Kosa lilianza hapa:-
1. Kumkaribisha Lowasa na kumpa nafasi ya kugombea urais, ili hali Dr. Slaa alikuwa kishaandaliwa.
Ikaonekana chama hakiheshimu hustle za wanachama wake bali hela.
2. Viongozi kushiriki maridhiano bila ya kuruhusiwa na vikao vya chama toka ngazi ya chini ya chama .
Ikaonekana kuwa kumbe chama ni cha viongozi tu.
3. Kutoa matamko yasiyosimamiwa. Mfano huko nyuma chadema ilosema haitashiriki uchaguzi bila kuwa na tume huru. Mara ghalfa chama kikabadili gia angani.
Hoja ya msingi uliyoitoa hapa ni umuhimu wamaamuzi makubwa ya chama kuhusisha chama kizima, yàani wanachama wote kupitia uwakilishi wa viongozi wote wa ngazi zote.
Chama kubadilisha uamuzi si jambo la ajabu na siyo jambo baya, lakini maamuzi ya kufanya mabadiliko ni muhimu kuhusisha wanachama wote kupitia wawakilishi wao.
Nakubaliana nawe kwa 100%, yale maamuzi ya Mwenyekiti wa CHADEMA pekee yake kuamua kufanya maridhiano na mwenyekiti wa CCM, lilikuwa kosa kubwa la kiufundi. Na kulikuwa na kelele nyingi ndani ya chama kupinga kilichokuwa kinaendelea. Lakini bahati mbaya mwenyekiti hakutaka kuzisikiliza sauti za wanachama. Mwenyekiti yeye alikasirishwa tu na ile kauli kuwa amelambishwa asali. Alirakiwa apuuze kauli za kipuuzi kama zile, yeye angezingatia hoja tu za wale waliotaka mchakato na majadiliano juu ya maridhiano, uboreshwe na kufanyiwa marekebisho kuliko ulivyokuwa ukienda.
Kama maridhiano yangehusisha chama kizima, lazima kungekuwa na agenda za kujadiliwa, kungekuwa na timetable ya majadiliano na timetable ya utekelezaji. Na umma ungejua kwa uhakika ni nani amekwamisha marudhiano. Lakini kwa kuwa kila kitu kilifanyika mafichoni, hata kunapokosekana utekelezaji, umma unabakia kuwa mtazamaji. Labda mazingira yale ambayo mwenyekiti alipitia, nayo yalichangia sana:
1. Mwenye alitekwa Mwanza na kusafirishwa mpaka Dar, wanachama kimya!!
Mwenyekiti aliwekwa mahabusu kwa miezi kadhaa, wanachama kimya!!
Mwenyekiti akabambikiwa kesi ya uhujumu uchumi, wanachama kimya!! Hali hiyo ilichangia ajione yupo pekee yake, na wanachama waliopo ni wa kupiga tu porojo!!
Lakini kwa vyovyote iwavyo, CHADEMA kama chama kinachotaka kuwa mbadala wa CCM, ni muhimu sana kifanye tofauti na CCM katika kuelekea kwenye ubora. Tatizo kubwa la CCM ni watu wachache kuhodhi maamuzi, hivyo CHADEMA inatakiwa kuonesha kwa vitendo kuwa maamuzi ndani ya chama hayahodhiwi na watu wachache.