Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Kabla ya uchaguzi alifika kufuata gari. Hakukuwa na maandalizi ya mahojiano ndugu.
Na alipokamatwa ilikuwa kwa kesi B sio kesi A. Kipi kigumu kueleweka hapo

..maana yangu ni kwamba kulikuwa na fursa / opportunity ya kumhoji lakini Polisi hawakuitumia.
 
Huyu bwana ni mlalamikaji wa kiwango cha PHD. Kama Rais kafunga safari mpaka Belgium na akataka waonane, ni lazima nia yake iwe ni njema.

Akumbuke kuwa rais ni taasisi yenye watu wengi nyuma wenye majukumu mbalimbali. Hivyo aondoe wasiwasi aliokuwa nao.

Kufariki kwa JPM kumaifanya taasisi ya urais iwe na mabadiliko makubwa. Aondoe shaka.
Mnajiteteaa, amini usiamini majina na Hadi tarehe za vikao na maelekezo mtawekwa wazi tu, na yule mwenye tako mkolomije anayeng'ang'ania vitu vya watu mjini
 
Mnajiteteaa, amini usiamini majina na Hadi tarehe za vikao na maelekezo mtawekwa wazi tu, na yule mwenye tako mkolomije anayeng'ang'ania vitu vya watu mjini
Sipo serikalini, ni mtu baki tu. Natumaini haki yangu ya kufikiri.
 
Wakati wa kampeni za uchaguzi, humu JF si ilishawahi kusemwa kuwa tayari Chadema ina riport ya uchunguzi wa Kupigwa Risasi kwa Lisu?. Uchunguzi uliofanywa kwa msaada wa wabobezi wa kujitegemea ambao ilipelekea kupigwa marufuku Makonda asiingie Marekani.

Nilitamani sana hiyo riport ingetolewa rasmi au pengine ndio maana inampa nguvu Lisu hadi anayaongea anachokifahamu.
 
Lissu kapigwa risasi kila mtu anajua na yote yaliyotokea ulimwengu mzima unafahamu mapaka huyo mama samia anafahamu hayo masaibu yaliyompata kiongozi wako, Tumesikitika sana lakini sasa Lissu anasimamia wapi?? hatua tunasema hazikuchukuliwa lakini Lissu sasa anasimamia wapi?? anarudi nchini hivyo hivyo kuendeleza siasa? au kwa sababu hakuna hatua zilizochukuliwa hadi sasa Ataendelea kubaki belgium?

Kwa sababu kama mwanasiasa lazima awe na msimamo thabiti kufa au kupona kama tunavyoona viongozi mbali mbali duniani wa upinzani wanavyo struggle kutoka kwenye dola tawala lakini sio kama hivi anavyofanya anawaparaganya hata hawa watu wake na chama chake,

Leo ukimuuliza msigwa vipi Lissu kaamua kukutana na mama belgium, msigwa atabaki kimya hana jibu mana si jambo walipanga kwenye chama na haikuwa ajenda ya chama, na hata ukimuuliza Heche pia ataganda kutoa majibu lakini hata huyo Lissu mwenyewe aliulizwa hivi karibuni ni kitu gani kilichompata mbowe kutoka jela akakimbilia Ikulu kwanza jibu lake alisema aulizwe mbowe mwenyewe kuna mikanganyiko na giza nene. Haikueleweka je mbowe ame-sarrenda kwa miezi 8 aliyokaa jela ameshindwa vita au kanunuliwa ili atoke jela au kapewa masharti atatolewa lakini abaki kimya kwa jambo hili na hili nk.

Chadema zamani mulikuwa munaamini Kiongozi wa upinzani akienda Ikulu kuonana na Rais mulikuwa mnasema kwa kelele ni msaliti, mara kadhaa maalim seif ameitwa msaliti ni Chadema, lakini leo chadema wenyewe na wao wanaonekana Ikulu.

Mimi ni muumini wa mabadiliko kupitia vyama vya upinzani kuiondoa CCM madarakani lakini mikanganyo imekuwa mingi sana sasa hatuji ni kiongozi gani hasa wa upinzani ni mkweli na hana chembe za usaliti, lakini nashindwa kufahamu misimamo ya viongozi hawa upinzani sasaiv, nilikuwa na matumaini sana na Chadema kwa Tanzania lakini napata shida sasa
Kama siyo mamlaka, basi mamlaka hiyo itoke hadharani na kuusema ukweli wa nani alihusika kumpiga Lissu risasi, na siyo kumsingizia kuwa eti hadi arudi au mlinzi wake.

Hii itakuwa ni kutufanya watanzania wajinga màana serikali hii hii imeshawahi kufanya uchunguzi wa mauaji na kufanikiwa vizuri bila kuwepo wahusika (wahanga) kwa màana ya wahusika wote kuuawa sembuse hili dogo ambapo eneo la tukio lilikuwa na cctv.

Lawama hizi watazibeba tu.

Angepigwa risasi na mamlaka asingeweza kupona labda mamlaka uchwara
 
Asante sana kwa matusi yako mkuu Allency. Mimi ni mshubi wa Ngara sio msukuma.

