Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu siku ya leo Jumatano Februari 12, 2025. anazungumza na wanahabari Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dar es Salaam
Endelea kufuatilia uzi huu hapa Jamiiforums kupata updates kuhusu hotuba hii
"Katika miaka hii 67 ya kufanya uchaguzi, mifumo yetu ya uchaguzi imepitia mabadiliko mengi sana, sheria zetu za uchaguzi zimefanyiwa marekebisho zimetungwa upya, katiba zetu zimebadilishwa , kwa kiasi kikubwa katika hii miaka 67 tumejifunza mengi, leo tunapozungumza tunategemea nini hasa?
Ninazungumzia uchaguzi wa mitaa na vijiji wa mwaka 2019, Uchaguzi Mkuu wa Marais, madiwani na wabunge wa mwaka 2020 na uchaguzi wa mitaa na vijiji uliofanyika Novemba 2024. Chaguzi hizi tatu zinatupa sababu ya kujiuliza uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakuaje?"
"Jambo la kwanza kabisa ni kwamba mfumo wetu wa uchaguzi ni mfumo unaodhibitiwa na Rais wa nchi yetu, ni mfumo unaodhibitiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa upande wa Zanzibar ni mfumo unaodhibitiwa na Rais wa Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiye anayeteua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mkurugenzi wa uchaguzi na wajumbe wote wa tume ya uchaguzi, anawateua bila kulazimika kushauriana na mtu yeyote yule, na wote hawa anaowateua wanafanya kazi kwa mapenzi ya Rais, anaweza kuwaondoa wajumbe wa tume kwasababu yoyote ile"
Kuna kura zaidi ya milioni 2.1 ambazo hazijulikani zilitokea wapi, na asilimia 92 ya kura hizo zilipelekwa kwa wabunge wa CCM, sisi CHADEMA tumegawiwa hizo kura haramu 148000 lakini kura zaidi ya milioni 2 zilipelekwa kwa CCM, kura haramu kabisa.
Sasa haya yanawezekana kwasababu tume haiwajibiki kueleza mtu yeyote idadi halisi ya wapigakura iliyowaandikisha, tume haiwajibiki kufungua server zake huko wanapohifadhi takwimu za wapiga kura kwa mtu yeyote.
Na kwasababu haiwajibiki kufungua server zake kuonesha hizo takwimu, Tume imekuwa pamoja na serikali na CCM wanatumia mianya hiyo kuingiza mamilioni ya kura feki katika kila uchaguzi, sasa kura feki ni jambo la kawaida"

- Tundu Lissu anasema rafu zilizotokea kwenye chaguzi za 2019, 2020, na 2024 zinatoa picha za mwelekeo wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
"Katika miaka hii 67 ya kufanya uchaguzi, mifumo yetu ya uchaguzi imepitia mabadiliko mengi sana, sheria zetu za uchaguzi zimefanyiwa marekebisho zimetungwa upya, katiba zetu zimebadilishwa , kwa kiasi kikubwa katika hii miaka 67 tumejifunza mengi, leo tunapozungumza tunategemea nini hasa?
Ninazungumzia uchaguzi wa mitaa na vijiji wa mwaka 2019, Uchaguzi Mkuu wa Marais, madiwani na wabunge wa mwaka 2020 na uchaguzi wa mitaa na vijiji uliofanyika Novemba 2024. Chaguzi hizi tatu zinatupa sababu ya kujiuliza uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakuaje?"
- Lissu pia amesema kwamba Uchaguzi wa Tanzania unadhibitiwa na Rais na kwamba Rais ana mamlaka makubwa sana juu ya Uchaguzi
"Jambo la kwanza kabisa ni kwamba mfumo wetu wa uchaguzi ni mfumo unaodhibitiwa na Rais wa nchi yetu, ni mfumo unaodhibitiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa upande wa Zanzibar ni mfumo unaodhibitiwa na Rais wa Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiye anayeteua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mkurugenzi wa uchaguzi na wajumbe wote wa tume ya uchaguzi, anawateua bila kulazimika kushauriana na mtu yeyote yule, na wote hawa anaowateua wanafanya kazi kwa mapenzi ya Rais, anaweza kuwaondoa wajumbe wa tume kwasababu yoyote ile"
- Lissu pia aligusia uwepo wa kura feki kwenye Uchaguzi wa mwaka 2020