Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Salamu kiongozi, mwenye dhamana yangu na watanzania wenzangu.

Naomba niwe mjumbe wa wanawake wote wenye ulemavu, haswa wale ambao wanaviungo vyote vya mwili ila wanakosa usikivu,

~ Elimu kwao imekuwa kwa taabu sana kwenye Nchi yetu.
~ Ajira kwao zimekua za taabu sana.

Kundi hili nadhani ile mikopo ya halmashauri ingewazingatia sana. Maana wamekuwa watu wakutengwa sana ilhali wana nguvu zao.

Mngeliangalia hili, hata waweze kujiunga na ujasiriamali kwa mikopo ile. Maana mikopo inapotea bila kufika kwa wahusika.

Swala hili nililifuatilia na nikaona ni la kukera. Je, Wizara yako imejipangaje pia kwenye maendeleo ya wananchi wenu wa kundi hilo?

Kama mmoja wa vijana ninayepambana kuwapa moyo, kuwasaidia wanawake wa kundi hilo ningependa kupata maelezo.

Nawakilisha.
 
Mh. Waziri umeupiga mwingi sana kujiunga hapa...karibu sana.
 
1. Katika kutoa semina za kuwawezesha wanawake, msifundishe kama vile wana ugonvi na wanaume, mjikite katika kujenga familia madhubuti.
Namimi nalisisitiza hili[emoji122]
 
Mh. Waziri,

Tafadhali tunaomba msaada muwasaidie wale watoto wanaoishi pale Ubungo darajani na wengine mwenge na pale jangwani waiteni mukae nao mujue chanzo cha wao kuwa pale, wapelekeni hata shule au wale wakubwa waende VETA.

Wale watoto nina uhakika wana wazazi ama wengine walilelewa na mama wa kambo wakakimbia mateso, manyanyaso na ugumu wa maisha nyumbani kwao, wasikilizeni muone vile mutawasaidia

Usiku wanalala pamoja wale wakubwa na wadogo, nina mashaka sana huenda wanaingiliana sana kinyume na maumbile (hawa ndio mashoga wazoefu wa baadae). Niliwahi kupata taarifa kuwa kuna watu wazima wanakuja na magari pale, wanawachukua wanaenda kuwapiga, kuwalawiti, wanawapa hela kidogo, wanarudi pale. Yaani hao ni watoto wa kiume wanaojiuza.

Maoni yangu; nendeni mkawasaidie tafadhali. Kama serikali haina msaada muwafukuze pale waondoke kabisa.
 
Mm nafanya kazi za child protection nimefurahi kukutana na wewe mh waziri maoni yangu nitayatoa wakati mwingine ila umefanya jambo jema
 
Heri ya Pasaka wana JamiiForums,

Mimi ni Dkt. Dorothy Gwajima, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum.

Ninayo furaha kujiunga nanyi katika mtandao huu. Nimekuwepo hapa tangu 2015 kama msomaji zaidi lakini sasa rasmi nitakuwa active member.

Naamini JF itakuwa sehemu nzuri ya kupokea maswali, maoni na mawazo yenu kuhusu namna tunavyoweza kuboresha maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake, na watu wenye makundi maalum nchini Tanzania.

Hivyo, ninawakaribisha nyote kushiriki kwenye majadiliano haya na mimi niko tayari kujibu maswali yenu na kusikiliza maoni yenu na hata kuyafanyia kazi haraka pale inapobidi.

Unaweza kutoa maoni yako kwenye mjadala huu au kupitia ujumbe wa faragha (PM).

Karibuni
Habari waziri, napenda kukujulisha kuwa wizara yako hii kwetu vijana bado ni ngeni sana. Bado hatuijui kwenye ground level kabisa, hatujui taasisi inazozisimamia, mipaka yake ya kimamlaka, wadau wakubwa, na participants wake wakuu ni wapi.

Desk zake za kukusanya matatizo ni zipi kwenye level za halmashauri hadi kata. Fursa kubwa kwenye hii wizara ni ipi?

Tunaomba kuelimishwa ili tuweze kunufaika na hii wizara.
 
Mheshimiwa waziri karibu sana JF, hongera pia kwa uthubutu wa kujiunga, uwekuwa mfano bora kwa viongozi wengine.

Mimi nakushauri muwawekee udhibiti hawa kwenye vibanda vya kuonyesha mipira na video (Vibanda umiza), hawa wengi sio waaminifu na kwa sababu wao wanajali pesa wakati mwingine huonyesha hata video zisizofaa, tena bila kujali hata kama kuna watoto. Hawa tafuteni namna ya kuwadhibiti ili wasiendelee kuharibu maadili ya jamii.

Pili, kwenye mabasi ya abiria kuna tabia pia ya kuweka movie na nyimbo ambazo hazina maadili kabisa bila kujali kwamba mule watu waliopo ni wa rika tofauti. Wengine wanasafiri na watoto wadogo, wengine wanasafiri na wakwe zao nk.

Huko nako angalieni namna ya kudhibiti, maana kama wanaweka movie ambazo iko rated 18+ wana uhakika mule hakuna watoto?

