Makosa hayo ya kiuandishi sio utetezi kabisa kisheria, Tundu anajua hilo na hiyo barua kupelekwa kwa Mwenyekiti wa Chama chake kwake sidhani kama ni utetezi anapaswa atambue kuwa Chama ni Cha mwenyekiti na Chama hicho ndio kimemdhamini yeye kuwa Mgombea wa Urais na hata alipofika Tume aliwasilisha barua ya Utambulisho kutoka kwa Chama ambayo Katibu wa Chama ndio alimtambulisha Tume. Hivyo Polisi kumtaarifu Mwenyekiti juu ya hilo ni sahihi kabisa kuwa mtu wako anahitajika. Na anahitajika kuhojiwa kutokana na matamshi na kauli zake alizozitoa.
Tundu anachofanya ni kuchelewesha tu lakini bado sheria inambana.