Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Mbona hajamtaja baba yako? Mwacheni aseme. Watawala walikuwa na maana yao waliokataa uchunguzi. Aseme chochote awezacho.

Amtaje Baba yangu kwa sababu zipi..???..

Umeelewa bandiko langu mkuu
 
UKo sahihi sana, ila hili analoongea Sasa ni ukweli wa wazi, suala la kuwa sahihi kwa wote hilo utajua ww.

Nilimaanisha hvo pia,, kwamba lissu huwa anasema achoona ni sahihi kwake.,, so kama kwako unaona ni sahihi ila kwa samia anaona sio sahihi.

Na wapo pia wanaoona ni sahihi mioyoni mwao,, ila mbele ya jamii wanajifanya kuona kama sio sahihi...

Infact ni ngumu kumuamsha aliyejifanya amelala,,, Tundu Lissu ndio kazi anayofanya,,, Walawala wanajifanya wamelala so ni kazi sana kuwaamsha.
 
Angepigwa risasi na mamlaka asingeweza kupona labda mamlaka uchwara

..mamlaka inaundwa na wanadamu.

..na jambo lolote linalofanywa na wanadamu linaweza kufaulu au kufeli.

..kwa hiyo mamlaka inaweza kuwa walijaribu kumuua lakini wakafeli.
 
Ilikuwa hakuna namna katika level ya mtaa ukijulikana wewe ni KERO wanachi wenye hasira Kali WANAFANYA Yao.
Kwenye kijiji nk.kuna namna ya kupambana na wanaokera.

Kudharau,kutukana kujimwambafai,kutweza ni mambo ambayo yanaweza kuchangia kupata kipigo na wengi wamepata matatizo makubwa.

Naamini unaweza kutumia staha na ukafanikiwa kama Dr.Slaa,Lowasa NK.
Lakini siasa za kina Bashite,Yule aliyefungwa miaka 30,Lamwai,Marando,Hayati Mtikila NK zinahitaji ujipange kivita na Vita haina macho.

Nchi ni yetu sote na wote tuna haki na majukumu ya kuhakikisha tunakomesha Kwa pamoja Yale yote ambayo ni KERO kwetu.
 
Kipilimbi bado yupo TISS? Hicho Kikosi Kazi anachodai bado kina exist? This dude has simply lost touch of reality and needs some serious psychological rehab or maybe even psychiatric treatment. He appears to be living in a bubble and sounds very paranoid and vindictive. Mtu wa visasi. Kila akihojiwa lazima aje na ishu ya yeye kupigwa risasi na blah blah zake za stahiki za matibabu etc. "Saaasaaa", "Saaasaaa" kila sentensi.
 
Hapo ndio unaoona umetupoteza maboya? Unadhani sisi ni watoto au mafamba na hatujui ukweli anaouzungumza Lisu.
Nilitarajia ungeweka bayana sababu ya dereva kufichwa Ulaya kwa gharama kubwa sana na pia sababu ya watu wazima wenye wadhifa kwenye chama kuongea uongo hadharani bila aibu kwa kusema dereva anatibiwa kisaikolojia
 
Nilitarajia ungeweka bayana sababu ya dereva kufichwa Ulaya kwa gharama kubwa sana na pia sababu ya watu wazima wenye wadhifa kwenye chama kuongea uongo hadharani bila aibu kwa kusema dereva anatibiwa kisaikolojia

..kama unajua dereva yuko ulaya ina maana kwamba hajafichwa.

..na kama serikali inaamini kwamba dereva ni mhalifu inatakiwa itoe taarifa zake Interpol ili aweze kukamatwa huko aliko na kurejeshwa nchini.
 
Tundu Lissu kama ni muadilifu aseme fedha za stahiki zake ni shilingi ngapi? Na je akilipwa atazipeleka kwenye charity gani? Walitangazia ulimwengu wote wako watu walifanya chariy kumeet gharama zake baada ya serikali kuzuia hizo stahiki zake. Analazimika kwa uungwana tu hizo stahiki zake anazo idai serikali kuzirudisha kwenye charity.
Kwani alikopa huko charity? Hivi umepungukiwa akili kiasi hiki kweli?
 
Mh. Tundu Lissu awataja waliohusika kumshambulia.

Tundu Lissu amesema Walionipiga risasi ni Kikosi kazi kilichopo chini ya Rais kikisimasimaiwa na Mkuu wa TISS Kipilimba. Kikosi kazi kimeua watanzania wengi sana.

Kimeua watu wengi sana, Kilijumuisha watu wa Usalam wa taifa, Watu wa Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi. Kinaitwa kikosi kazi cha kupambana na Ugaidi na madawa ya kulevya.

Watu wote waliouawa Maeneo ya Mkuranga, Kibiti Kilwa Rufiji zaidi ya watu 400. Wale waliokuwa wanatupwa mtoni maiti zinaokotwa kwenye beach, wote ni Wahanga wa Kikosi hicho.

