Tutafika kama Taifa kwa aina ya “vijana wa ovyo” tulionao?

Mitanzania ni mijinga totally kuanzia Mimi unafuatia wewe na wengine wote.
 
kwa hyo mleta mada unataka tubebe mapanga na mashoka tuingie mtaani?
Au una shauri nini?
 
Vijana wote wamelelewa na wazee wao, kwa hiyo kama kuna lawama, anza na wazee waliowalea.
 
Mambo ya nchi pambana nayo wewe ambaye ni masikini usilazimishe Kila mtu ajiangaishe na ujinga
 
Damn inasikitisha sana bro. Niko around watu ambao wanajadili upuuzi mtupu. Kila ukiwakuta ni chama, sijui mkulu yanga simba. Hawajui hata kama kuna siku ya vijana duniani. Hawajui hata kama Mbowe yupo cell, hawajui hata kama Biteko amesababisha usumbufu Geita kisa msafara. Hawajui hata saa hii presda yupo kwa tolu.

Ni kelele
 
watawala walishaligundua hilo mapema wakaamua kusomeaha watoto wao shule nzuri wakaamua kuishi kifahari na wanajua wanapotoa tshirt na kanga mchezo umekwisha...

tz kamwe hatuwezi kubadilika maana hatutaki kubadilika ni ngumu maiti kufufuka mkuu maana hata tukisema gen z (gen hovyo) wa hapa wana maono gani utakuta ni bhange mirungi pombe wanawake sasa jamii ya hivi haiwezi jua thamani ya bandari ngorongoro wala mali yoyote tuliyonayo....
 
Mzee kwani Kuna mtu ulie kuja nae hapa duniani mbona unalaumu watu Kwa umasikini wako wakati watu wanaishi maisha yao
 
Wewe ni Mtanzania? Naona kama unaandika kiswahili cha Kikenya!
 
Ili watanzania tuwe na akili unataka tuletewe bunduki tuingie mitaani.?
Au unashauri nini?msiishie tu kulaumu.
Mtoe NA SULUHISHO.ndo mtaonekana mna akili
mkuu kwa mifumo kandamizi tuliyo nayo ukitoa suluhisho watawala wanaona nyani huyu kayachoka maisha ya kwenye zoo
 
Ishi maisha Yako mzee hamna mtu uliekuja nae duniani Kila mtu kaja kivyake
 
How are we going to change that?
Hayo mambo hayabadiliki kirahisi, japo wengi hawapendi kusikia lakini ukweli ni kwamba wakati mwingine mabadiliko nayo ni bahati, kuna siku inawezekana watu aina ye Lee Kuan Yew wanaweza kubahitika kushika mpini mambo yakabadilka kabisa

Mazingira pia yanabadilika, japo ni suala la muda mrefu sana lakini rasilimali nyingi tulizo nazo zitapungua sana na kuondoa faida ya rasilimali inayowafanya watu kuwa relaxed, hapo itawalazimu wengi kutumia bongo zao zaidi kuendesha maisha

Historia na tamaduni navyo vinabadilika kutokana na athari ya mabadiliko ya nje, migration za watu, kubadilika kwa makundi ya umri(demographic shifts)
 
Mkuu kuna vitu viwili ukijaribu kufanya katika hili taifa ni sawa na KAZI BURE.
1)Uzalendo.
2)Siasa safi/uadilifu.
Hili taifa halina shukurani na wala halieleweki.Jikute mzalendo tukuokote kwa Kiroba ama jikute muadilifu tukuzike.
Usidhani kama watu hawaoni ama hawasikii ama hawajui Madudu yanayoendelea,ila swali ni je wakiamua kuchukua hatua yatasikilizwa hayo madai yao na effort zao zitakua productive!!??
Kwa bongo hii jibu ni BIG NO,ndio maana unaona raia wanaamua kuridhika na maisha muhimman wanapata ugali kwa amani maisha yanaendelea.
Hata wewe nakushauri masuala ya uongozi wa hili taifa achana nayo,jitafutie ugali tena ukifanikiwa ikiwezekana hama hata nchi ama hama Afirka kiujumla.
Jirani zetu Kenya hao hapo zaidi ya mwezi mmoja wameandamana na mamia ya vijana kufariki hadi mwandishi wa habari kufariki ila maandamano hayakuzaa matunda.
Halafu BANGLADESH WATU wameandamana Wiki moja tu wamemtoa waziri mkuu Sheikh Hasina madarakani,wakati wanaandamana wanajeshi na polisi walikataa kuungana na waziri mkuu wakaungana na raia.
Ila Afrika is differente.
Kaka tubakie tu kuzungumzia Simba na Yanga.
 
Ili watanzania tuwe na akili unataka tuletewe bunduki tuingie mitaani.?
Au unashauri nini?msiishie tu kulaumu.
Mtoe NA SULUHISHO.ndo mtaonekana mna akili
Mleta Uzi kaeleza wazi kuwa hatudili na mambo ya msingi japo tunakandamizwa na kubwa lkn hayo hatuna habar nayo.......... Anasema tuna Dili na mambo ya hivyo yasiyokuwa na tija Wala kuleta mabadiriko.

Anakiri wazi kuwa tupo busy kumfuatilia Simba na yanga
Diamond na harmonize nk isipokuwa mambo ya msingi

Hadi hapo unataka Nini mkuu?
Bado hujajijua shida iliyopo?

Je vibopa waendelee kula Mali za uma watakavyo?

Je hizi Kodi ni halali?

CAG Kila anapotoa list ya mbalioni kupoibwa na mengine kupotea na wahusika bila kuchukiliwa hatua ni sahihi?

Je kuandamana Kwa amani kudai haki Zenu ni kosa?

Wingeleza hawafanyi hivyo na kwingine kote?
 
Hatuwezi enda mbele. Tuamke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…