Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Labda ujifanye umesahau. Wakati Lissu akiwa Nairobi na akawa ameanza kufanya mahojiano na vyombo mbali mbali vya habari IGP Sirro alitamka kuwa atapeleka vijana wake Nairobi kwenda kumhoji ili shauri liweze kuendelea. Wa kwanza ku-react alikuwa mgonjwa Lissu akidai kuwa polisi wa Tanzania hawana uwezo wa kumhoji akiwa Kenys labda wapate kibali cha mwanasheria mkuu wa Kenya. Sasa kwa nini Lissu afikiri kuwa IGP wa Tanzania hafahamu taratibu??? Cha kushangaza zaidi ni kuwa baada ya hili tamko la IGP Sirro, ilichukua muda mfupi sana Lissu na dereva wake wakahamia Ubeljiji. Inabidi ujivue ufahamu sana ili uone kuwa matukio hayo ya Lissu ni ya kawaida. Dereva aliyekuwa anatibiwa kisaikolojia Nairobi mara anahamishwa ghafla na mgonjwa Lissu kwenda Ubeljiji!!!!
P
 
P

..IGP Sirro alisema ametuma makachero wake wale top kabisa kwenda Dodoma kuchunguza tukio la Lissu.

..huu ni mwaka wa 4 tangu makachero watumwe Dodoma hatujasikia kama walitoa mrejesho gani IGP.

..Lakini Polisi walisema wame-retrieve CCTV cameras toka eneo la tukio.

..Binafsi najiuliza, hivi kunaweza kuwa na ushahidi mwingine mzuri kuliko unaoonekana kwenye cameras?

..Na madai kwamba ulinzi wa area D uliondolewa siku ya tukio?

..Hivi aliyeondoa walinzi aliagizwa na nani? Na aliyetoa maelekezo walinzi waondolewe hahusiki kweli na mipango ya kumshambulia Lissu?

Cc Meela
 
Hakuna visingizio tuliona kesi ya Lipumba Na CUF, kwa mahakama hizi Za CCM ni kupoteza wakati

Sasa malalamiko kwamba polisi hawajachunguza ni ya nini kama unaamini mahakama zetu zenyewe ni hopeless?
 
Taifa lenye kujielewa haliwekezi kuua Raia wake, bali huwalinda kwa kila namna pasipo kujali tofauti zao.

Sasa Rais kinachomfanya ashindwe kumpa guarantee ya usalama wake ni nini kama kweli hawana nia ovu?

Kwahiyo kila Mtanzania aliyewahi kunusurika (au atakayenusurika) kuuawa anastahili kupata guarantee ya Rais juu ya usalama wake? Wapo wengi wa aina hiyo!
 
Hili na mimi ndio nilikua nataka kulisema haya yote anazuga tu pesa ya ukimbizi ya bure keshaiona tamu kuliko kurudi bongo. Asiwasingizie watu ubaya kikosi cha kujumuisha TISS, JWTZ na polisi kingemtaka kisingetumia risasi 36 na atoke mzima. Hao jamaa wa kazi risasi mbili tu angekua sasa hivi jina lake linatanguliwa na marehemu. waliompiga risasi hawajui anabahatisha ila watakua ni wahuni tu waliotaka kuivuruga nchi. Lisu anatafuta scapegoat ya kutorudi bongo mjanja sana huyu wakili msomi😀😀😀😀😂😂😂
Wataje wewe
 
Lkn kabla ya kupigwa risas si alishawataja wanaomfuata fuata wametumwa na kipilimba pamoja na siro
Au na hili tena linahitaji mjadala
 
Rais alishamtembelea wakati akiwa mgonjwa , na baadae rais ameenda Belgium kikazi lakini akatenga muda wake ili aongee nae hilo tu lingemuonesha kua usalama wake ni kipaumbele kwa serikali hii. Mama angeweza kumpotezea tu hata asionane nae huko Belgium kwani Tundu Lisu ni nani??? Ulinzi gani anaoutaka kwa sasa ??? au anataka walinzi toka Scotland Yard na FBI??? Huyu jamaa mie namuona siasa imeshamshinda sasa hivi anataka kupigania tumbo lake na familia yake basi .
TL na Mbowe kuwa gerezani ilikuwa ni kero kwa mama, Tz ingekuwa kama Urusi angeendelea kushupaza shingo lkn haiwezekani, mama kila alipokanyaga anaulizwa hao watu wa wili na mama naye anataka kusafishanchi, akaona isiwe taabu. Kwahiyo yawezekana yasiwe ni mapenzi yake mojakwa moja bali ni kama shinikizo, Yawezekana hautaki kufika kwenye msiba wa jirani yako au ndugu yako kwa sababu ya ugonvi wenu lkn kwa kufikiria kuwa jamii ya pale itakuonaje ukalazimika kufika ili usiharibu taswira na heshima yako, kwani kutofka kila aliyekuzunguka atauliza kwanini haukwenda kwenye msiba sasa hiyo ikawa kero kwako.
 
Lkn ukimsikiliza sana utaona bado hajapona. Hii kauli ni kama ilimchomoka tu
 
Back
Top Bottom