Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Hiyo amri ya kuwaua hao uliowataja ilitolewa na nani, lini na wapi?

Unadhani vijiswali vyako uchwara hivi vinauondoa ukweli kuwa mamlaka ilidhamiria rasmi kabisa kumwua huyu bwana?

Kwani hata Jenerali Sabaya hukumsikia akitekeleza operations zile rasmi kabisa kwa maelekezo kutokea wapi?
 
Tatizo unadefine suala la Lissu Kichama. Lissu kalimwa Risasi halafu kaondolewa kwenye Ubunge.

Wewe jasiri sawa. Kuna mtu jasiiri Kama Lissu? Kalimwa Risasi lakini bado alirudi nchini. Kurudi baada ya matokeo wakataka kummaliza ndio kujificha ubalozini. Usipende kuona shida za wengine hazikuhusu kisa upo CCM . Kuna watu wanalia kuonewa wakati just tu Happ walikuwa juu ya sheria. Acha dharau hujui kesho yako.
Lissu kapigwa risasi kila mtu anajua na yote yaliyotokea ulimwengu mzima unafahamu mapaka huyo mama samia anafahamu hayo masaibu yaliyompata kiongozi wako, Tumesikitika sana lakini sasa Lissu anasimamia wapi?? hatua tunasema hazikuchukuliwa lakini Lissu sasa anasimamia wapi?? anarudi nchini hivyo hivyo kuendeleza siasa? au kwa sababu hakuna hatua zilizochukuliwa hadi sasa Ataendelea kubaki belgium?

Kwa sababu kama mwanasiasa lazima awe na msimamo thabiti kufa au kupona kama tunavyoona viongozi mbali mbali duniani wa upinzani wanavyo struggle kutoka kwenye dola tawala lakini sio kama hivi anavyofanya anawaparaganya hata hawa watu wake na chama chake,

Leo ukimuuliza msigwa vipi Lissu kaamua kukutana na mama belgium, msigwa atabaki kimya hana jibu mana si jambo walipanga kwenye chama na haikuwa ajenda ya chama, na hata ukimuuliza Heche pia ataganda kutoa majibu lakini hata huyo Lissu mwenyewe aliulizwa hivi karibuni ni kitu gani kilichompata mbowe kutoka jela akakimbilia Ikulu kwanza jibu lake alisema aulizwe mbowe mwenyewe kuna mikanganyiko na giza nene. Haikueleweka je mbowe ame-sarrenda kwa miezi 8 aliyokaa jela ameshindwa vita au kanunuliwa ili atoke jela au kapewa masharti atatolewa lakini abaki kimya kwa jambo hili na hili nk.

Chadema zamani mulikuwa munaamini Kiongozi wa upinzani akienda Ikulu kuonana na Rais mulikuwa mnasema kwa kelele ni msaliti, mara kadhaa maalim seif ameitwa msaliti ni Chadema, lakini leo chadema wenyewe na wao wanaonekana Ikulu.

Mimi ni muumini wa mabadiliko kupitia vyama vya upinzani kuiondoa CCM madarakani lakini mikanganyo imekuwa mingi sana sasa hatuji ni kiongozi gani hasa wa upinzani ni mkweli na hana chembe za usaliti, lakini nashindwa kufahamu misimamo ya viongozi hawa upinzani sasaiv, nilikuwa na matumaini sana na Chadema kwa Tanzania lakini napata shida sasa
 
Nakubaliana kwa kiasi fulani na hoja hii.
Lisu kaketi na kuongea na mama Samia huko Ubelgiji.
Anayosema Lisu hawakuyaongea?
Kama sivyo waliongea nini haswa!
Body language ya mkutano ule ni kwamba wasiojulikana sasa hawapo na waliondoka na mtangulizi wa mama Samia.
Na experience ya mwaka huu mmoja imedhihirisha hili.
Nia ya Lisu , aidha ni political capital juu ya suala lenyewe-kitu ambacho kina ukakasi, au Lisu anataka waliohusika wapelekwe mahakamani, suala ambalo ni vema likafanyika ingalau gumu kulitekeleza.
Akubaliane na mazingira ya sasa. Sifa ya mwanasiasa ni kuwa na busara ya kukubaliana na kitu ambacho waingereza wanaita 'compromise'.

