Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

  • kwamba walitaka kumuua, kuna ubishi?
  • kwamba risasi ziliingia mwilini mwake, kuna ubishi?
  • kwamba walishindwa katika azma yao kutaka kumuua, kuna ubishi?
  • kwamba kikosi cha upelelezi kimeshindwa kazi, kuna ubishi?
  • kwamba, kama binadamu yeyote, Lissu amepitia kipindi kigumu, kuna ubishi?
  • kwamba hadi leo, waliofanya hilo jaribio wanaitwa wasiojulikana, kuna ubishi?
Swali ni je, inapofikia Tanpol imefikia ukomo wa uwezo wa kupeleleza, kwa sababu yyt ile, hawaombi msaada kwa vyombo vya kimataifa, k.m Interpol, ambavyo tunakua na mikataba fulani katika kusaidiana kufanikisha shughuli?! badala yake tunatamba kuwa ss hatujashindwa! umepita muda gani hadi ss tunasingizia wasojulkana!

kabla hatujamshutumu Tundu, fatilia dhamira, matamko na maazmio mblmbl yalofanywa juu yake, uvae ubinadamu wake, ingia ktk nafsi yake, yaone yanayomsibu, muone kama mwenye familia halafu ndo uyaseme yanayoujaza moyo wako.
tukubaliane, Lissu wa ss sio yule. walio na shutma dhidi yake, yapaswa ziwe na zimesheheni mantiki zaidi kuliko jazba
 
Ohooo! kusha kucha huku

Lakini mbona hao hao TISS ndo walimpa ulinzi kipindi cha uchaguzi

Au ndo yale mambo ya mchawi mpe mwana akulelee


Amepewa ulinzi na TISS ya Diwani sio kapilimba
 
Walimuita kistaarabu wakajua ni muungwana mwenye hashima zake ataitika akipata wasaa... Bahati mbaya kabla kuitika akaona maisha yako hatarini akakimbilia ubalozin akatiimua

..kabla ya uchaguzi mkuu Lissu alifika ofisini kwa rpc wa Dodoma, hakuhojiwa.

..kipindi cha kampeni IGP Sirro alimtaka Lissu aripoti Polisi kwa kukiuka ratiba ya kampeni, badala ya kumuelekeza ni wapi akahojiwe kutokana na jaribio la kuuwawa.

..baada ya uchaguzi mkuu Lissu alikamatwa na Polisi wakampeleka central lakini hawakumhoji kuhusu kushambuliwa kwake.
 
Watu wengine wana akili sifuri mpaka unashangaa waliwezaje ku login JF!
 
Aondoe shakaa!? Sio rahisi kama mnavyodanganyana. Jaribu hata kwa sekunde kuvaa viatu vyake.
 
Moja katika tiba nzuri sana ni mtu kujieleza, mwacheni Lissu aendelee kujitibu kwa kueleza kila anachokijuwa.


Nnaamini Mama Samia Suluhu kafanya kazi nzuri sana ya kukutana na Lissu na kumtoa hofu aliyonayo.

Waliotajwa hawana chembe ya kujali wala kustuka wala ku "regret" kwani walifanya kazi chini ya kiapo cha kumtii Rais. Hapa wa kulaumiwa si mwengine bali ni "bwana yule".

Lissu ni mwanasheria, ukirudi nyumbani fungua kesi ili haki yako ipatikane kisheria, ikibidi wahukumiwe hata "posthumous".

Wengine wote wanahukumika na wanaweza kupandishwa mahakamani kujibu tuhuma, wataosepa ni wafu tu.

Makonda aka Bashite, hayumo kwenye hicho "kikosi kazi"?
 
Ujinga wa kitoto.
Mdomo mkubwa kuzidi akilj
 
Kwa maoni yangu, Tundu Lissu anahitaji ushauri nasaha. Binadamu ukipitia maswahibu na mapito kama aliyopitia, unaathirika ki fizikia, ki emosheni na kisaikolojia, (physical, emotional and psychological), hivyo anahitaji ushauri nasaha jinsi ya kutoka kwenye jinamizi hili na kuendelea na maisha.

