Uchaguzi ni sayansi: Lissu anaenda kugaragazwa vibaya sana na Mbowe

Uchaguzi ni sayansi: Lissu anaenda kugaragazwa vibaya sana na Mbowe

Napenda lisu awe kiongozi, lakini , uchaguzi huu lisu atashindwa, anatumia mkwara wa kelele, kwenye vyombo vya habari, lakini kikubwa najua lisu utashindwa Ila usikimbie chama , ubaki kuimarisha chama.

Naona lisu anajua kwamba anaenda kushindwa,Sasa Kuna mazingira anayaanda ionekane kushindwa kwake kuwa ni mizengwe,mfano:-

1. Rushwa imetamkwa kutoka mdomoni mwa lisu kuwa chaguzi za CHADEMA zimegubikwa na Rushwa,Rushwa,hii yote ni kujenga mawingu yenye mwangwi wa radi ,ku justify kuonesha ameenguliwa kwa sura ya kukichafua chama na mwenyekiti,hivyo ili cama kiwe Safi na ili wakinusuru chama,inabidi Lisu ashindwe,hiyo ni ngao anayojaribu kuijenga lisu kwenye jamii ,ili akishindwa apate utetezi
2.Kelele za Lisu na mkwara wa lisu kupitia Media,bila shaka nguvu ya mbowe bado ni kubwa Sana,ndani ya chama,Sasa anachokifanya Lisu ni sawa na mbwa kumbwekea fisi,lakini fisi akijitikisa kidogo tu huyu mbwa anatimua mbio Hadi vumbi linatimka.

3.Bado naona mbowe Yuko strong,mkwara w kwenye midia unaotolewa na Lisu haujamtisha mbowe, mbowe ni mpambanaji Sana katika siasa hizi za kuchaguliwa,

Mwisho,sipendi kumkosa lisu katika Safi za upinzani Bora wa Tanzania
Wewe ni mpigakura?
 
Tunajua kabisa Mbowe atasaidiwa na Samia kwa kutumia fedha za waarabu na vyombo vya usalama. Tunajua kuwa mpaka TISS itatumika ili tu Lissu asishinde. Hii ni kwa sababu Mbowe ameshapewa fedha nyingi na Samia ili CHADEMA isipige kelele wakati waarabu watakapokuwa wanapora raslimali zetu na pia CHADEMA isimpe Samia ushindani kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani. Tusibiri tuone mwisho wake.
Lissu mlimchangia anunue gari lipo wapi? Na alochangiwa mpka na CCM . Subiri utayajua mengi
 
Kataka mwenyewe huyu chizi fresh. Acha afunzwe adabu.
Sijaona uchizi wa yeyote, huo ni mtazamo wako Mimi naamini kuwa chadema wanapaswa kutumia wakati huu ambao watanzania wengi wana waangalia kuonyesha kuwa chadema sio Chama Cha MTU na Kila mwanachama ana Haki ya kugombea nafasi yeyote. Pia Mbowe huu ungekuwa wakati mzuri wa kuwaonyesha wapinzani wake kuwa yeye sio kin'gan'ganizi wa madaraka na Chadema sio saccos ila ni tasisi ya wananchi
 
Lissu mlimchangia anunue gari lipo wapi? Na alochangiwa mpka na CCM . Subiri utayajua mengi
Hili ndilo jambo unalotaka kunirusha nalo roho? Fedha za gari bado zipo na siku si nyingi tunaanza tena mchango mpaka kiwango tulichopanga kitimie. Unadhani Lissu ni mroho wa fedha kama kina Wenje na Mbowe waliofikia hatua ya kumpeleka Abdul nyumbani kwa Lissu ili kumshawishi apokee fedha za hongo kama wao? Na ushahidi upo wa video upo.
 
View attachment 3175794

Tundu Lissu ni baba aambiliki nilimuonya hapa majuzi aache mission yake ya kukiua chama hajataka kusikia.

Sasa anaenda kufundishwa adabu na bingwa wa sayansi ya siasa za upinzani Aikael Mbowe.

Kelele ni nyingi mtandaoni lakini hazitomsaidia Lissu na kichapo cha mbwa mwizi toka kwa Mbowe.