Jitahidini sana kuwadhibiti hawa watu wanachangia sana uvunjifu wa maadili.
 
MH WAZIRI
Tafadhali tunaomba msaada muwasaidie wale watoto wanaoishi pale Ubungo darajani na wengine mwenge na pale jangwani waiteni mukae nao mujue chanzo cha wao kuwa pale, wapelekeni hata shule au wale wakubwa waende VETA.

Wale watoto nina uhakika wana wazazi ama wengine walilelewa na mama wa Kambo wakakimbia mateso,manynyaso na ugumu wa maisha nyumbani kwao wasikilizeni muone vile mutawasaidia

Usiku wanalala pamoja wale wakubwa na wadogo nina mashaka sana huenda wanaingiliana sana kinyume na maumbile(hawa ndio mashoga wazoefu wa badae) niliwahi kupata taarifa kuwa kuna watu wazima wanakuja na magari pale wanawachukua wanaenda kuwapiga kuwalawiti wanawapa hela kidogo wanarudi pale yaani hao ni watoto wa kiume wanaojiuza

MAONI YANGU NENDENI MUKAWASAIDIE TAFADHALI, KAMA SERIKALI HAINA MSAADA MUWAFUKUZE PALE WAONDOKE KABISA
Duuuh maskinii wee, hali ni mbayaa kwa kweli.
 
Sema tumshauri Dkt. Gwajima D wapige marufuku vigodoro, baikoko, inayofanyika mitaani kwa uwazi. Huko ndiko kiwanda, chimbuko la madudu yote.

Ova
 
Duuuh maskinii wee, hali ni mbayaa kwa kweli.
Kuna wakati pale walikuwa wanafukuzwa wanarudi
Ila kwa ubongo pale si walipazungushia uzio, sasa sijui kama bado watoto wanaingia mule tena au la

Ova
 
Kuna wakati pale walikuwa wanafukuzwa wanarudi
Ila kwa ubongo pale si walipazungushia uzio, sasa sijui kama bado watoto wanaingia mule tena au la

Ova
wapo mkuu na ikifika usiku wanapanda zile waya wanarukia ndani kule juzi nimetoka Dar hapo nimewaona wengi sana. ukitaka kujua wingi wao pita kuanzia saa nne wote wanakuwa sehemu moja
 
wapo mkuu na ikifika usiku wanapanda zile waya wanarukia ndani kule juzi nimetoka Dar hapo nimewaona wengi sana. ukitaka kujua wingi wao pita kuanzia saa nne wote wanakuwa sehemu moja
Napajuwa vizuri sana hapo, kuna wakati tushaingia hapo ilikuwa kama saa nane usiku, kuna mtoto tulienda kumchomoa. Ni kitambo, alitoroka kwao sasa mjomba wake alikuwa anamtafuta.

Hapo kundi la watoto walitutolea visu, viwembe, yaani ilikuwa tafrani! Pale siyo kabisa na watoto pale wanapaona kama heave.

Watoto wengi pale kisaikolojia washaaribikiwa, mtoto anayekaa pale lazima awe bandidu, kutokana na maisha wanayoishi.

ova
 
NAPAJUWA VIZURI SANA HAPO,KUNA WAKATI TUSHAINGIAGA HAPO ILIKUWA KAMA SAA NANE USIKU,KUNA MTOTO TULIENDA KUMCHOMOA...KITAMBO ALITOROKA KWAO SASA MJOMBA WAKE ALIKUWA ANAMTAFUTA
HAPO KUNDI LA WATOTO WALITUTOLEA VISU VIWEMBE YAANI ILIKUWA TAFRANI.....
PALE SIYO KABISA NA WATOTO PALE WANAPAONA KAMA HEAVEN
WATOTO WENGI PALE KISAIKOLOJIA
WASHAARIBIKIWA
MTOTO ANAYEKAA PALE LAZIMA AWE BANDIDU ,KUTOKANA NA MAISHA WANAYOISHI

ova
hahahaha kwa hiyo huyo dogo mulishindwa kabisa kumchomoa hapo?
 
Kuna wakati pale walikuwa wanafukuzwa wanarudi
Ila kwa ubongo pale si walipazungushia uzio, sasa sijui kama bado watoto wanaingia mule tena au la

Ova
Duuuh inasikitishaa mnooo.
 
hahahaha kwa hiyo huyo dogo mulishindwa kabisa kumchomoa hapo?
Tushindwe tena? Tulimchomoa, na usiku ule ule alisafirishwa kwa mjomba wake Songea!

Yaani pale mamlaka husika wakisema waende, wapeleke kabisa karandinga kuwabeba wote wawatoe pale.

Ukiongea na baadhi ya watoto pale kila mmoja ana mkasa wake. Sana sana mambo ya kifamilia yamewakimbiza, sijui mama wa kambo, baba wa kambo, wengine wazazi wote wamekufa familia haiwatazami tena, wengine akili zao ujeuri tu nk.

Hivi Dogodogo Centre ipo bado?

Ova
 
Back
Top Bottom