Bahati mbaya sana JPM hakuwa na uwezo wa kufanya suluhu na wanasiasa wenzake, alikuwa na zile hulka za kisukuma za kushindwa kujishusha katika masuala hata ya msingi na madogo tu.

Mama ni mzenji, na anao utayari wa kujishusha ili muafaka uweze kupatikana, Lissu kama mwanasiasa mzoefu kwa sasa anatakiwa awe ameshaiona tofauti ya SSH na JPM na aitumie katika kujijenga upya kisiasa.

Uzuri wa haya maisha siku zote kuna nafasi ya kuanza upya, kuna nafasi ya kufanyia kazi makosa ya siku za nyuma na kuanza ukurasa mpya.
 
Shida hapa ni uelewa wako kuwa chini. Lissu anazungumza mambo aliyoulizwa na Maria Sarungi kufuatia mahojiano mapya baina ya Rais Samia na BBC hivi karibuni, ambayo yaligusia kuhusu Tundu Lissu kurudi nchini na iwapo serikali inamhakikishia usalama wake
Hana haja ya kutomuamini Samia akisema kuwa eti mazingira ya wasiojulikana kwa sasa hayapo. Rais ni bosi wa taasisi zote nchini, huna sababu ya kutomuamini ikiwa ameshaonyesha kutaka ushirikiano na wewe.
 
Kama ni kweli Marehemu alihusika kwa kuwatumia kikosi kazi TISS na wakatimiza mauwaji hayo, basi Mungu atawalipa kwa walichokifanya.....though siko chadema na wala sina mpango wa kuwa chadema.....Nampenda mama na sio ccm....
 
Ohooo! kusha kucha huku

Lakini mbona hao hao TISS ndo walimpa ulinzi kipindi cha uchaguzi

Au ndo yale mambo ya mchawi mpe mwana akulelee
Hukumbuki pia ile orodha ya mafisadi ambapo Lowassa alikuwemo ila mwisho wa siku Lissu huyo huyo akapanda jukwaani kumpigia debe huyo huyo Lowassa kwamba tumchague awe rais wetu?
 
Yeye ndiye aliyekimbilia ubalozini baada kudai amepokea simu 2 za vitisho dhidi ya maisha yake
Wakati huo kwenye kampeni akikuwa anapanda daladala kwenda kununua nyanya kariakoo!

Nakumbuka pia akiwahi kukatalia barabarani hadi saa 4 za usiku wanazozana na polisi eti wamruhusu afanye kampeni usiku.

Kumuelewa Lisu inabidi uwe zuzu

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Cry baby
Mh. Tundu Lissu awataja waliohusika kumshambulia.

Tundu Lissu amesema Walionipiga risasi ni Kikosi kazi kilichopo chini ya Rais kikisimasimaiwa na Mkuu wa TISS Kipilimba. Kikosi kazi kimeua watanzania wengi sana.

Kimeua watu wengi sana, Kilijumuisha watu wa Usalam wa taifa, Watu wa Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi. Kinaitwa kikosi kazi cha kupambana na Ugaidi na madawa ya kulevya.

Watu wote waliouawa Maeneo ya Mkuranga, Kibiti Kilwa Rufiji zaidi ya watu 400. Wale waliokuwa wanatupwa mtoni maiti zinaokotwa kwenye beach, wote ni Wahanga wa Kikosi hicho.

Ndio waliomteka Ben Saanane, Azory Gwanda Mdude, Mo Dewji. Yote yalitekelezwa na hicho kikosi kazi hichi chiini ya Kipilimba ammbaye sasa ni Balozi.

 
Yeye ndiye aliyekimbilia ubalozini baada kudai amepokea simu 2 za vitisho dhidi ya maisha yake
Kumbukumbu

Msikie hapa👇 akihojiwa
---
 
Back
Top Bottom