Leo wakati Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akielekea Bagamoyo kurecord filamu ya kutangaza utalii wa Tanzania alisimama kwenye jimbo la Kawe ili kusalimia wananchi.
Rais alimsimamisha Mbunge wa Kawe ili kutoa neno lakini kabla ya kumsimamisha aliwauliza wananchi wa Kawe kama watachanja au la kama video inavyoonyesha hapa chini.Katika hali ya kustaajabisha na ya kushangaza wananchi walimwambia Rais bila ya kupepesa macho kuwa hawatachanja kama video hii inavyoonyesha hapa chini.
Nimejiuliza maswali mengi sana.Kwa nini Rais aulize swali hilo kwenye jimbo ambalo mbunge wake hakubaliani na mambo ya chanjo?Ina maana Rais hajui kwamba kazi kubwa ambayo walifanya katika awamu ya tano ya kupinga chanjo ilifanikiwa sana hasa ukizingatia kuwa kazi hiyo ilifanyika katika Taifa lenye umasikini mkubwa sana wa akili?
My take:
Kwa sasa hivi serikali ya CCM inapata shida sana kula matapishi yake yenyewe ambayo waliyatapika katika awamu ya tano.Ni vyema serikali ikiri mbele ya wananchi kuwa Rais Magufuli hakuwa sahihi na alipotosha sana uma ili wananchi waanze upya kuelimishwa juu ya gonjwa la Corona na chanjo.