Lissu ana wapiga kelele haswa wa mtandaoni, Mbowe ana wapiga kura. Mpaka hapo nani anaenda kushinda?

Uchaguzi wa Chadema una wajumbe wa mkutano mkuu wanakaribia 1300 ambao wana vigezo vya kupiga kura.

Mpaka hapo nafikiri mnaelewa kwa nini Lissu alikuwa anatoa milio mingi kwenye chaguzi zilizokuwa zinaendelea kwa sababu anajua Mbowe alikuwa anapanga safu yake ya kumpigia kura. Yani Mbowe mpaka sasa ana wapiga kura wa kutosha.

Kilichobaki ni Lissu kunyolewa bila maji then akimbie chama kwa hasira yeye na wapiga kelele wenzake.

Baada ya hapo Mbowe ataisuka upya Chadema yake na kurecruit damu mpya nyingi za vijana watiifu wafanya siasa sio harakati.

Lissu anasema uchawa kwenye chama haufai wakati yeye ndio alikuwa chawa namba moja wa Mbowe. Zitto na Kitila wanafukuzwa Lissu ndio kijumbe yupo pembeni ya Mbowe anatoa ushauri wa kisheria.

Dr Slaa anakimbia Chadema, Lissu yupo pale anamnyoosha Dr Slaa.

Yeye ndio alikuwa mastermind wa kuondoa ukomo wa uongozi kwa kuwa alikuwa ananufaika leo anawadanganya chama hakikuwa na watu.

Nasemaje Lissu anatakiwa apigwe vizuri mpaka hata hicho chama anachotaka kuanzisha aghairishe arudi kula pensheni ubeligiji.

Sababu ni moja ni TRAITOR.

Alimsaliti JPM mkamshangilia.

Amefanya kwa Mbowe kipenzi chenu.

Amesaliti watu wengi sana ili yeye ajenge jina lake kwamba anaipenda Tanzania kuliko kiumbe yoyote.

Mimi sio shabiki wa Mbowe ila watu kama Lissu wenye kelele nyingi na hekma sifuri hawatakiwi kuongoza taasisi yoyote. Chadema ipo hapo ilipo kwa vingi ikiwemo hekma za Mbowe. Mbowe ni Nigga ila ni kiongozi mara 200 kumzidi Lissu.
Wewe nani kwani na umetoka wapi...?

Unafikiri Freeman Mbowe ni mjinga na mpumbavu kama ulivyo wewe na fikra zako hizi kuwa anaweza kuua chama hiki kwa sababu ya madaraka...?

BY THE WAY;

Mbona kama unanuka harufu ya Chawa wa CCM ya Lumumba na Chimwaga Dodoma wewe...?

Si siku zote mmetaka Freeman Mbowe aondoke kwa sababu ni mng'ang'ania madaraka...?

Si siku zote Chawa mlikuwa mnasema CHADEMA hakuna succession plan ya uongozi na Freeman Mbowe ni CHADEMA na CHADEMA ndiye Freeman Mbowe...?

Mbona mnabweka tena kwa huyuhuyu Freeman Mbowe ambaye ameshaanda mrithi wake na aliyemwandaa kwa siku nyingi Tundu Lissu arithi kiti chake...?

Au hujui kuwa huu ni mpango mkakati wa chama kwamba Tundu Lissu ndiye Mwenyekiti ajaye wa CHADEMA?

Na hata hujui kuwa Freeman Mbowe ndiyo hivyo anastaafu na hatagombea...?

SIKILIZA BWANA. USITULETEE MAMBO YA SHETANI HAPA NA WAKALA WAKE HAYATI JOHN POMBE MAGUFULI...

Tunafahamu kuwa CCM hawakutarajia kuwa Tundu Lissu ndiye atachukua nafasi ya Freeman Mbowe...

Tunafahamu kuwa, CCM wasingependa kumwona huyu mtu akiongoza chama hiki...

Tunafahamu pia kuwa, mpango mkakati TISS - CCM na serikali yenu kwa ujumla ilikuwa ni kumzodoa Freeman Mbowe kuwa ni mng'ang'ania madaraka, ajione hafai, wanachama wamchukie kisha vurugu na magomvi yatokee ndani ya CHADEMA na kisha TISS waisaidie CCM kuweka mamluki kuongoza CHADEMA kama Mwenyekiti Ili mkipige na kukiua chama hiki kama mlivyofanya kwenye vile vyama mamluki vingine NCCR Mageuzi na CUF...

