Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Akikujibu usiache kutuletea mrejesho
[emoji16]
Screenshot_20220323-230845.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Umewahi kusikia hata mlio wa baruti, achilia mbali kuparazwa na risasi mwilini kwako?
Kaa ivo ivo kuuliza umewahi kusikia mlio wa baruti... ukiamini kila anaepost humu ni ‘’just anybody’’ 😂
 
Lissu ni coward leader, poor politician, kuna wakati anatufuta suluhu na kusahau yaliyopita arudi nchini, kuna wakati anataka kesi ziendelee kuna wakati kama anataka kurudi tanzania, kuna wakati kama anatafuta sababu kuendelea kuishi belgium

Tumechoka clips za mtandaoni za huyu jamaa, watu kule vijijini ambao walimpigia kura za urais hawaoni wala kupata hizi clips si watu wote wanamiliki hii mitandao anatakiwa ajipambanue kama ana interest ya kuendeleza siasa Tanzania labda na matumaini ya kushika dola kwa chama chake.

Lakini ni kitu gani hasa kilimsukuma kuongea na mama samia belgium, ni kwa vipi alijenga matumaini ya kufanya maongezi na mtesi wake?? Lissu anakuwa hafahamiki anawaparaganya na wenzake, ilibidi mbowe atoke jela amfate mama Ikulu yote ni yeyee
Sasa ofsa hiyo midosho huoni kama inasababishwa na mamlaka ya juu namna wanavyo badilika badilika misimamo wanamfanya naye abadili mitizamo?

Hujamskia kwenye clip akiliongelea hilo kuwa kwa jinsi mambo yanavyofanyika hamkadirii raisi kama ambavyo alivyokuwa anamtizamia?

Au hata samia anapochukua madaraka hukusikia kauli ya lisu alivyo hojiwa BBC alisema ana weka matumaini kwa huyu raisi, lakini baada ya kuona anachukulia poa mambo mazito ni sahihi kuondoa imani ya matumaini kwa mtu huyo
 
Angeishia alivyoshambuliwa

Kutetea kibiti na mkuranga nimemdharau sana
 
Mtu alishambuliwa ili kuuwawa. Imewekwa wazi kuwa laiti angeuwawa washambuliaji wasingekaa wafahamike milele.

Anayetaka Kiki hapo nani? Wewe au yeye?
Mpumbavu tu, sasa anatetea wahuni wa mkuranga na kibiti iweje? Anaunga matukio ya hovyo kujustify malalamiko yake yasiyo na maana
 
Alafu unaweza hisi tangia apigwe risasi akuwai kurudi Tanzania,kumbe alirudi na akatembea nchi nzima kufanya kampeni tena huku akuchimba mikwara.

Inawezekana wewe ni mmoja wapo wa hicho kikosi kazi, Kwani kama alirudi ndo asiwataje waliomshambulia sababu alirudi akafanya kampeni si alikuwa na ulinzi.
 
Tundu Lissu kama ni muadilifu aseme fedha za stahiki zake ni shiklingi ngapi? Na je akilipwa atazipekekwa kwenye charity gani? Walitangazia ulimwengu wote wako watu walifanya charity kumeet gharama zake baada ya serikali kuzuia hizo stahiki zake. Analazimika jwa uungwana tu hizo stahiki zake anazo idai serikali kuzirudisha jwwnye charity.
U shetani wewe. Una roho mbaya hadi inanuka.
 
Lissu huwa anaongea anachoona kwake ni sahihi....

Na hakuna ulazima kiwe sahihi kwa wote pia
Mbona hajamtaja baba yako? Mwacheni aseme. Watawala walikuwa na maana yao waliokataa uchunguzi. Aseme chochote awezacho.
 
Tueleze basi mkuu, who are you?

But be sure, whoever you're, that won't impress anybody, if your actions are lousy.
Ni member tu wa JF mkuu ... !
But tambua JF ina watu wa kila namna na kila unachotafuta Duniani kipo hapa JF...!