JPM alikuwa na mawazo mazuri ya kizalendo, hakutaka tuchezewe kirahisi tu. Alijivunia utanzania wake siku zote.
Alikuwa Mrundi. Mtanzania hawezi kuwa hash kiasi kile. Jitu lilijaa visasi na wizi tu
 
Mh. Tundu Lissu awataja waliohusika kumshambulia.

Tundu Lissu amesema Walionipiga risasi ni Kikosi kazi kilichopo chini ya Rais kikisimasimaiwa na Mkuu wa TISS Kipilimba. Kikosi kazi kimeua watanzania wengi sana.

Kimeua watu wengi sana, Kilijumuisha watu wa Usalam wa taifa, Watu wa Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi. Kinaitwa kikosi kazi cha kupambana na Ugaidi na madawa ya kulevya.

Watu wote waliouawa Maeneo ya Mkuranga, Kibiti Kilwa Rufiji zaidi ya watu 400. Wale waliokuwa wanatupwa mtoni maiti zinaokotwa kwenye beach, wote ni Wahanga wa Kikosi hicho.

Ndio waliomteka Ben Saanane, Azory Gwanda Mdude, Mo Dewji. Yote yalitekelezwa na hicho kikosi kazi hichi chiini ya Kipilimba ammbaye sasa ni Balozi.

Arudi nyumbani, saccos itampa VIP protection ya kina Adamoo.
 
Hajaweka wazi nini haswa hoja yake. Ni kama mtu mwenye wasiwasi usiokwisha kwa vigezo vya mwanzoni mwa maongezi haya.

Inaweza kuwa ni muendelezo wa siasa za mitandaoni, hataki kutoka midomoni mwa watu kirahisi hivyo inambidi aongee hata kama anachokiongea ukikipima hakina undani sana.
Mnaweweseka Ushetani wa Mwendazake Jiwe ukiwekwa hadharani
 
Huyu bwana ni mlalamikaji wa kiwango cha PHD. Kama Rais kafunga safari mpaka Belgium na akataka waonane, ni lazima nia yake iwe ni njema.

Akumbuke kuwa rais ni taasisi yenye watu wengi nyuma wenye majukumu mbalimbali. Hivyo aondoe wasiwasi aliokuwa nao.

Kufariki kwa JPM kumaifanya taasisi ya urais iwe na mabadiliko makubwa. Aondoe shaka.
Kwa hiyo unakiri kuwa Ibilisi Jiwe ndio alitaka Kumuua sio ?
 
Kama siyo mamlaka, basi mamlaka hiyo itoke hadharani na kuusema ukweli wa nani alihusika kumpiga Lissu risasi, na siyo kumsingizia kuwa eti hadi arudi au mlinzi wake.

Hii itakuwa ni kutufanya watanzania wajinga màana serikali hii hii imeshawahi kufanya uchunguzi wa mauaji na kufanikiwa vizuri bila kuwepo wahusika (wahanga) kwa màana ya wahusika wote kuuawa sembuse hili dogo ambapo eneo la tukio lilikuwa na cctv.

Lawama hizi watazibeba tu.
Serikali ndio ishatoa majibu akirudi ulinzi ni kama wanavyoishi watanzania wengine, Tundu aseme sasa what Next ili tushike hapo sio hivi mara vile, anabaki belgium au anarudi
 
Mungu sio mwanadamu unawaza wanaotoa maoni tofauti na nini chawa wa Lisu Mungu awape adhabu! Fuuuuuu! Nyingi ndo lile kundi mlishangilia sana baada ya Magufuli kufariki mkisema Mungu fundi! Kwa hiyo huwezi kuzuia hisia na maoni ya mtu!
Kifo chá magufuli hakikutuathir kwa vile ni muuaji aliyejificha kwenye kiti chá urais.
 
Wasiojulikana kumbe bado wapo chini ya Samia wanatamba tu mtaani halaf ma.a kaufyata!
 
Its just a beggining.!

Lissu anawajua woote waliohusika na lile jaribio la kumtoa uhai, Lissu ana marafiki wema kwenye mfumo!
 
Serikali ndio ishatoa majibu akirudi ulinzi ni kama wanavyoishi watanzania wengine, Tundu aseme sasa what Next ili tushike hapo sio hivi mara vile, anabaki belgium au anarudi
Haya majibu siyo yanayotakiwa hii ni kuendelea kutufanya watanzania kama ta wajinga, watuambie je uchunguzi wa wahusika utafanyika au hautafanyika? kwani hapa nako kuna utata? Maana watuhumiwa bado wapo mitaani tena Wana kula Bata na hapa ndipo hofu ilipo.
 
Hivyo aondoe wasiwasi aliokuwa nao.
Aondoe shaka.
Hayo ndiyo anataka yasemwe na mamlaka, siyo Phillipo mtandaoni.
Wakati fulani nilikuwa nalima shambani nikatega mtego wa kumnasa panya buku. Jembe lilimkosa kidogo; huwezi kuamini, ilikuwa kama saa 10 jioni, hadi kufikia kesho yake saa 2 asubuhi alikuwa ameshakimbia zaidi ya mita 50 chini kwa chini!
Fikiria aliyepigwa risasi kadhaa halafu akanusurika - jiwekeni kwenye viatu vyake muone .....
Tumwache aseme mwisho atatulia
 
Back
Top Bottom