Ndio waliomteka Ben Saanane, Azory Gwanda Mdude, Mo Dewji. Yote yalitekelezwa na hicho kikosi kazi hichi chiini ya Kipilimba ammbaye sasa ni Balozi.

inasemekana risasi huwa zna sumu ya kudumu znaweza sababisha had ukichaa ohooo

Sent from my itel W6004 using JamiiForums mobile app
 
Wajasiria siasa utawajua tu. Fungu litapungua na mko wengi sana ilioguswa na hii post.
Wewe ndio una wivu wa kike kike! Wakati mwingine unaweza kujilaumu na kuona michongo yako haiendi fresh kumbe gundu unalitafuta mwenyewe. Badilika you young lady
 
God of Nazareth anahusika vipi ,Hivi haya mauwaji Na mateso Itakuwa wewe ni katika watu wa kikosi kazi
Who knows...unayumba sana, hizo ramli zako zinatabu sana
 
Hivi umeandika ukiwa umelewa?

Unauthibitisho gani Magufuli alitoa maagizo ya kuuwa Tundu Lissu?

Iweje pia wauaji wakashindwa?

Ama karma ndiyo ikapelekea Rais wetu mchapakazi akatangulia yeye?

Hebu iweke sawa hii mkuu.
Lisu mjinga mchungaji Kipilimba mlokole alikataa kumwaga damu ya Lisu Magufuli akampiga chini na kumpa ubalozi Namibia akamtoa usalama wa taifa baada ya kugoma Kuua Lisu

Waliopewa mission ya Kuua Lisu ikawa unsuccessfully sababu ya maombi ya mchungaji Kipilimba

Lisu awe na shukrani hakufa mpuuzi mkubwa
 
Alijitolea au aliteuliwa? Na je kiapo chake kilikua na maana gani?je alikua halipwii?
Hata kukubali kiapo ni wito...Tuwaenzi walinzi wetu...Ni thawabu kwa Mungu kuheshimu kazi za watu ikiwemo yangu na yako ukiifanya kwa uadilifu
 
kama ni kweli, case closed,,amiri jeshi was nchi yeyote Dunia,ananguvu sana,
cheki Trump alitoa amri TU,watu wakapotea,,
huu ukweli watu wanajifanya hawautambui,,bush aliamuru jeshi liingie iraq ,matokeo take watu milioni kadhaa walikufa,,,
mfalme Daud,aliaamuru kamanda wake mkuu auWe ili tu yeye arithi Mke,,
kama anavyodai ni kweli Lisu awe mpole tu,hakuna kitu sisi tutaweza msaidia
Mbona Magu hakutoa amri kama ya hao marais.

Angesimama na kuagiza kabisa kaueni Tundu Lissu.
 
Kipilimbi bado yupo TISS? Hicho Kikosi Kazi anachodai bado kina exist? This dude has simply lost touch of reality and needs some serious psychological rehab or maybe even psychiatric treatment. He appears to be living in a bubble and sounds very paranoid and vindictive. Mtu wa visasi. Kila akihojiwa lazima aje na ishu ya yeye kupigwa risasi na blah blah zake za stahiki za matibabu etc. "Saaasaaa", "Saaasaaa" kila sentensi.
Sishabikii mtu kukatishwa uhai wake na wala si muumini wa kuonea watu, but sometimes ku play victim pia ni dhambi mbaya sana...The guy seems to be so...Hajui hata kuji self evaluate nakuona ni kwa jinsi gani na yeye ana makosa yake katika hilo na kisha angesamehe pengine angepata haki yake zaidi ya hivi kuwa cry baby na kutegemea hisani ya watu ambao hawakuwahi kutoa hisani kwa bara letu...Mungu na amsaidie ajue kuwa hakuna haki nje ya Mungu na huanza kuoatikana pale wewe unaposamehe ili sasa wale malaika wazamu watumie binadamu kumpa haki yake
 
Nilitarajia ungeweka bayana sababu ya dereva kufichwa Ulaya kwa gharama kubwa sana na pia sababu ya watu wazima wenye wadhifa kwenye chama kuongea uongo hadharani bila aibu kwa kusema dereva anatibiwa kisaikolojia

Tuna uzoefu na vyombo vyetu vya uchunguzi, kwenye shambulio la aina ile wangemtisha huyo dereva na kumuwekea maneno mdomoni ili kupindisha ukweli. Mfano halisi wa uchunguzi wq vyombo vyetu vya dola, ni ushahidi wa uongo uliokuwa unatolewa na polisi kwenye kesi ya Mbowe. Ni mjinga tu anayeweza kuamini vyombo vyetu vya dola kuwa vinaweza kuchunguza shambulio kama la Lisu na kutoa taarifa ya ukweli. Hata Lisu asingeenda kutibiwa Nairobi kisha apelekwe Muhimbili, leo hii ingekuwa ni kumbukumbu ya kifo chake.
 
Back
Top Bottom