Tusahau kuindoa CCM kupitia ballot box

Tusahau kuindoa CCM kupitia ballot box

Nguvu?
Kwa maana ipi?
Uungwaji mkono na raia au kutumia mabavu , hila, fitna na majeshi kubaki madarakani[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]

Au kuendelea kuidunisha Tanganyika na Tanzania kwa ujumla bila kuja na mipango mkakati wa kuwakwamua raia?

Kuendelea kubakia na mamlaka kwa kila njia na kuwa mkoloni mweusi?
Kwani hujui nguvu ya chama cha siasa? Unataka nianze kukufundisha vitu hivi vidogo vya chekechekea?
 
..Je, tulijikomboa ili Tanu na baadae Ccm ije ifanye ukatili dhidi ya wengine?

..Ukatili wa Ccm dhidi ya wapinzani sio unyama?

..Kwanini sheria zinafanya kazi dhidi ya wapinzani tu, na hatuoni Ccm wakichukuliwa hatua kupitia sheria hizo?

..Hivi inaingia akilini sheria ya uchaguzi kwa miaka 30 imeengua maelfu ya wagombea wa upinzani, lakini haijawahi kuengua mgombea hata mmoja wa Ccm?!

..Kwa maoni yangu sheria hiyo ni ya kinyama, au wanaoitekeleza na kuisimamia wana tabia za kinyama.
Ukatili upi umefanyiwa?
 
Lengo ni kushika Dola hatukatai
Ila nini malengo baada ya kushika Dola?
Vipi ni vipaumbele vyao?

Kwa miaka 60 wamefanikiwa nini?
Maana hata uliokuwa mji wao mkuu ni hovyo hovyo tu.

..kauli mbiu ya Mwalimu Nyerere ktk uchaguzi wa kwanza mwaka 1958 ilikuwa Tanu inataka Wakoloni waondoke kwasababu wametuweka ktk ujinga, maradhi, na umasikini.

..Je, tangu wakoloni waondoke na Tanu na Ccm waingie ujinga, maradhi, na umasikini, umeondoka Tanzania?

..Unaridhika na hali ya nchi kisiasa, kiuchumi, na kijamii, miaka 61 tangu tupate uhuru?
 
Nenda kasome katiba ya CCM utapata majibu yako yote haya. Au unataka nikutafunie?
Hutachelea kusema pia niende nikasome katiba ya Jamhuri ya mwaka 1977

Je yaliyopo kwenye katiba ya Jamhuri wanayatekeleza? Kama katiba hawaifuati ambayo ndio dira ya nchi?

Watafuta na kutekeleza katiba ya chama?
Ambayo Leo hii Makamba mzee kasema wameandika wenyewe na kukengeuka kumtaja bi mkola ndio mgombea pekee?

Kama Katiba ya nchi hawaifuati:
Iliyotoa haki za raia ikiwemo na kujumuika, unataka nikahangaike ili nipate nini?
 
Ukiona inafaa unaweza kuisoma vilevile lakini mimi nimekupatia test ndogo tu ya kusoma katiba ya Chama Dola. Kama unashindwa nitakupatia ABC
 
..kauli mbiu ya Mwalimu Nyerere ktk uchaguzi wa kwanza mwaka 1958 ilikuwa Tanu inataka Wakoloni waondoke kwasababu wametuweka ktk ujinga, maradhi, na umasikini.

..Je, tangu wakoloni waondoke na Tanu na Ccm waingie ujinga, maradhi, na umasikini, umeondoka Tanzania?

..Unaridhika na hali ya nchi kisiasa, kiuchumi, na kijamii, miaka 61 tangu tupate uhuru?
Niridhike wapi?
Kwanza hata hao viongozi wao wa kijani wengi ni wajinga tu wakielezea mambo mbalimbali ya nchi.
 
Niridhike wapi?
Kwanza hata hao viongozi wao wa kijani wengi ni wajinga tu wakielezea mambo mbalimbali ya nchi.
Nashangaa sasa hao unaowaita wajinga ndio wanaokutawala. Sasa CCM na wewe nani mjinga?
 
Ukatili upi umefanyiwa?
..viongozi wa CCM kuishi maisha ya anasa na fahari kwa kodi zetu, huku wananchi wakiteseka ktk umasikini sio ukatili?

..wapinzani kuwekwa mahabusu bila makosa sio ukatili?

..viongozi wa upinzani na wafuasi wao kufunguliwa kesi na kufungwa kwa mashtaka ya uongo sio ukatili?

