Pre GE2025 Tundu Lissu: Tuungane na ACT ili iweje? Tukishirikiana na vyama vingine kwenye Uchaguzi, tunaenda kuliwa vichwa

Pre GE2025 Tundu Lissu: Tuungane na ACT ili iweje? Tukishirikiana na vyama vingine kwenye Uchaguzi, tunaenda kuliwa vichwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii ndiyo waingereza huiita "Panic attack" 😀😃😆
kwa hiyo hapo amepanic right?

naona anafuta mdomo tu na kuangalia pembeni kama maji yapo au hayapo,

maandalizi ya press conference nyingine bana dah ni shida tupu:pedroP:
 
Wewe huwezi kujua athari zake kwa kuwa siye uliyekusudiwa. Kina Wassira ndiyo wanajua athari ya anachokisema Lissu.
anazungumzia atapataje wabunge wa viti maalumu huku :pedroP:

viti vingine haiwezekani dah, hesabu imegoma:pedroP:
 
Una haraka sana mpiga chabo... Wenye gemu lao wanajua nini wanafanya😆
apewe maji ya kunywa basi jamani mpaka aombe?

kuna na huruma basi kwa wasaidizi wake?

wakamchukulie maji yake kwenye gari analo chupa kubwa la maji :pedroP:
 
Kweli hakuna tatizo kwenye chaguzi za "Tanazania", ila kuna tatizo kubwa sana kwenye chaguzi za Tanzania.
kwa ukurupukaji na papara za huyu kiongozi,

bilashaka yoyote wagombea udiwani na ubunge wa chama hicho watenguliwa tu tena zaidi hata ya uchaguzi wa serikali za mitaa, kwasababu wanachochewa kugombea uongozi ni watu midomo na makelele tu badala ya kuzingatia sifa na vigezo vya kisheria na kikatiba vilivyopo.

Rais ataendelea kuwateu makamishna wa tume huru ya uchaguzi kwa mujibu wa sheria.
na watumishi wa uma wa ngazi yoyote huko wilayani na mikoani na kwenye kata wataendelea kusimamia uchaguzi bila mbambamba ya chama chocho cha siasa,

uchaguzi huru, haki na wa wazi nchini, ngazia ya udiwani, ubunge na urais utafanyika kwa salama na amani mapema oct.2025. hakuna haji kubaika na makelele ya vibaraka wa mabwenyenye ya magharibi.

hakuna tatizo hata moja kwenye uchaguzi wa Tanazania,
watakao leta fujo watadhibitiwa vilivyo bila kuchelewa.

ni muhimu sana kila mtanazia kufahamu na kuzingatia hili :MODS:
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu siku ya leo Jumatano Februari 12, 2025. anazungumza na wanahabari Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dar es Salaam

Endelea kufuatilia uzi huu hapa Jamiiforums kupata updates kuhusu hotuba hii

  • Tundu Lissu anasema rafu zilizotokea kwenye chaguzi za 2019, 2020, na 2024 zinatoa picha za mwelekeo wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.​

"Katika miaka hii 67 ya kufanya uchaguzi, mifumo yetu ya uchaguzi imepitia mabadiliko mengi sana, sheria zetu za uchaguzi zimefanyiwa marekebisho zimetungwa upya, katiba zetu zimebadilishwa , kwa kiasi kikubwa katika hii miaka 67 tumejifunza mengi, leo tunapozungumza tunategemea nini hasa?

Ninazungumzia uchaguzi wa mitaa na vijiji wa mwaka 2019, Uchaguzi Mkuu wa Marais, madiwani na wabunge wa mwaka 2020 na uchaguzi wa mitaa na vijiji uliofanyika Novemba 2024. Chaguzi hizi tatu zinatupa sababu ya kujiuliza uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakuaje?"

  • Lissu pia amesema kwamba Uchaguzi wa Tanzania unadhibitiwa na Rais na kwamba Rais ana mamlaka makubwa sana juu ya Uchaguzi

"Jambo la kwanza kabisa ni kwamba mfumo wetu wa uchaguzi ni mfumo unaodhibitiwa na Rais wa nchi yetu, ni mfumo unaodhibitiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa upande wa Zanzibar ni mfumo unaodhibitiwa na Rais wa Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiye anayeteua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mkurugenzi wa uchaguzi na wajumbe wote wa tume ya uchaguzi, anawateua bila kulazimika kushauriana na mtu yeyote yule, na wote hawa anaowateua wanafanya kazi kwa mapenzi ya Rais, anaweza kuwaondoa wajumbe wa tume kwasababu yoyote ile"

acha upotoshaji ndugu mvaa bullet proof vest,

nani anasifia uchaguzi wa kenya kua ni huru na wa haki kama sio muendelezo wa upotoshaji wako? :BASED:
 
Kweli hakuna tatizo kwenye chaguzi za "Tanazania", ila kuna tatizo kubwa sana kwenye chaguzi za Tanzania.
hakuna paragraph, nukta wala koma kwenye sheria au katiba ya Tanzania itabadilishwa kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania oct.2025.

