Tupeana updates za kuhama kwa Wamachinga
Hili la Wamachinga lisiangaliwe kwa upande mmoja wa shilingi, ukigeuza mwingine ni kuna MaDon kwa makusudi mazima ya kukwepa kodi wanaleta vijana kutoka vijijini wanawapa bidhaa waingie nazo mitaani kwa mgongo wa MACHINGA huku wao wakinufaika,

Machinga ana uwezo wa kununua hadi mzigo wa Milioni 5 huyo ni Machinga???

Bidhaa zao ni ghali kuliko za dukani, wasiopenda kutembea wanadhani wamenunua kwa rahisi kumbe kapigwa dabo na machinga,

Sipati kusema hiyo kuchafua jiji na lugha chafu,

Naipongeza sana Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mama yetu mpenzi SSH, kufanya maamuzi magumu ni jambo la kuumiza lakini litazoeleka,

Bado hawa Omba Omba wanaowatembeza watoto wadogo kwenye jua kali na wengine kuwanyima haki yao ya kusoma na kuwageuza mtaji, habari zao tunazo wanafadhiliwa na watu jioni wanapeleka hesabu.
Umeongea ukweli mtupu
 
Kumbe kichwa chako kibovu.
Kuwapanga wamachinga nako NI kuwasaidia?
Kuna wamachinga wangapi wanna elimu kwanini asiwape ajira?
hivi umachinga nayo ni kazi ?
So wanafanya tu sababu ya shida
We jamaa..hivi unadhani kazi ni kuchukua na kuwapa watu kama peremende..kuna utaratibu wa kuajiri pia kulingana na bajeti..ukiwaajiri ushindwe kuwalipa unataka iweje.

#MaendeleoHayanaChama
 
Njia bora ya kuondoa machinga na kupunguza bodaboda mijini ni kuboresha kilimo.
 
Kuna mitaa nusura kijiko kiondoke na machinga washukuriwe walinzi wa sheli baada ya kupiga kelele kuna mtu kalala ndani
 
Mji ulikuwa kama wanaishi Wanyama na sio binadamu
Na shida ni kwamba population inaongezeka na vijana ambao wangeendelea kuja mijini kufanya Umachinga wangeongezeka mara dufu..yaani ingezidi kuwa balaa..

Serikali ni bora ikaze watu waumie lakini baada ya hapa kila mtu ajue atatafuta mkate wake kwa utaratibu sahihi na bila kubughudhi wengine.
 
Huku kwetu Dom tumepangiwa eneo zuri sana yaani no malalamiko nawapongeza Mh.Mtaka, Mh Shekimweri na mkurugenzi wa jiji
 
Tunachekelea tukienda nchi za wenzetu kwamba zinapendeza, mandhari nzuri, mpangilio wa shughuli za kiuchumi ziko vizuri, haikuwa rahisi kuwa hivyo, ni matokea ya usimamizi mzuri na mkali wa serikazi zao, cha msingi mtu asionewe, tusitafute huruma kwa kuvunja utaratibu uliowekwa.

Naimani serikali imewaandalia maeneo sahihi ya kufanya shughuli zao. Na sisi ambao niwateja wao tutawafuata huko waliko.
 
Back
Top Bottom