Tutafanya nini na Serikali mnayo nyinyi wakristo ?
Mnafanya ujangili Mali zinafichwa makanisani. Kama vile Yesu na roho mtakatifu ndio walinzi.
Unaweza kuniambia kesi ya huyu Padri iliishia vipi ?
PADRI AKAMATWA KWA UJANGILI HUKU BUNDUKI 48, RISASI 764 ZIKIKAMATWA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda, akionyesha bunduki aina ya AK47 kati ya silaha zilizokamatwa katika msako maalum wa ujangili.
Na Daniel Mbega, Namanyere
PADRI wa Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga (jina linahifadhiwa) ni miongoni mwa watu 50 waliokamatwa kwa ujangili na Kikosi Kazi cha Taifa katika Pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkasi katika Mkoa wa Rukwa.
Padri aliyekamatwa ni wa Parokia ya Kirando katika mwambao wa Ziwa Tanganyika, ambaye bunduki yake aina ya Rifle yenye darubini inadaiwa kutumika katika ujangili ndani pori hilo la Lwafi wilayani humo.
Taarifa za kipolisi zimeeleza kwamba, mbali ya kukamatwa kwa watu hao, pia jeshi hilo limekamata bunduki 48 za aina mbalimbali ikiwemo ya Padri huyo anayoimiliki kihalali, pamoja na risasi 764 na maganda ya risasi 101.
Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Jacob Mwaruanda amesema kuwa baadhi ya waliokamatwa silaha zao wanazimiliki kihalali lakini zinatumika kinyume na utaratibu wa kumilikishwa kwao.
"Watu hawa bado wanahojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake," alisema Kamanda Mwaruanda.
Kamanda Mwaruanda alisema kati ya bunduki 48 imo moja ya kivita aina ya AK47, bunduki 8 aina ya Rifle na risasi zake 83, Shortgun 19 na risasi zake 138, bastola 5 na risasi zake 133, magobore 15, magazine nne za bunduki aina ya Sub-Machine Gun, maganda matano ya bunduki aina ya Rifle, maganda 96 ya risasi za bunduki ya shortgun pamoja na vifaa vya kutengenezea bunduki za kienyeji na mitutu sita.
Watuhumiwa hao walikamatwa pia na nyara za serikali ambazo ni mikia sita ya tembo, nyama ya nyati kilo 20, miba ya nungunungu, ngozi moja ya paka-pori na pembe ya Nshya.