Sasa mpango huu umefeli spectacularly. Hamkujua mipango mikakati ya CHADEMA kuwa ni kumleta asiyetakiwa na CCM, mzimu wenu mliotaka kumuua kwa risasi mwaka 2017...

CCM, kama mnafikiri mnaweza, basi tunawashauri njooni na plan C maana plan A & B za kuivuruga CHADEMA Ili idhoofu zote zimeshafeli tayari....

Aidha Tunafahamu kuwa CCM hawapendi na msingependa kuona Tundu Lissu anasimama kugombea u - Rais na mama yenu Bi Kizimkazi hapo mwakani 2025...

Hayo yote tunayafahamu.....

Lakini Iko hivi: MSIYEMPENDA NDIYO HUYO ANAKUJA VYUMBANI MWENU. SAFISHENI VIWE SAFI. OTHERWISE KAENI MKAO WA KUPOKEA ADHABU...
 
Sijaona uchizi wa yeyote, huo ni mtazamo wako Mimi naamini kuwa chadema wanapaswa kutumia wakati huu ambao watanzania wengi wana waangalia kuonyesha kuwa chadema sio Chama Cha MTU na Kila mwanachama ana Haki ya kugombea nafasi yeyote. Pia Mbowe huu ungekuwa wakati mzuri wa kuwaonyesha wapinzani wake kuwa yeye sio kin'gan'ganizi wa madaraka na Chadema sio saccos ila ni tasisi ya wananchi
Ulitaka Lissu apite bila kupingwa?
 
Kwa nini lissu achukuliwe kama adui kwa kutaka kuwa mwenyekiti wakati katiba ya chama inaruhusu.

Kwani CHADEMA ni mali binafsi au ya wananchi
Na Mimi nashangaa, wasipofanya uchaguzi wanasema CHADEMA hakuna demokrasia ,mbowe dikteta, haya chaguzi unataka kufanyika wanajitokeza watu wakugombea mnapiga kelele, mnasema hawafai na BAHATI MBAYA MAKADA WACHAMA FULANI NDIO WANAONGAZA KAMPENI YA LISU HAFAI kwani anagombea kwenu?
 
Hili ndilo jambo unalotaka kunirusha nalo roho? Fedha za gari bado zipo na siku si nyingi tunaanza tena mchango mpaka kiwango tulichopanga kitimie. Unadhani Lissu ni mroho wa fedha kama kina Wenje na Mbowe waliofikia hatua ya kumpeleka Abdul nyumbani kwa Lissu ili kumshawishi apokee fedha za hongo kama wao? Na ushahidi upo wa video upo.
Lissu anaenda kupigwa kwenye sanduku la kura kelele zozote zile hazitomsaidia ashaelekezwa kibra
 
Kama Uchaguzi ni Sayansi mbona huyo Mama na Mkwe wake wanaiba na kuharibu Chaguzi au wao sio Wanasayansi?
 
Hiyo si ndio demokrasia, wasipogombea shida wakigombea shida, tatizo nini?
 
Lissu anaenda kupigwa kwenye sanduku la kura kelele zozote zile hazitomsaidia ashaelekezwa kibra
Note: Ni ''kibla'' na siyo kibra. Tunajua kabisa Mbowe aliweka machawa yake wengi kwenye nafasi za wilayani, mikoani na kanda wakati wa uchaguzi kwa kutumia fedha kutoka kwa Abdul. Tunajua kabisa kuwa Mbowe anaendesha CHADEMA kama familia yake na yupo hapo kwa faida yake. Tnajua kabisa kuwa Mbowe ana makubaliano na Samia na vijana wa CHADEMA kama kina Soka ni yeye alitoa idhini wakamatwe. la kuna jambo moja. Siku zake za kujificha kwenye kivuli cha ''mwamba tuvushe'' zinafika ukingoni na mwisho wake utakuwa ni wa aibu sana.
 
View attachment 3175794

Tundu Lissu ni baba aambiliki nilimuonya hapa majuzi aache mission yake ya kukiua chama hajataka kusikia.