Binafsi nimekutana na watu kutoka sehemu mbali mbali Tanzania na nje ya Tanzania hapa hapa JF na baadhi tumekua ndugu na baadhi kwa kutumia skills,knowledge,education,trust nk tumefanya Na kufanikisha projects mbali mbali ... ni kubadili tu mtazamo wa namna unavowachukulia watu humu au popote unapokutana na new people itakusaidia sana na utakuja gundua baadae kumbe ata mtu ambae ungeweza kumtusi Au kumdharau ni daraja ambalo hukulifikiria...

Humu watu wanayo comment sometimes no contrary kabisa na reality walivo.... just some hints ... take it or drop it
 
Hili na mimi ndio nilikua nataka kulisema haya yote anazuga tu pesa ya ukimbizi ya bure keshaiona tamu kuliko kurudi bongo. Asiwasingizie watu ubaya kikosi cha kujumuisha TISS, JWTZ na polisi kingemtaka kisingetumia risasi 36 na atoke mzima. Hao jamaa wa kazi risasi mbili tu angekua sasa hivi jina lake linatanguliwa na marehemu. waliompiga risasi hawajui anabahatisha ila watakua ni wahuni tu waliotaka kuivuruga nchi. Lisu anatafuta scapegoat ya kutorudi bongo mjanja sana huyu wakili msomi😀😀😀😀[emoji23][emoji23][emoji23]

Kwahiyo jeshi letu la polisi limeshindwa kukamata wahuni waliomshambulia mtu mchana kwenye makazi ya viongozi wa serikali. Mbona kama unataka kuwafanya watanzania wajinga sana. Hivi yule mfanya bishara wa mtwara aliyeuawa yule wahusika wamejulikanaje nayeye hayupo ili ahojiwe. Ni sahihi kiongozi wa nchi kusema upelelezi hauwezi kufanyika kwakuwa Lissu hayupo. Au hakuna cha kupeleleza wahusika ndiyo hao waliotajwa na walitumwa na kiongozi. Hii kesi kuna siku wahusika wote watafikishwa kizimbani maana jinai huwa haiishi, hata ipite miaka mingapi siku itafika tu.
 
Huyo jamaa alikuwa nchi gani alipouliwa Na alikuwa pia Na uraia wa nchi gani?
Anwar Al awlik alikua mmarekani,aliuliwa Iraq au Yemen sikumbuki,,lakini off the record hata ndani ya US ukionekana tishio wanakupiga chuma,,
hizi nchi zetu,hata mkuu was kituo TU anaweza ku order uwe termed iwapo utaonekana kutishia usalama,,
 
Mh. Tundu Lissu awataja waliohusika kumshambulia.

Tundu Lissu amesema Walionipiga risasi ni Kikosi kazi kilichopo chini ya Rais kikisimasimaiwa na Mkuu wa TISS Kipilimba. Kikosi kazi kimeua watanzania wengi sana.

Kimeua watu wengi sana, Kilijumuisha watu wa Usalam wa taifa, Watu wa Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi. Kinaitwa kikosi kazi cha kupambana na Ugaidi na madawa ya kulevya.

Watu wote waliouawa Maeneo ya Mkuranga, Kibiti Kilwa Rufiji zaidi ya watu 400. Wale waliokuwa wanatupwa mtoni maiti zinaokotwa kwenye beach, wote ni Wahanga wa Kikosi hicho.

Ndio waliomteka Ben Saanane, Azory Gwanda Mdude, Mo Dewji. Yote yalitekelezwa na hicho kikosi kazi hichi chiini ya Kipilimba ammbaye sasa ni Balozi.

Duuh hatari
 
Huyu bwana ni mlalamikaji wa kiwango cha PHD. Kama Rais kafunga safari mpaka Belgium na akataka waonane, ni lazima nia yake iwe ni njema.

Akumbuke kuwa rais ni taasisi yenye watu wengi nyuma wenye majukumu mbalimbali. Hivyo aondoe wasiwasi aliokuwa nao.

Kufariki kwa JPM kumaifanya taasisi ya urais iwe na mabadiliko makubwa. Aondoe shaka.
Elewa anamsaidia rais afahamu ni watu wa aina gani anafanya nao kazi na si vinginevyo. Kumbuka hata wewe kuna wakati unakua informer kuwaambia polisi wahalifu ni kina nani kwakuwa polisi peke yao ingawaje ni taasisi kuna wakati inawalazimu kufanya kazi na informers
 
Back
Top Bottom