..viongozi na wafuasi wa upinzani kutekwa, kushambuliwa, kupigwa marisasi, sio ukatili?

..kuzuia mikutano ya vyama vya upinzani huku ya Ccm ikiruhusiwa sio dhuluma, sio ukatili?
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Je kuwekwa mahabusu ndio ukatili?
Kesi gani wamefunguliwa? Mbona Mbowe amewafungulia akina Halima Mdee?
Kwahiyo Mbowe ni katili dhidi ya wanawake?
Hakuna haki kwenye katiba imesema kufanya mikutano.
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Mzee akili ulizonazo zinakutosha wewe pekee yako. Usijifananishe na wengine. CCM ni chama dola. Kinatumia akili kubwa kukufanya wewe uwe hapo ulipo.
 
Nguvu?
Kwa maana ipi?
Uungwaji mkono na raia au kutumia mabavu , hila, fitna na majeshi kubaki madarakani[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Sasa hayo unayasema wewe. Lakini nilichokuambia kuwa hakuna chama chenye nguvu kupita CCM hapa barani Africa. Mengine unayoyasema ni nyongeza tu.
 
Nashangaa sasa hao unaowaita wajinga ndio wanaokutawala. Sasa CCM na wewe nani mjinga?
Bado mjinga atabaki kuwa mjinga tu.

Wapo madarakani sio kwa nguvu ya hoja Bali kwa mambo mengine ambayo ninyi chama dola mnayajua na kuyafanya.

Wapo madarakani sio kwa lengo la kuipeleka m ele nchi Bali kwa ajili ya matumbo yao yaani yeye na kizazi Chao.

Wapo madarakani kwa sababu ya kundi kubwa la Watanzania ni wajinga na kushindwa kung'amua mambo.
 
Mzee akili ulizonazo zinakutosha wewe pekee yako. Usijifananishe na wengine. CCM ni chama dola. Kinatumia akili kubwa kukufanya wewe uwe hapo ulipo.
Unaelewa hata maana ya akili kubwa?
Hakuna akili kubwa itumikayo Bali nguvu na mabavu.

Ndio maana ya kujiita chama dola
 
Sasa hayo unayasema wewe. Lakini nilichokuambia kuwa hakuna chama chenye nguvu kupita CCM hapa barani Africa. Mengine unayoyasema ni nyongeza tu.
Na Mimi nakwambia CCM halina nguvu hasa inazotakiwa iwe nazo kama chama Cha siasa.
 
Je kuwekwa mahabusu ndio ukatili?
Kesi gani wamefunguliwa? Mbona Mbowe amewafungulia akina Halima Mdee?
Kwahiyo Mbowe ni katili dhidi ya wanawake?
Hakuna haki kwenye katiba imesema kufanya mikutano.

..kuwekwa mahabusu kwa kesi ya kusingiziwa ni ukatili.

..ukiacha viongozi kama Mbowe, Mdee, Sugu, Lijualikali, kuna wanachadema zaidi ya 400 waliokuwa wamefungwa au kushtakiwa kwa kesi za kusingiziwa. Je huo sio ukatili?

..Wilaya ya Tunduma peke yake kulikuwa na makesi au wafungwa waliobambikiwa kesi zaidi ya 80. Huo sio ukatili?

..Ccm walimfungulia kesi Halima Mdee, Esther Bulaya, na Esther Matiko. Waliwapiga na kuwafunja mikono. Hata wakoloni hawakuwa wakatili kwa wanawake wa Tanu kiasi hicho. Hatukuwahi kusikia Bibi Titi kapigwa na askari wa Wakoloni.

..Vilevile, hoja kwamba Mbowe kamshtaki Halima Mdee umeitoa wapi? Kesi iliyopo mahakamani imefunguliwa na Mdee dhidi ya Chadema.
 
Bado mjinga atabaki kuwa mjinga tu.

Wapo madarakani sio kwa nguvu ya hoja Bali kwa mambo mengine ambayo ninyi chama dola mnayajua na kuyafanya.

Wapo madarakani sio kwa lengo la kuipeleka m ele nchi Bali kwa ajili ya matumbo yao yaani yeye na kizazi Chao.

Wapo madarakani kwa sababu ya kundi kubwa la Watanzania ni wajinga na kushindwa kung'amua mambo.
Sasa kama wameweza kuwa madarakani kukuzidi wewe mwenye akilli. Maana yake huna mbinu za kuwazidi. Wewe endelea tu kuwa na akili hizo maana zinakutosha wewe pekee yako.
 
Back
Top Bottom