Sasa anaenda kufundishwa adabu na bingwa wa sayansi ya siasa za upinzani Aikael Mbowe.

Kelele ni nyingi mtandaoni lakini hazitomsaidia Lissu na kichapo cha mbwa mwizi toka kwa Mbowe.

Lissu ana wapiga kelele haswa wa mtandaoni, Mbowe ana wapiga kura. Mpaka hapo nani anaenda kushinda?

Uchaguzi wa Chadema una wajumbe wa mkutano mkuu wanakaribia 1300 ambao wana vigezo vya kupiga kura.

Mpaka hapo nafikiri mnaelewa kwa nini Lissu alikuwa anatoa milio mingi kwenye chaguzi zilizokuwa zinaendelea kwa sababu anajua Mbowe alikuwa anapanga safu yake ya kumpigia kura. Yani Mbowe mpaka sasa ana wapiga kura wa kutosha.

Kilichobaki ni Lissu kunyolewa bila maji then akimbie chama kwa hasira yeye na wapiga kelele wenzake.

Baada ya hapo Mbowe ataisuka upya Chadema yake na kurecruit damu mpya nyingi za vijana watiifu wafanya siasa sio harakati.

Lissu anasema uchawa kwenye chama haufai wakati yeye ndio alikuwa chawa namba moja wa Mbowe. Zitto na Kitila wanafukuzwa Lissu ndio kijumbe yupo pembeni ya Mbowe anatoa ushauri wa kisheria.

Dr Slaa anakimbia Chadema, Lissu yupo pale anamnyoosha Dr Slaa.

Yeye ndio alikuwa mastermind wa kuondoa ukomo wa uongozi kwa kuwa alikuwa ananufaika leo anawadanganya chama hakikuwa na watu.

Nasemaje Lissu anatakiwa apigwe vizuri mpaka hata hicho chama anachotaka kuanzisha aghairishe arudi kula pensheni ubeligiji.

Sababu ni moja ni TRAITOR.

Alimsaliti JPM mkamshangilia.

Amefanya kwa Mbowe kipenzi chenu.

Amesaliti watu wengi sana ili yeye ajenge jina lake kwamba anaipenda Tanzania kuliko kiumbe yoyote.

Mimi sio shabiki wa Mbowe ila watu kama Lissu wenye kelele nyingi na hekma sifuri hawatakiwi kuongoza taasisi yoyote. Chadema ipo hapo ilipo kwa vingi ikiwemo hekma za Mbowe. Mbowe ni Nigga ila ni kiongozi mara 200 kumzidi Lissu.
Ni wazi Lissu atashindwa na pia ni wazi hatakubali kushindwa atatoa visingizio vya rushwa na blah blah zingine. Kisha atahama chama hawezi anzisha chama maana itakuwa vigumu kupata usajili.

Atatimkia ACT, huko watampa fursa ya kugombea ili awapatie wabunge na ongezeko la ruzuku, pia huko hataupata urais wa Tanzania ila atakuwa ameifaidisha ACT . Hicho ndicho mnafiki Zitto anachobet.

Kisiasa ukichanganya na umri kusogea na ulemavu ndio itakuwa ameanza mwisho wake kisiasa.

Hata hii hoja ya kusema no reforms no election haiwasaidii kwa sababu sheria za vyama ni rahisi msajili kukifuta chama kinachotumia nguvu kufikia malengo yake. Pia ili chama kifanikiwe kutumia nguvu lazima wafuasi wake wawe tayari kujitoa mhanga, kwa Tanzania hiyo haipo kama maandamano tu watu wanashindwa kujitokeza sembuse kuzuia uchaguzi kwa mabavu.

Ili mwanasiasa yeyote awe na impact lazima awe na watu ambao wako tayari kujitoa mhanga kwa ajili yake, Tanzania hapa hakuna mwanasiasa hata mmoja mwenye watu zamani walikuwa wanasiasa wawili tu ambao ni Nyerere na Maalim Sefu basi. Kenya wanafanikiwa kwa sababu kila mwanasiasa kule ana watu anaoweza kuwacommand wakafanya jambo.

Tanzania kuna mashabiki wa mtandaoni kwa kutumia key board tu.
 
Back
Top Bottom