Hili la Wamachinga lisiangaliwe kwa upande mmoja wa shilingi, ukigeuza mwingine ni kuna MaDon kwa makusudi mazima ya kukwepa kodi wanaleta vijana kutoka vijijini wanawapa bidhaa waingie nazo mitaani kwa mgongo wa MACHINGA huku wao wakinufaika,
Machinga ana uwezo wa kununua hadi mzigo wa Milioni 5 huyo ni Machinga???
Bidhaa zao ni ghali kuliko za dukani, wasiopenda kutembea wanadhani wamenunua kwa rahisi kumbe kapigwa dabo na machinga,
Sipati kusema hiyo kuchafua jiji na lugha chafu,
Naipongeza sana Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mama yetu mpenzi SSH, kufanya maamuzi magumu ni jambo la kuumiza lakini litazoeleka,
Bado hawa Omba Omba wanaowatembeza watoto wadogo kwenye jua kali na wengine kuwanyima haki yao ya kusoma na kuwageuza mtaji, habari zao tunazo wanafadhiliwa na watu jioni wanapeleka hesabu.