Huku kutaja taja majina ya watu, na kutangazia ulimwengu kuwa vyombo vyetu tukuka vya ulinzi na usalama kuwa ndio walio husika, shambulio lake, bila ushahidi wowote, ni kuzidi kuibagaza tuu nchi yetu!.

Ametaja Kikosi kazi kinachojumuisha Polisi, JWTZ na TISS,, hawa ni askari wetu, trained, how could they do such a messy dirty job?. Kwa trained snipers, only one single shot would have finished the job!. Hili hata Mama Samia amewahi kuizungumzia, askari wetu trained wakimiss target by two shots, wanaandika maelezo kujieleza!.

Mimi kwa upande wangu naendelea kusisitiza Tuacheni ramli chonganishi: Tusihukumu tusije tukahukumiwa. Karma ndio pekee hutoa hukumu ya haki hapa duniani!

Pia Lissu niliisha mshauri na namshauri tena, ajifunze kunyamaza.


Kitendo cha Rais Samia kukubali kukutana na Lissu ni uthibitisho tosha wa kauli na matendo she is healing this nation.

kwenye bandiko hilo nilisema
P
 
Mpumbavu tu, sasa anatetea wahuni wa mkuranga na kibiti iweje? Anaunga matukio ya hovyo kujustify malalamiko yake yasiyo na maana
Umewahi kusikia operation tokomeza? Au ulikuwa bado mdogo sana ukicheza kombolela kipindi hicho?
 
Shida hapa ni uelewa wako kuwa chini. Lissu anazungumza mambo aliyoulizwa na Maria Sarungi kufuatia mahojiano mapya baina ya Rais Samia na BBC hivi karibuni, ambayo yaligusia kuhusu Tundu Lissu kurudi nchini na iwapo serikali inamhakikishia usalama wake
 
Ushauri wako kwa Lissu umekaa 'kichawachawa'. Kwanza, ushahidi kwamba alishambuliwa na TISS hupaswi kuitumia kama hoja ya kupingana na anachokisema. Hii ni kwa sababu haitakuwa mara ya kwanza kwa watu wa vyombo vya dola kuhusisha na matendo hayo. Ulimboka ni miongoni mwa wahanga. Pili, katika tuhuma hizi Lissu hajaombwa ushahidi at this juncture. Halafu kwa sisi tunaoamini uwepo wa Mungu na uingiliaji wake katika matukio mbalimbali, hatuwezi kushangazwa na marisasi ya trained snipers kushindwa kuondoa uhai wa Lissu. Kama Mungu alikuwa hajaamua Lissu afe basi hata wangeletwa masnipers kutoka wapi siku hiyo angebaki na uhai wake.

Hili la mama ku heal this nation unaweza kuwa mjadala ambao hauzuii watu wengine kueleza feeling zao kwenye yale yanayowagusa moja kwa moja. Kitendo alichofanyiwa Lissu ni wachache wanaoweza kukichukulia poa, na nina mashaka kama wewe unaweza kuwa miongoni mwao!
 
Naona kama Rais alikuwa anataka picha tu na Lissu, Dunia ione apate mikopo ya kutosha.
 
Mkuu Paschal , unasema polisi wetu wako well trained hawakosei target hivi liletukio la Hamza pale ubalozini uliliona . wale askari walikua wangapi dhidi ya mtu mmoja .
Kisha jiulize iliwachukua muda gani na risasi ngapi kumlenga jamaa.?
 
Analiponya taifa kutoka kwa nani aliyelifanya liumwe?
 
Mungu akujalie angalau upate madhara yanayoweza kusabihiana japo kidogo tu na yake halafu tujetukukejeli. Ameen
 
Lisu anatukanaaaa alafu akimaliza anaenda kupanda Dreamliner ya Magufuli.

Shame upon him na mme wake amsterdam
Mungu wajalie wote wanaomkejeli akiwemo huyu wape angalau japo ya madhara kama waliomsababishia ili wajifurahiye kama wanafurahia matatizo yake. Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…