#COVID19 Tutegemee nini baada ya Rais Samia kusema 'Gwajiboy oyee Tunachanja, hatuchanji' mbele ya Askofu Gwajima?

#COVID19 Tutegemee nini baada ya Rais Samia kusema 'Gwajiboy oyee Tunachanja, hatuchanji' mbele ya Askofu Gwajima?

Uzuri ni kuwa wengi wao wakiugua wataishia kwa waganga ambao watawaambia wamelogwa au kwa wakina Gwajima ambao watawafufua hata kama watakufa.

Amandla...
 
Leo wakati Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akielekea Bagamoyo kurecord filamu ya kutangaza utalii wa Tanzania alisimama kwenye jimbo la Kawe ili kusalimia wananchi.

Rais alimsimamisha Mbunge wa Kawe ili kutoa neno lakini kabla ya kumsimamisha aliwauliza wananchi wa Kawe kama watachanja au la kama video inavyoonyesha hapa chini.Katika hali ya kustaajabisha na ya kushangaza wananchi walimwambia Rais bila ya kupepesa macho kuwa hawatachanja kama video hii inavyoonyesha hapa chini.

Nimejiuliza maswali mengi sana.Kwa nini Rais aulize swali hilo kwenye jimbo ambalo mbunge wake hakubaliani na mambo ya chanjo?Ina maana Rais hajui kwamba kazi kubwa ambayo walifanya katika awamu ya tano ya kupinga chanjo ilifanikiwa sana hasa ukizingatia kuwa kazi hiyo ilifanyika katika Taifa lenye umasikini mkubwa sana wa akili?

My take:
Kwa sasa hivi serikali ya CCM inapata shida sana kula matapishi yake yenyewe ambayo waliyatapika katika awamu ya tano.Ni vyema serikali ikiri mbele ya wananchi kuwa Rais Magufuli hakuwa sahihi na alipotosha sana uma ili wananchi waanze upya kuelimishwa juu ya gonjwa la Corona na chanjo.

Ndugai anajisikiaje uko aliko?
 
Na Mh Gwajima alipopewa kuongea kaonesha heshima kwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu. Yeye hakutaka kugusia lolote kuhusu chanjo maana alijua Rais tayari kapata jibu stahiki kutoka kwa wananchi anao waongoza. Na Mh Rais ajiongeze huko mbele ya safari wataulizwa kuhusu faida ya fedha walizozipeleka au watakazo zipeleka kwenye hii chanjo ya corona. Ni bora akaanza kutafuta majibu yake mapema.
 
Leo wakati Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akielekea Bagamoyo kurecord filamu ya kutangaza utalii wa Tanzania alisimama kwenye jimbo la Kawe ili kusalimia wananchi.

Rais alimsimamisha Mbunge wa Kawe ili kutoa neno lakini kabla ya kumsimamisha aliwauliza wananchi wa Kawe kama watachanja au la kama video inavyoonyesha hapa chini.Katika hali ya kustaajabisha na ya kushangaza wananchi walimwambia Rais bila ya kupepesa macho kuwa hawatachanja kama video hii inavyoonyesha hapa chini.

Nimejiuliza maswali mengi sana.Kwa nini Rais aulize swali hilo kwenye jimbo ambalo mbunge wake hakubaliani na mambo ya chanjo?Ina maana Rais hajui kwamba kazi kubwa ambayo walifanya katika awamu ya tano ya kupinga chanjo ilifanikiwa sana hasa ukizingatia kuwa kazi hiyo ilifanyika katika Taifa lenye umasikini mkubwa sana wa akili?

My take:
Kwa sasa hivi serikali ya CCM inapata shida sana kula matapishi yake yenyewe ambayo waliyatapika katika awamu ya tano.Ni vyema serikali ikiri mbele ya wananchi kuwa Rais Magufuli hakuwa sahihi na alipotosha sana uma ili wananchi waanze upya kuelimishwa juu ya gonjwa la Corona na chanjo.

Acha zako hizo wewe. Kama kuchanja ni hiari na wao hawachanji kuna ubaya gani. Yote hiyo kutaka kuonyesha anti zako kwa magufuli. Mwenyewe alisema kama ni chanjo lazima tuzichunguze na kuona kama ni salama kwanza wala hakukataa. Ila vibaraka na maagent wa ubeberu wenye kukubali kwa furaha kila wakiambiwa kitu na wazungu bila kujiridhisha kama hamna hila ndio wanajidai wanajua saaana.
 
Uzuri ni kuwa wengi wao wakiugua wataishia kwa waganga ambao watawaambia wamelogwa au kwa wakina Gwajima ambao watawafufua hata kama watakufa.

Amandla...
KWANI kuna shida gani ni haki ya kidemokrasia ya mtu kuamua tatizo lake likatatuliwe wapi iwe kujifukiza or whatever kama anaona yeye kama yeye vinamsaidia wewe kinakusumbua nini?

Ni sawa na kusema ohh kuna makanisa wanapeli watu pesa tu wakati wewe husali huko na hao unaosema wanatapeliwa hawajawahi kufungua kesi popote kuwa wametapeliwa na unasahau kuwa mtu akishajipatia pesa yake yuko huru kuitumia atakavyo aweza lewea,kuhonga malaya au kumpa tapeli ni pesa yake wewe kinakuuma nini? mfano mtu kapata mshara wake kodi yako umeshachukua bado unaendelea kumfuta eti hiyo hela kwa nini apeleke kwa Gwajima au mchungaji fulani tapeli.Yanakuhusu nini? hizo ni private affair zake.Kwa hiyo utataka hata kufuatilia akienda kuhonga kuwa kwa nini unaenda kuhonga malaya? Huo ni ukorofi usiokuwa na sababu

Kila mtu aheshimu imani ya mtu mwingine
 
Ni kweli, lakini nanyi mkubali kwamba HAMJUI KUWA HAMJUI, NDIO MAANA MNADANGANYWA !!
Wewe mtanzania unajua nini kuhusu chanjo zilizotengenezwa Ulaya? Unaelimu yoyote kuhusu chanjo? Kama hauna vyote hivyo, hata wewe ni wale wale bendera fata upepo.

Si ajabu mpaka Sasa bado haujachanjwa.
 
Ndiyo tatizo la Serikali yetu kutotaka kusikiliza wananchi kwa miaka mingi! Inasikiliza wanasiasa badala ya wananchi.
Hayo ndiyo majibu sasa!
 
Back
Top Bottom