana lolote huyo. Mlopokaji tu.
 
Subiri watetezi wa serikali uchwara waje kumsuta
 
Learned brother Lissu ana msimamo gani jinsi Bandari yetu ilivyouzwa kwa Waarabu? Lissu amekuwa mpole sana sio kawaida yake.

​

Ukosoaji wa Lissu umebase kwenye lugha kali ili kufukisha ujumbe in a hard way. This time Lissu amepewa nini na mamlaka? Yupo kama hayupo, anakosoa kwa kusita sita.

Ikumbukwe inshu ndogo tu katika uongozi wa Magufuli, Lissu alikuwa anaitisha press kila siku na kutumia lugha ngumu. Ila awamu hii amekuwa mpole sana kwa utawala uliopo.

Lissu tunakutegemea brother, kuuzwa bandari ni aibu ya karne ambayo haijawahi kutokea duniani.

Umepatwa na nini Lissu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…