Na uchaguzi utafanyika kwa mujibu wa sheria kwa amani na salama,
na chama chenye sera nzuri na viongozi makini kitapewa dhaman ya kushika dola na kuongoza nchi kupitia sanduku la kura,

hakuna haja ya makelele wala mdomo :NoGodNo:
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Tundu Lissu siku ya leo Jumatano Februari 12, 2025. anazungumza na wanahabari Makao Makuu ya chama hicho mkoani Dar es Salaam

Endelea kufuatilia uzi huu hapa Jamiiforums kupata updates kuhusu hotuba hii

  • Tundu Lissu anasema rafu zilizotokea kwenye chaguzi za 2019, 2020, na 2024 zinatoa picha za mwelekeo wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.​

"Katika miaka hii 67 ya kufanya uchaguzi, mifumo yetu ya uchaguzi imepitia mabadiliko mengi sana, sheria zetu za uchaguzi zimefanyiwa marekebisho zimetungwa upya, katiba zetu zimebadilishwa , kwa kiasi kikubwa katika hii miaka 67 tumejifunza mengi, leo tunapozungumza tunategemea nini hasa?

Ninazungumzia uchaguzi wa mitaa na vijiji wa mwaka 2019, Uchaguzi Mkuu wa Marais, madiwani na wabunge wa mwaka 2020 na uchaguzi wa mitaa na vijiji uliofanyika Novemba 2024. Chaguzi hizi tatu zinatupa sababu ya kujiuliza uchaguzi mkuu wa mwaka huu utakuaje?"

  • Lissu pia amesema kwamba Uchaguzi wa Tanzania unadhibitiwa na Rais na kwamba Rais ana mamlaka makubwa sana juu ya Uchaguzi

"Jambo la kwanza kabisa ni kwamba mfumo wetu wa uchaguzi ni mfumo unaodhibitiwa na Rais wa nchi yetu, ni mfumo unaodhibitiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa upande wa Zanzibar ni mfumo unaodhibitiwa na Rais wa Zanzibar.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ndiye anayeteua Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Mkurugenzi wa uchaguzi na wajumbe wote wa tume ya uchaguzi, anawateua bila kulazimika kushauriana na mtu yeyote yule, na wote hawa anaowateua wanafanya kazi kwa mapenzi ya Rais, anaweza kuwaondoa wajumbe wa tume kwasababu yoyote ile"

  • Lissu pia aligusia uwepo wa kura feki kwenye Uchaguzi wa mwaka 2020
"Wapiga kura waliopiga kura halali za wabunge kwa mujibu wa taarifa ya tume ya uchaguzi walikuwa takribani milioni 11. 8 lakini ukienda kwenye matokeo ya uchaguzi ya kila jimbo katika nchi yetu, ambayo tume iliyachapisha tarehe 5 Januari 2021 ukajumlisha matokeo ya kura halali katika majimbo yote ya nchi hii unagundua kwamba wapigakura halali waliopiga kura za wabunge katika uchaguzi mkuu uliopita ni takribani milioni 8.8

Kuna kura zaidi ya milioni 2.1 ambazo hazijulikani zilitokea wapi, na asilimia 92 ya kura hizo zilipelekwa kwa wabunge wa CCM, sisi CHADEMA tumegawiwa hizo kura haramu 148000 lakini kura zaidi ya milioni 2 zilipelekwa kwa CCM, kura haramu kabisa.

Sasa haya yanawezekana kwasababu tume haiwajibiki kueleza mtu yeyote idadi halisi ya wapigakura iliyowaandikisha, tume haiwajibiki kufungua server zake huko wanapohifadhi takwimu za wapiga kura kwa mtu yeyote.

Na kwasababu haiwajibiki kufungua server zake kuonesha hizo takwimu, Tume imekuwa pamoja na serikali na CCM wanatumia mianya hiyo kuingiza mamilioni ya kura feki katika kila uchaguzi, sasa kura feki ni jambo la kawaida"

anaomba hela tena :pedroP:
 
Back
Top Bottom